Maisha ni kuzaliwa, kusoma, kupata kazi, kuoa/kuolewa, kupata watoto kisha yanaishia hapo au kuna kingine?

Maisha ni kuzaliwa, kusoma, kupata kazi, kuoa/kuolewa, kupata watoto kisha yanaishia hapo au kuna kingine?

Mkuu ukishakuja duniani ni wewe kuchagua utakavyoishi na namna gani utaishi.
Kuna mfumo tuliwekewa na jamii kwa mfano kusoma, kupata kazi, kuoa/kuolewa, kuzaa etc. Haimaanishi usipoishi ndani ya huo mfumo basi maisha yako yanakua hayajakamilika.

Ukishazaliwa kinachofuata ni kufa. Kabla hujafa hakikisha unaishi ile namna ikupendezavyo kwa sababu hakuna manual ya kukuelekeza namna utaishi mpaka pale utakapokifikia kifo.

Huyo jamaa yako amechagua kuishi kwa namna yake wakati anasubiri kuhitimisha safari yake duniani.
Yes.. hapo umeongea mamii
 
Haupaswi kuwa hivyo, there must be a special purpose you were created for,ila huijui, kama unaijua huiendei, kama unaindea huifikii ndipo tunaona maisha yetu yana ufa mkubwa sana, ukilijua lengo halisi la maisha yako hapa duniani utafikia maximum utilization of "you" na hapo ndipo utatapata the maximum satisfaction, utafurahia maisha.
Wachache sana wamepata bahati hiyo, wengi tunajisindikiza tu including me na ndio maana kuna wakati tukijitathmini tunaona kama vile maisha hayana maana wala thamani.

Ukiuliza kwa nini hatujui makusudi ya kuumbwa kwetu, jibu ni kuwa makusudi yetu yameibiwa, yamefichwa, yameharibiwa na muharibu tukingali tuli wadogo,kwa hiyo tunayembea kwa kupapasa papasa tu.
Asante mkuu
 
Wengine wanapiga michepuko, wanafumaniwa, wanaenda kupigana vita huko Ukraine, wanakaa bar, wanapigwa chupa, wanafanya biashara, wanafilisika, wanaanza upya, wanatembea kila kona ya dunia, wanakua magaidi, wanaenda jela, wanafanya siasa, yaani mambo ni mengi muda ni mchache.
 
Wakuu..

Hiv maisha ndo yanaishia hapo tu au kuna la ziada... Maana naona watu weng accomplishment zao znacheza hapo.. So. Nauliza ni hapo tuu au? Kuna kitu na regret sana mim kama mim.. niko mbion angalau kukibadili. Well.. perhaps tumezaliwa kwenye land of no dream... Tunafanyaje sasa hapo.

Kama vijana na vikwazo viiing vilivyopo mbele yetu kiuchumi.. kujikwamua etc.. Je tunatokaje hapo... Au ndo kupambana? Mbona watu wanapambana snaa ila matokeo ni madogo mnoo.. (kwa legal things) Je wafanye illegal doings kufikia mahala fulan mapema..? Kwasasa bila connection kwa mazingira yetu ni ngum sana kutoboa... Je watu waluke vihunzi na kwenda tafuta oportunity kwingne?

Je tufanye hivyo? Mazingira ya kufanya biashara kwann yamekua magum sana kwenye maeneo yetu haya? Tatzo ni nin?.. Tukija kwenye ajira rasmi.. mbona progress ni hafifu sana... Maslah madogo mno. Je tufanyaje? Well mim binafsi nna maamuzi yangu fulan mwaka huu.. ni magum ila itabid yafanyike. Au labda mim siridhik na kidogo nilichpata.

Perhaps kwa wenzangu ni worse zaid.. Enewei.. nna mikakat mizito mwaka huu.. itabid itik tuu kwa namna yoyote. Au tuendelee kuvumilia?

Uzi tayar..

(Niko site hapa nikitekeleza majukum ya nchi.. joto.. jua kal had kichwa kinauma..)

Mawazo haya yamekuja gafla
Umesahau Kufumaniwa
 
Seriously ukiyafikilia sana hayana maana kabisa.
Embu waza kidogo mtu aliyezaliwa mwaka 1970 ana muda mchache sana wakuishi ukiweka kando maradhi na mengineyo ambayo yanaweza kumfanya apoteze uhai

Wa 1980 naye hayuko mbali kufikia ukomo akiishi sana ni miaka 15 - 20 tu mbele hii ndio life expectancy yetu dah [emoji17]
Ndio maana Yesu aliona aje ili kufanya Life-Endless Extension.
 
Maisha ni kuzaliwa, kubarehe na kufa.

kama kuna maisha baada ya kufa hili tutalijua huko huko.
 
Chagua unavyotaka wewe jamii itakubaliana na maamuzi yako na isipokubaliana pia sio shida yako.
Kuna vingne ni vigum ndugu yangu.. acha tu.. for example mi napenda kuwa rasta.. ila siwez sabab job haiwezekan.. home pia hawatonielewa.. pia mfano mi ni christian ila napenda kuwa na wake wawil.... You see what am sayin?
 
Wengine wanapiga michepuko, wanafumaniwa, wanaenda kupigana vita huko Ukraine, wanakaa bar, wanapigwa chupa, wanafanya biashara, wanafilisika, wanaanza upya, wanatembea kila kona ya dunia, wanakua magaidi, wanaenda jela, wanafanya siasa, yaani mambo ni mengi muda ni mchache.
You see.. thats life..
 
Baada ya hapo ni kula bata kama kipato kinaruhusu na kumuabudu Mungu.
 
The Alchemist by Paul Coelho kinaweza kuwa msaada kwako ..

Pia mastery cha Robert Greene.

Maisha ni namna unavyoridhika wewe kuishi.

Kama unavyoishi Hakuridhishi wala kuamanisha nafsi ipo namna ambayo unapaswa uishi tofauti na unavyoishi hivi sasa.

Mimi pia bado najitafuta mimi ni nani
 
Mimi nina imani na maisha baada ya kifo yaani kuna pepo na moto hakuna vingine isipokuwa mtu atalipwa kwa matendo yake ya hapa duniani.

Starehe za dunia za udanganyifu ;
#Mtu unapiga mitungi , bangi nk unakuja kuleta madhara kiafya baadae

#Unakuwa mtu watotozi unajivagaa unapata Ukimwi , magonjwa mengine ya zinaa , kufumaniwa , kubambikiwa watoto nk

#Unanunua gari kwa starehe linakuja kumaliza kwa ajali

#Tajiri bado unaishi kwa hofu hauna amani asimilia kubwa.Kuuliwa nje nje

#Duniani hakuna utulivu kabisa ukraine sasa wote tajiri na masikini mpk Raisi hawana amani.
 
Haya maisha hutakiwi kuyachukulia siriaz saana.. we fanya kile unachoweza kufanya ku survive maana hilo ndio lengo la kuwepo hapa duniani. Mengine ni nyongeza tu.
 
Sidhan.. mbona kubwa sana dunia
Mimi hua naona sisi binadamu hatuna tofauti na kuku waliofungiwa bandani. Unaishi kulingana na matakwa ya mfugaji, unakula unachopata, unahangaika kujipambania wewe na jamii yako, mwisho wa siku mwenye banda anakamata kuku ampendae na kumchinja, huku wengine mnabaki hamna pa kukimbilia wala cha kufanya mnasubiri zamu yenu 😪
 
Back
Top Bottom