Maisha tuliyoishi na Telephone Operators

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ninakumbuka zile enzi za kusubiri line, line ikipatikana unakuta namba iko engaged.

Sisi tuliokulia vijijini simu ilikua inaunganishwa na operator Wilayani. Zile familia maarufu hata habari walipata kutoka kwa operator.

Ilikua ni rahisi kumpata operator na kumpa taarifa za kifo, uzazi au harusi. Kujiweka vizuri na operator akija dukani kuna siku unampa sukari ya bure, wengine walitoa nyama ya bure na wengine walitoa kadi za harusi kwa operator. Alikua ni mtu wa mihimu sana Wilayani.

Ma operator walibeba siri nyingi, bahati nzuri hakukua na social media.

 
Kweli miaka ile nakumbuka nikiwa mbeya unatuma hela kwa mzazi lazima uende posta utume hela kwa regista

Ukitoka posta uende kwa telephone operator uombe kupiga simu kijijini tena kwa Askofu Moshi ndo pekee palikuwa na simu,

Unaomba akaitwe mzazi wako ilenumpe namba za register

Was tired some, heko operators
 
... kuna ile ya kutuma TELEGRAM; max. maneno 10 zaidi ya hapo unalipia every extra word. Sijui hii ndio equivalent na SMS siku hizi? Kuna binadamu wa sasa hawajui kabisa kama hii kitu iliwahi kuwepo wakati ni just a few years ago!
 
... kuna ile ya kutuma TELEGRAM; max. maneno 10 zaidi ya hapo unalipia every extra word. Sijui hii ndio equivalent na SMS siku hizi? Kuna binadamu wa sasa hawajui kabisa kama hii kitu iliwahi kuwepo wakati ni just a few years ago!
Hiyo niliitumia miaka hiyoooo, kaka alienda mafia akazamia huko mmh, hakuna njia hatukutumia ili kumtafuta,

Hiyo ilikuwa inafikia polisi then ujumbe unaenda sijui wapi,

Maisha safari ndefu
 
Kweli miaka ile nakumbuka nikiwa mbeya unatuma hela kwa mzazi lazima uende posta utume hela kwa regista...
... ha ha ha! Registered mail; inakupa assurance itafika salama kwa sababu mnakuwa "mmeandikishana" na Posta na ni gharama kidogo.

Ila zile za kubandika stempu ukadumbukiza kwenye box kuna mawili; inaweza kufika au isifike na ikifika kama ilikuwa na "kaunene" fulani lazima mpokeaji atakuta imechanwa wafanyakazi wa Posta "walichungulia" kuna nini! Kulikuwa na upumbavu sana! Thanks to technology!
 
Hiyo niliitumia miaka hiyoooo, kaka alienda mafia akazamia huko mmh, hakuna njia hatukutumia ili kumtafuta,

Hiyo ilikuwa inafikia polisi then ujumbe unaenda sijui wapi,

Maisha safari ndefu
... tumetoka mbali sana kwa kweli. Nilikuwa naendaga wilayani kuomba reverse call kwa operator ili nimjulishe ba' mkubwa natarajia kufika Dar es Salaam kwa treni baada ya miezi mitatu; wanipokee mwisho wa reli!
 
Hiyo niliitumia miaka hiyoooo, kaka alienda mafia akazamia huko mmh, hakuna njia hatukutumia ili kumtafuta,

Hiyo ilikuwa inafikia polisi then ujumbe unaenda sijui wapi,

Maisha safari ndefu
... halafu kulikuwa na miaka fulani hivi wanafamilia walikuwa "wanapotea" sana! Yaani mtu akiondoka kijijini ameondoka hamtokaa mumwone tena ila mtakuwa mnasikiasikia sijui yuko wapi hadi wazazi wanafariki kaka mkubwa hajulikani alipo! Sijui kulikuwa na tatizo gani!
 
Mambo hayakuwa mepesi, pamoja na operator kusaidia kumpata mzazi, hela zilienda zikakwama pale Marangu mtoni , yaani kuzitoa hapo hizo regista zifike ofisi ya kanisa ambapo ndo mzazi atasomwa jina kanisani ili akachukue bahasha ilikuwa mbinde

Wakati mwingine zilikusanyika hapo hata regista tano mpaka ukienda likizo unaitwa kuzifuatilia

But all in all tuliwapenda na kuwajali wazazi, sijui vijana wa leo
 
Sema huyu kaka alipatikana ila kwa kumpa mtu nauli kwenda kumfuata, naona Ashura wa mafia alimficha 🤣🤣
 
Haka kaupumbavu wafanyakazi wa Posta wanako hadi leo
 
... mavijana ya leo tena ukileta za kuleta yanaku-block; ha ha ha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…