Maisha ni kama ua yana chanua na kunyauka.

Maisha ni kama ua yana chanua na kunyauka.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Sifahamu nianzie wapi na habari hii. Tulipokuwa wadogo jirani yetu alikuwa mama mrembo tukizoea kumwita auntie. Auntie alikuwa mzaliwa wa mikoa yenye wanawake warembo. Auntie aliumbika, alikuwa na miguu chupa ya bia, rangi ya chungwa na hakuwa mfupi wala hakuwa super tall.


Auntie aliishi kwenye nyumba ya msajili lakini hakuwa na kazi. Alikuwa mchepuko wa mzee mmoja maarufu na tajiri sana wa enzi hizo Mhindi. Mhindi huyu aliishi Masaki na familia yake, pale kwa auntie alionekana kwa nadra sana.

Mara nyingi auntie akiwa mpweke alituita watoto twende kwake. Nyumba ilikuwa safi na nadhifu, tulipenda sana kwenda kwa auntie. Enzi zile za ujamaa TV hazikuruhusiwa lakini auntie alikuwa na TV ya black and white, alikuwa na deck tuliona cartoon za Tommy and Jerry.

Auntie alikuwa anakwenda Nairobi shopping kila baada ya miezi mitatu, alirudi na sabuni, dawa za meno, mafuta ya kula na ya kujipaka. Sisi tulifurahia BigG na Cadbury chocolates wakati wazazi walipewa dawa za meno na mafuta. Hizi ni zile enzi uhusiano wetu na Kenya ulivunjika na mipaka kufungwa.

Yule mzee wa Kihindi alifariki, na pale ilikuwa ni siri yake. Wakati huo tukiwa boarding tuliambiwa auntie alishindwa kuishi pale ilibidi ahame. Baadae tulisikia auntie alishindwa kabisa kumudu maisha utu uzimani. Watoto aliotulea tulijikusanya na kumsaidia. Tulimudu kumlipia kodi na hela ya kula. Utu uzima ulivyozidi aliamua kurudi kwao lakini auntie alitusisitiza tuwe na familia, Alisema watoto ndiyo urithi mkubwa duniani.
 
Kwa hiyo Sky una shauri tufyatue tuu.
 
Kuna waswahili watakwambia kuzaa si kupata....

Siku zote namuomba mungu pamoja na vyote nilivyonavyo anipe uzee mwema unikute nikiwa na haiba kama niliyonayo sasa.

Siijui kesho yangu japo naindaa na kujipa moyo itakuwa kama nilivyopanga.

Alamsiki.
 
hakuna maisha mabaya kama maisha ya uzeeni, maisha ya kuomba omba msaada yanaumiza sana. ukiwa masikini its better to die young kuliko kuja kuadhirika uzeeni. wazee wanaoinjoi maisha ni wale walioenvest kwenye real estate kama nyumba za kupanga. guest house, hotel, viwanda n.k
 
Wanawake wengine miaka ileee walipenda starehe na mali kutoka kwa wahindi wakasahau kuna kesho
Wengine walidanganywa watoe vizazi Leo hii wamekuwa wakiwa.

Mungu aliposema nimewaleta duniani mkaijaze dunia alikuwa na maana nyingi
 
Wanawake wengine miaka ileee walipenda starehe na mali kutoka kwa wahindi wakasahau kuna kesho
Wengine walidanganywa watoe vizazi Leo hii wamekuwa wakiwa.

Mungu aliposema nimewaleta duniani mkaijaze dunia alikuwa na maana nyingi
Kikubwa cha maana alichofanya ni kuleta watoto wa kaka zake mjini, mhindi hakuwa anapenda watu pale kwa kuhofia privacy yake. Auntie aliwapangishia vyumba haraka haraka.

Amini ninakuambia alipopata matatizo wale aliowaleta ndiyo walimcheka. Kilichotoka tumboni mwako hakitakutupa.
 
Kuna waswahili watakwambia kuzaa si kupata....

Siku zote namuomba mungu pamoja na vyote nilivyonavyo anipe uzee mwema unikute nikiwa na haiba kama niliyonayo sasa.

Siijui kesho yangu japo naindaa na kujipa moyo itakuwa kama nilivyopanga.

Alamsiki.
Naomba tuzae Kasie [emoji1787][emoji1787]
 
Na hata pia nikizeeka watoto wangu wataniacha na kumchukua mama yao na kwenda kumtunza kisha Mimi nijifie!

Tujipange!

Na mjipange kweli vinginevyo mjigawe, mtafute hela ya matumizi ya akiba ya baadae na utumie Muda wako wote wa ziada kujenga upendo kwa wanao ili Hata ukizeeka wakutunze au hata kukutembelea tuu na wajukuu.
 
Umepotelea wapi wewe rijali...?? Nani amekuficha??

Unataka pacha, triplets au mmoja wa dawa?

Ila tangu zygote ikiwa na siku 7 hadi anazaliwa Uwe tayari kwa huduma za maudhi madogo madogo ya preg.

Kasinde.
Am ready..
.niko huku Iraq vitani my wife to be
 
Back
Top Bottom