Mi nashangaa sana watu wanaosema Dar hapaeleweki ila hawaondoki! Dar kuna spenders, ukiweza kukaa kwenye chain yao kutoka ni chap.Mbeya masikini.
Ondoka huko urudi Dar uendeshe hata bodaboda.
Hiyo hela utaiona saa 6 mchana.
Mkuu naona umetoka nje ya mada kwa makusudi kabisa🤣🤣Ndio maana inabidi mtusikilize walume ndago! Sio kushupaza shingo, Men will always be Men!
Mi nashangaa sana watu wanaosema Dar hapaeleweki ila hawaondoki! Dar kuna spenders, ukiweza kukaa kwenye chain yao kutoka ni chap.
Inahitajika akili kidogo ili uweze ku balance income & expenses! Bila maisha kuwa juu Dar pesa isingeonekanaDar hela ipo hata ufumbe macho unaigusa...ila maisha yako juu sana!...
Tupe somo mkuu tuko hapa🤗Inahitajika akili kidogo ili uweze ku balance income & expenses! Bila maisha kuwa juu Dar pesa isingeonekana
Hahaha hamna somo zaidi ya ubahili tu. Unapata 100 unalimit matumizi kwenye 50! Usivuke hapo yani. Ili unachokitafuta kionekaneTupe somo mkuu tuko hapa🤗
Sawa! Umeeleweka!labda pia na kuwa side hustle za kutosha!..Hahaha hamna somo zaidi ya ubahili tu. Unapata 100 unalimit matumizi kwenye 50! Usivuke hapo yani. Ili unachokitafuta kionekane
Mkuu mbeya wadada wanapenda kuvaa na urembo, una mtaji wowote nikupe wazo zuriHabari za muda huu wakuu.
Katika hali ya kupambana na maisha, siku chache zilizopita nmepata nafasi ya kuingia jijini Mbeya kwa lengo la kutafuta namna ya kujikwamua kiuchumi.
Hivyo basi naomba kwa Wenyeji wa Mkoa wa Mbeya mnipe mawazo yenu: Biashara gani ninaweza nikaifanya na ikaonesha mafanikio kwa kipindi kifupi? Yaani atleast nikaingiza hata 5000/= kwa siku?
Usisite kutoa wazo lolote lile unalohisi linaweza kuwa na manufaa kwangu.
KARIBUNI
Side hustle ndo zinawapa relief watu wengi bongo. Sasa imagine ukiwa hauko tied na ajira ya mtu. Kama mjanja unatengeneza hela.Sawa! Umeeleweka!labda pia na kuwa side hustle za kutosha!..
Wanaume wana machaguo mengi sana kuliko wanawake! Basi tu
Dar inatakiwa ufanye vitu vinavyoonekana vya kipuuzi maana ndio vina hela ya chap chap japo watu wengi wanavidharau.Sawa! Umeeleweka!labda pia na kuwa side hustle za kutosha!..
Dar hela ipo hata ufumbe macho unaigusa...ila maisha yako juu sana!...
Kwenye hili huwa natofautiana na watu wengi sana,
Mfano kwenye chakula, karibu mikoa yote inayozalisha chakula, kituo cha kwanza kupeleka mchele, mahindi, maharage, matunda n.k ni Dar
Mfano msimu wa machungwa au mananasi unaweza kuta hayo matunda ni bei aghali Tanga mjini/Morogoro mjini kuliko Sterio pale Temeke au Buguruni au Kariakoo
Mchele unaweza kutoka Ifakara lakini Morogoro mjini ukauzwa bei ghali kuliko masoko mengi tu ya Dar es salaam
Dar kila kitu unakipata kulingana na mfuko wako hata ukitaka msosi wa Tsh.1000/= unapata, hata ukitaka chumba cha Tsh. 10,000/=
Inategemeana na sehem .sehem zingine ngumu kukubalikaMkuu hata wewe unaweza kuendesha boda
Dar inatakiwa ufanye vitu vinavyoonekana vya kipuuzi maana ndio vina hela ya chap chap japo watu wengi wanavidharau.
Niliposikia mchanganuo wa biashara ya mahindi na jinsi yanavyouzwa nikamuwaza jamaa mmoja yuko posta ambaye anauza mahindi kuanzia asubuhi saa 4 mpaka jioni kabisa. Anakusanya hela kiasi gani. Ration ya mtaji na faida ni almost 1:3
Ahsante mkuu.. Mm nahisi bado nipo kwenye stage za mwanzo kabisa za kutafuta nn cha kufanya, sijawahi kuwa na wazo permanent kuwa natamani kufanya kitu cha aina fulani..Hongera mkuu kwa nia ya kupambana, lakini wewe kama wewe ungependa kufanya nini? At least idea yako uliyowahi kuifikiria na ukatamani kuifanya, pili una mtaji kiasi gani?
Kila la kheri
Ahsante ndugu kwa ushauri makini.Kilimo mkuu jumua mihogo kutoka tukuyu lete mbeya au anza kukaanga sehemu ukosi pesa, ukiwa na mtaji mkubwa tafuta Bajaji au boda ukosi hiyo pesa,
Wahi asubuhi maeneo ya mnada wa ccm ukiwa na laki na nusu kodii eneo fungua belo nguo za kike hutojutia uwezi kosa faida 15 kwenda juu kazi ya masaa tu,
Kila lakheri, mtafutaji achoki akichoka kapata, maisha ni mapambano.