Maisha yanazidi kunichachia kila kukicha, nimetafuta sana kazi bila mafanikio yoyote mpaka ninahisi nimerogwa.
Mtaani thamani yangu imeshuka mno maaana nilipiga hatua kidogo ya kielimu ila nikakosa mtu wa kuniendeleza baada ya kufiwa na mama (baba yupo ila ni baba jina) hivyo nikakata tamaa ya kuandika barua ya ku-postpone maana nilishawahi ku-postpone lakini mambo hayakwenda vizuri hivyo nikaamua kuacha chuo.
Kwa sasa nahitaji angalau kupata kazi niingize japo elfu 7 kwa siku.
Mawazo ya kujiua yananiandama mara kwa mara ila ninapingana nayo kiume. Nina imani ipo siku nitafanikiwa.
Mkuu nilikuwa na shughuli yangu nilikuwa naifanya, nilikuwa natumia nguvu na akili mingi sana, mambo yakaingiliana nikapata kesi ambayo sijui mbele wala nyuma. Yaani jambo limefanywa na mtu mwingine ila mawasiliano yangu kukutwa kwenye simu ya mhusika nikadakwa na Mimi.
Nimekaa mahabusu siku 11 , usiku na mchana nipo polisi, dhamana hakuna aliyetegemea kama ningepata, kesi ni ya jamhuri ndiyo inayonishtaki.
Vifaa vyangu vyote vya kazi vipo polisi. Nina mtoto mmoja na mke, balance yangu iliyokuwepo nilikuwa pesa ya kulipa kodi tu maana nilitegemea kadiri ambavyo ningeendelea na kazi yangu pesa za kutumia zingeendelea kupatikana.
Sina balance yoyote, kodi mwisho ilikuwa December 2020, inatakiwa familia iudumiwe, nitafute pesa ya kodi maana imeisha iliyokuwepo mzee wangu mwenye nyumba hodi na vikao haviishi, mpaka sina kazi yoyote, sijui hatima ya kesi maana naambiwa upelelezi bado unaendelea na kila siku inatakiwa nitoe nauli kwenda kuripoti.
Kuna mengi sana ambayo yanaendelea kwasasa katika maisha ILA mpak sasa mkuu sijakata tamaa bado na nina hustle kutafuta kazi yoyote ili kujikwamua.
December na hii January imekuwa nyakati ngumu sana kwangu.
Ila bado sijakata tamaa.
Mkuu nikuweke wazi tu, wewe huna MATATIZO ila una CHANGAMOTO.
Changamoto zipo kukujenga
Changamoto zipo kukufundisha.
Changamoto zipo kukuonyesha watu wako.
Changamoto zipo kukufunulia yale yaliyojificha.
Changamoto zipo kukuandaa kwaajili ya fursa kubwa zaidi.
Changamoto zipo kukufungua kichwa.
Nyakati ngumu zisikufanye ukate tamaa na kuona ndiyo mwisho wa maisha, hapana. Nyakati ngumu zinakuja pale ambapo unahitajika kuingia hatua nyingine katika maisha hivyo lazima uandaliwe mkuu.
Huu ni wakati wa maandalizi. We ni mwanaume, kaa, tafakari, tafuta njia za kutatua na pia fanya juu chini kutekeleza njia hizo ili kufikia lengo.
Huna matatizo mkuu, kuna watu humu wana shida kiasi kwamba wakiona unapata mawazo ya kujikatisha uhai kisa hayo, watakushangaa sana.
Simama mkuu, nyakati ngumu hazidumu milele.