Kwenye hili huwa natofautiana na watu wengi sana,
Mfano kwenye chakula, karibu mikoa yote inayozalisha chakula, kituo cha kwanza kupeleka mchele, mahindi, maharage, matunda n.k ni Dar
Mfano msimu wa machungwa au mananasi unaweza kuta hayo matunda ni bei aghali Tanga mjini/Morogoro mjini kuliko Sterio pale Temeke au Buguruni au Kariakoo
Mchele unaweza kutoka Ifakara lakini Morogoro mjini ukauzwa bei ghali kuliko masoko mengi tu ya Dar es salaam
Dar kila kitu unakipata kulingana na mfuko wako hata ukitaka msosi wa Tsh.1000/= unapata, hata ukitaka chumba cha Tsh. 10,000/=