Maisha ni kutafuta: Nahitaji Msaada wa mawazo yako ndugu

Maisha ni kutafuta: Nahitaji Msaada wa mawazo yako ndugu

Habari za muda huu wakuu.

Katika hali ya kupambana na maisha, siku chache zilizopita nmepata nafasi ya kuingia jijini Mbeya kwa lengo la kutafuta namna ya kujikwamua kiuchumi.

Hivyo basi naomba kwa Wenyeji wa Mkoa wa Mbeya mnipe mawazo yenu: Biashara gani ninaweza nikaifanya na ikaonesha mafanikio kwa kipindi kifupi? Yaani atleast nikaingiza hata 5000/= kwa siku?

Usisite kutoa wazo lolote lile unalohisi linaweza kuwa na manufaa kwangu.

KARIBUNI
Mkuu mbeya wadada wanapenda kuvaa na urembo, una mtaji wowote nikupe wazo zuri
 
Sawa! Umeeleweka!labda pia na kuwa side hustle za kutosha!..
Side hustle ndo zinawapa relief watu wengi bongo. Sasa imagine ukiwa hauko tied na ajira ya mtu. Kama mjanja unatengeneza hela.

Kitu nilichoona watu wengi sahivi wame invest kwenye kuremba biashara kuliko kufanya biashara hapo town. Biashara ina mazingira makali ila hamna kitu kinafanyika.

Naona Mak juice mwenyewe ana struggle kinoma sahivi. Watu juice sijui hawanywi tena. Hata matangazo sioni.
 
Sawa! Umeeleweka!labda pia na kuwa side hustle za kutosha!..
Dar inatakiwa ufanye vitu vinavyoonekana vya kipuuzi maana ndio vina hela ya chap chap japo watu wengi wanavidharau.

Niliposikia mchanganuo wa biashara ya mahindi na jinsi yanavyouzwa nikamuwaza jamaa mmoja yuko posta ambaye anauza mahindi kuanzia asubuhi saa 4 mpaka jioni kabisa. Anakusanya hela kiasi gani. Ration ya mtaji na faida ni almost 1:3
 
Kwenye hili huwa natofautiana na watu wengi sana,

Mfano kwenye chakula, karibu mikoa yote inayozalisha chakula, kituo cha kwanza kupeleka mchele, mahindi, maharage, matunda n.k ni Dar

Mfano msimu wa machungwa au mananasi unaweza kuta hayo matunda ni bei aghali Tanga mjini/Morogoro mjini kuliko Sterio pale Temeke au Buguruni au Kariakoo

Mchele unaweza kutoka Ifakara lakini Morogoro mjini ukauzwa bei ghali kuliko masoko mengi tu ya Dar es salaam

Dar kila kitu unakipata kulingana na mfuko wako hata ukitaka msosi wa Tsh.1000/= unapata, hata ukitaka chumba cha Tsh. 10,000/=
Dar hela ipo hata ufumbe macho unaigusa...ila maisha yako juu sana!...
 
Kwenye hili huwa natofautiana na watu wengi sana,

Mfano kwenye chakula, karibu mikoa yote inayozalisha chakula, kituo cha kwanza kupeleka mchele, mahindi, maharage, matunda n.k ni Dar

Mfano msimu wa machungwa au mananasi unaweza kuta hayo matunda ni bei aghali Tanga mjini/Morogoro mjini kuliko Sterio pale Temeke au Buguruni au Kariakoo

Mchele unaweza kutoka Ifakara lakini Morogoro mjini ukauzwa bei ghali kuliko masoko mengi tu ya Dar es salaam

Dar kila kitu unakipata kulingana na mfuko wako hata ukitaka msosi wa Tsh.1000/= unapata, hata ukitaka chumba cha Tsh. 10,000/=

Usemayo ni sawa....! Hapa wewe umeangalia kwa jicho jingine pia ...!
 
Dar inatakiwa ufanye vitu vinavyoonekana vya kipuuzi maana ndio vina hela ya chap chap japo watu wengi wanavidharau.

Niliposikia mchanganuo wa biashara ya mahindi na jinsi yanavyouzwa nikamuwaza jamaa mmoja yuko posta ambaye anauza mahindi kuanzia asubuhi saa 4 mpaka jioni kabisa. Anakusanya hela kiasi gani. Ration ya mtaji na faida ni almost 1:3

Point..lakini vijana wengi wa sasa wanaona haya!
 
Hongera mkuu kwa nia ya kupambana, lakini wewe kama wewe ungependa kufanya nini? At least idea yako uliyowahi kuifikiria na ukatamani kuifanya, pili una mtaji kiasi gani?
Kila la kheri
Ahsante mkuu.. Mm nahisi bado nipo kwenye stage za mwanzo kabisa za kutafuta nn cha kufanya, sijawahi kuwa na wazo permanent kuwa natamani kufanya kitu cha aina fulani..

Nnachokitafuta kwa sasa ni ideas mbalimbali then ntachagua naanzia wapi.. Kuhusu mtaji usijali ndugu, naamini utapatikana tu, kikubwa ni wazo la biashara coz kuna watu wanapesa lakin hawana idea wazifanyie nn..

Ila tu liwe wazo la kijasiriamali, sio la mtaji wa mamilioni ya fedha, hapana! Huko tutafika taratibu
 
Kilimo mkuu jumua mihogo kutoka tukuyu lete mbeya au anza kukaanga sehemu ukosi pesa, ukiwa na mtaji mkubwa tafuta Bajaji au boda ukosi hiyo pesa,

Wahi asubuhi maeneo ya mnada wa ccm ukiwa na laki na nusu kodii eneo fungua belo nguo za kike hutojutia uwezi kosa faida 15 kwenda juu kazi ya masaa tu,

Kila lakheri, mtafutaji achoki akichoka kapata, maisha ni mapambano.
Ahsante ndugu kwa ushauri makini.
 
Back
Top Bottom