Caroline Danzi
JF-Expert Member
- Dec 19, 2008
- 3,713
- 1,265
I am a failure when it comes to balancing my time..... All blames to TBL/SBL. Why on earth are they brewing this kind of drinking liquid? ...When I get out of my office the only thing in my addicted mind is Beer......... and only Beer!
Dah Mbu umeniumbua vibaya weye mie sina mpangilio kabisa ngoja nisome na kukariri kha!! mpaka naona aibu kabisa.........................
MwanajamiiOne,...
Tatizo la wengi wetu tufanyao hizi kazi za kuajiriwa tuna nidhamu ya uwoga!...
Kwanza ni haki ya muajiriwa kudai Job description!...msinambie eti Bongo hakuna hiyo....
Haya, hata kama wafanya kazi kwa mhindi... masaa ya kazi ni yale yale,...either 8- 4/5pm!
Hakuna Muhindi ambaye anataka kufanya kazi/biashara zake zaidi ya masaa nane...chunguza!
Kwa wakazi wa Dar, jioni mtawaona hawa wenzetu waasia wamejazana kwenye gari na wake zao na watoto haooo Coco Beach kula upepo wa bahari na madafu. Tukirudi kwa wabantu wenzangu na mie,...waajiriwa tukishatoka maofisini/vibaruani, wengi wetu tunaishia 'vikaoni' na washkaji kupoozea mbili tatu kabla ya kurudi nytumbani. Tena usipoonekana kikaoni utaulizwa, unakimbilia nini nyumbani?!
Kuhusu hizo worrk overloads,...kiukweli kuna kila dalili nasi twachangia kujitwisha hayo ma home work!....Hivi kuna raha gani upo nyumbani na mkeo/mumeo, badala ya kutumia masaa machache baada ya mihangaiko ya kutwa kuwasaidia watoto homework, kula pamoja, na kubembelezana kwenye kochi kabla ya kwenda kulala...wewe mke/mume unakuwa busy na mafaili yako ya ofisini? Hasta huo muda wa kubadilishana mawazo unakuwepo kweli?
By the time mke/mume huyo anakwenda kulala, tayari mwenziwe anakuwa keshaboreka...keshajilalia zamani. Au kama mume ndio ana roho ndogo, atajionea bora akazurure nje...awe anarudi nyumbani kulala tu. There's alimit kwa kila kitu,...kuna kazi za dharura, hizo ni kawaida kufanyika nyumbani,...lakini si vizuri kujenga mazoea Monday to monday mke/mume yupo busy na mafaili ya ofisi,...au nakosea jamani?
Binafsi, I can tolerate baadhi ya kazi, lakini zile nionazo mke wangu anazidiwa kiasi kwamba huko kazini wanahataraisha maisha ya ndoa yangu, maisha ya mke wangu, na watoto wetu...sitasita kumjengea tabia ya kuanza kuacha mafaili huko huko ofisini. Tena akirudi nyumbani na simu zizimwe. Haiwi ati bosi yupo Kempinski na mkewe, anampigia mamsapu eti a submit report by 6am... unless mke wangu nae ni mzito wa kumaliza kazi zake huko ofisini.... that's another case.
Duh yaani hapa umenichoma, ukanichoma na kunichoma..........yaani ni kama vile ninavyoishi huwa unaka-video kadogo unanimonitor mimi Mh sasaa dah hata sijui nisemeje Mbu
Hii wheel of life haina jinsi ya kutufundisha kujaribu basi kubalance?
....khaaa? Mwj1 hapo juu umeandika kilugha gani bana, hebu fanya editing kidogo..
eeehhh? kama hivyo ndivyo unavyoishi basi wahitaji reality check kwenye prioroties za maisha yako.
Kumbuka, kila siku ina masaa 24,...waweza yagawa hayo masaa 24/3?....hebu nipe mfano unavyogawa muda wako katika siku, tubadilishane mawazo....
Mh.................................nahau hii Mbu. Sasa nlikuwa nawaza kwa kuwa mtu kuwa buzy kikazi kunaoanishwa na kuwa na pesa nyigni. Je inawezekana ukugundua kuwa unafanya kazi saha, unakosa muda wa kubalance maisha lakini unapata pesa nyingi. Je haiwezekani mtu kureset targets zake ili apunguze muda wa kazi? Say anafanya kazi 28 hrs na anapata wastan wa dola 6,000 kwa mwezi but all the time yuko stressed up, familia inaishi maisha ya upweke ingawa they have everything but ndo hivyo vya story ya WoS ! but akijichunguza anagundua kuwa ili aishi maisha ambayo atapata muda wa kuishi na kupata quality time na familia yake, kurudisha uhusiano mzuri na MUNGU wake n.k then inambidi afanye kazi masaa hayo 8 kwa wastani wa Dola 2000 with opportunity cost $ 4000! je kuna ataewezasacrifice??
Mh Mbu nayagawaje? kwani hata siku nyingine kukumbuka kuwa siku ina masaa 12 ya mchana huwa sikumbuki itakuwa hayo ya kugawanywa? Nayagawa kwa kigezo gani?
Hiyo avatar mpya Mhhhhh! π ndio kaichagua nanihii!? hahahahahah lol! naogopa kuchema π
Mkuu Mbu katika huo mduara wa "wheel of life" wengine wameuvunja vunja na kutengeneza kamduara kao kadogo kadogo katika yale mambo ambayo wanayaona yanastahili kupewa kipaumbele katika maisha yao.
Kwa mfano wengine hawaoni umuhimu wa kwenda kanisani/msikitini kwa masaa chungu nzima kwa wiki pamoja na kuwa wanaamini kwamba Mungu yuko. Husali kwa dakika chache nyumbani kwao kila siku inapoanza na kwisha kumshukuru kwa yale aliyowajalia na kumuomba mengine wanayoyahitaji. Wengune pamoja na kuwa wanayapenda maisha ya ndoa huamua kuoana lakini hawataki watoto kutokana na gharama za malezi zilivyo kubwa na pia "kuharibu" life style ya wanandoa pale watoto wanapohusika kama bile badala ya kujirusha saa yoyote ile wanayotaka au kulala masaa yoyote ile au kwenda vacation za nguvu katika vivutio mbali mbali duniani kama kwenye mbuga za wanyama π ufukweni mwa bahari iwe East Africa, Carribean au kwingineko. Wengine wameshajijenga vya kutosha kwa hiyo mambo ya carrer na finance kwao hayana matatizo.
Ninachotaka kusema ni kwamba huo mduara original wa 'wheel of life" familia nyingi zinauvunja vunja na kutengenza mduara wao mdogo kutokana na mambo yale wanoyayaona yanasyahili kupewa kipaumbele kla siku, kila wiki, kila mwezi na pia kila mwaka. Kwa hiyo si ajabu kukuta kwamba mduara mdogo wa "wheel of life" wa familia A umetofautiana kidogo/sana na ule wa familia B kutokana na kuwa vipaumbele tofautu katika maisha yao ya kila siku. Kwa wale ambao wanajitahidi kuufuta mduara huo mkubwa wa wheel of life, kwa maoni yangu ni kazi kubwa mno! na kama wapo wanaofanikiwa basi ni wachache sana.
Hiyo avatar mpya Mhhhhh! π ndio kaichagua nanihii!? hahahahahah lol! naogopa kuchema π