Maisha magumu sana ila nina imani ipo siku nitafanikiwa

Mkuu acha kukata tamaa ya maisha.. 7 elfu kwa siku Ni ndogo na inapatika na zaidi... Ila unahitaji kuchanganya akili kwa haraka na kuepuka kuchagua kazi.. je unajua kuendesha gari.. bike.. au bajaji. Je una driving lesen

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, kwa bahati mbaya sijajifunza kuendesha chombo chochote cha usafiri,ila nina malengo ya kujifunza .
 
Tatizo wimbi la vijana matapeli na walagai Ni wengi Sanaa,wanakujagaa na sura za onyongee na maneno ya kuuzunisha,Ila wakisha saidiwa kishuhuli Ni heri ya nyokaa.kuna jamaa alikuja golini kwangu Kama wiki mbili mfululizo akinieleza maswaibu yanayo mfikaa na jinsi life lilivyo mchapa.sina kipato kikubwa Ila Imani ikaniingia na kunipoza.nikaona kwa vile nikijana mwezangu ngoja niwe na mpaa PRS kazaa za viatu akizungusha hatakosaa Cha juuu.walaaaaah nilivyo mpa sikuwai kumuona tenaa
 
Mi nakosaga mia ila nikikaa kidogo napata maisha kujiua haifai.
 
Niuzie hio simu upate mtaji wa kuuza Apple barabarani
 
Well said......Nime screenshot hii
 
Usichoke kupambana jaribu kila sehemu kuomba ujitolee hata kwa wauza chipsi, wajenzi wa nyumba, na fani zote za chini utapewa chakula cha siku ukizoeleka utaanza kulipwa kwa siku na hatimae utapata uzoefu na utasimama mwenyewe. Usikate tamaa maisha yana mapito mno
 
unamuita baba yako baba jinA?
Heshimu wazazi wako Kwanza hata kama hawakusaidii
 
Pole sana. Naenda sehemu wajengazo Majengo upate kibarua hapo, ujipange. Daily 7,000 utaokoa sana. Acha Mawazo ya kufa. Kuna wenzako wawili wanadegree wanasogeza Tofali kwa fundi, vyeti kaacha home. Maisha yanaendelea
 
Yani humu hakuna hata mtu wa kumpa mchogo jamaa awe anapate hata hiyo buku 7?
 
Kuwa na mawazo kama haya wewe tayari ni tajiri bigup watu hujua thamani ya walichonacho pindi kinapotoweka ni hivyo tu. Unaweza kulalamika huna pesa ili hali familia yako ni wazima kuna wenye mali lakini zinaishia kwenye matibabu ya mwanafamilia. Utajiri na umasikini huanzia ndani ya mtu kisha kujidhihirisha katika ulimwengu wa mwili
 
Komaa, tafuta hata miji midogo ambayo gharama za maisha ziko chini ukaanzie huko.
 
Good advice, God be with you today and forever.
 
Mungu Akubariki hii ni comment bora sana bila shaka Uliyeandika ni Mtu mwenye roho nzuri sana Umemaliza kila kitu Mungu ni mwema Atafanya njia pasipo na njia
 
Usikate tamaa mkuu kuna jamaa alimaliza SUA food science and technology alikaa miaka minne ndo akaajiriwa tena sehemu nzuri now ana family maisha yanaenda alishasahau kama alikuwa dereva wa uber jamaa yupo TANZANIA DIARY BOARD kawa kibonge kama pipa

Don't give up
 


mkuu mm najua kuendesha vyote hvyo na nina leseni tafadhal kama kuna kaz naomba niunganishe namba yangu 0687886600
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…