Maisha ndo haya haya, tuache majivuno

Maisha ndo haya haya, tuache majivuno

Leo nimepokea kwa masikitiko habari za kufulia kwa mkaka niliyewahi kuwa nae kwenye uhusiano kwa muda wa miaka 3. Nasikia amefulia ameuza kila alichokuwa nacho amebaki na komwe lake tu. Huyu kaka alininyanyasa sana kipindi ana vijipesa mi nikiwa kajamba nani. Alininyanyasa kisaikolojia kuna baadhi ya vitu nikikumbuka hadi leo nakuwa mnyonge.

Kuna siku nilimnunulia zawadi akaniuliza bei ya zawadi nilivyomwambia bei yake akanijibu i dont use cheap things keep it for yourself 🥲

Siku anaachana na mimi akaniambia relationship yetu illkuwa just for fun nothing was serious and it wasnt even a relationship it was a situationship 🥲 Kumbuka hapo wakati anaongea haya tulikuwa pamoja kwa miaka 3. Halafu akaongeza nimekuwa nakuonesha signs zote za kutotaka kuendelea kuwa nawe lakini bado ukaendelea kuniganda. Naomba kuanzia leo usinitafute kwa namna yoyote ile its over!!

Katika maisha yangu yote hakuna kipindi moyo uliniuma kama siku ambayo alinitamkia maneno haya. Mungu si Athumani, sasa hivi amepigika maisha yanamnyoosha tu. Licha ya mambo yote aliyonifanyia nimesikitika sana. Mwanga wa Mungu umuangazie arudi katika hali yake ya zamani. Tuweni humble jamani maisha ndo haya haya tuache kudharau watu katika maisha haijalishi ni maisha ya kimapenzi au kikazi, hakuna mtu anayeijua kesho yake.

NB: Roby nitafute nikupe mchongo, mimi sina roho mbaya kama yako!
miaka mi3 na hukumzalia mtoto
 
Hakuna mtu wa hovyo kama mwanamke akipata fursa sehemu au kazi ya maana, wakati nahangaika kuomba ajira secretary wengi sana walikuwa wanachana vyeti vyangu kwa sababu ya chuki...wanachana halafu wanatupa kwenye dustbin utasubili kupigiwa simu mpaka yesu anarudi
Mbona sjawai bahatika kuchaniwa vyeti jaman
 
Back
Top Bottom