Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Sifahamu nianzie wapi na habari hii. Tulipokuwa wadogo jirani yetu alikuwa mama mrembo tukizoea kumwita auntie. Auntie alikuwa mzaliwa wa mikoa yenye wanawake warembo. Auntie aliumbika, alikuwa na miguu chupa ya bia, rangi ya chungwa na hakuwa mfupi wala hakuwa super tall.
Auntie aliishi kwenye nyumba ya msajili lakini hakuwa na kazi. Alikuwa mchepuko wa mzee mmoja maarufu na tajiri sana wa enzi hizo Mhindi. Mhindi huyu aliishi Masaki na familia yake, pale kwa auntie alionekana kwa nadra sana.
Mara nyingi auntie akiwa mpweke alituita watoto twende kwake. Nyumba ilikuwa safi na nadhifu, tulipenda sana kwenda kwa auntie. Enzi zile za ujamaa TV hazikuruhusiwa lakini auntie alikuwa na TV ya black and white, alikuwa na deck tuliona cartoon za Tommy and Jerry.
Auntie alikuwa anakwenda Nairobi shopping kila baada ya miezi mitatu, alirudi na sabuni, dawa za meno, mafuta ya kula na ya kujipaka. Sisi tulifurahia BigG na Cadbury chocolates wakati wazazi walipewa dawa za meno na mafuta. Hizi ni zile enzi uhusiano wetu na Kenya ulivunjika na mipaka kufungwa.
Yule mzee wa Kihindi alifariki, na pale ilikuwa ni siri yake. Wakati huo tukiwa boarding tuliambiwa auntie alishindwa kuishi pale ilibidi ahame. Baadae tulisikia auntie alishindwa kabisa kumudu maisha utu uzimani. Watoto aliotulea tulijikusanya na kumsaidia. Tulimudu kumlipia kodi na hela ya kula. Utu uzima ulivyozidi aliamua kurudi kwao lakini auntie alitusisitiza tuwe na familia, Alisema watoto ndiyo urithi mkubwa duniani.