MwanajamiiOne,...
Tatizo la wengi wetu tufanyao hizi kazi za kuajiriwa tuna nidhamu ya uwoga!...
Kwanza ni haki ya muajiriwa kudai Job description!...msinambie eti Bongo hakuna hiyo....
Haya, hata kama wafanya kazi kwa mhindi... masaa ya kazi ni yale yale,...either 8- 4/5pm!
Hakuna Muhindi ambaye anataka kufanya kazi/biashara zake zaidi ya masaa nane...chunguza!
Kwa wakazi wa Dar, jioni mtawaona hawa wenzetu waasia wamejazana kwenye gari na wake zao na watoto haooo Coco Beach kula upepo wa bahari na madafu. Tukirudi kwa wabantu wenzangu na mie,...waajiriwa tukishatoka maofisini/vibaruani, wengi wetu tunaishia 'vikaoni' na washkaji kupoozea mbili tatu kabla ya kurudi nytumbani. Tena usipoonekana kikaoni utaulizwa, unakimbilia nini nyumbani?!
Kuhusu hizo worrk overloads,...kiukweli kuna kila dalili nasi twachangia kujitwisha hayo ma home work!....Hivi kuna raha gani upo nyumbani na mkeo/mumeo, badala ya kutumia masaa machache baada ya mihangaiko ya kutwa kuwasaidia watoto homework, kula pamoja, na kubembelezana kwenye kochi kabla ya kwenda kulala...wewe mke/mume unakuwa busy na mafaili yako ya ofisini? Hasta huo muda wa kubadilishana mawazo unakuwepo kweli?
By the time mke/mume huyo anakwenda kulala, tayari mwenziwe anakuwa keshaboreka...keshajilalia zamani. Au kama mume ndio ana roho ndogo, atajionea bora akazurure nje...awe anarudi nyumbani kulala tu. There's alimit kwa kila kitu,...kuna kazi za dharura, hizo ni kawaida kufanyika nyumbani,...lakini si vizuri kujenga mazoea Monday to monday mke/mume yupo busy na mafaili ya ofisi,...au nakosea jamani?
Binafsi, I can tolerate baadhi ya kazi, lakini zile nionazo mke wangu anazidiwa kiasi kwamba huko kazini wanahataraisha maisha ya ndoa yangu, maisha ya mke wangu, na watoto wetu...sitasita kumjengea tabia ya kuanza kuacha mafaili huko huko ofisini. Tena akirudi nyumbani na simu zizimwe. Haiwi ati bosi yupo Kempinski na mkewe, anampigia mamsapu eti a submit report by 6am... unless mke wangu nae ni mzito wa kumaliza kazi zake huko ofisini.... that's another case.