Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
The wheel of life is a valuable tool to help you evaluate what's working and what's not working in your life.
...ni kawaida kusikia mtu anakujia na excuse ya,."..sikuwa na muda!"...lakini je? huwa unajipangia mambo yako kwa mujibu wa muda, au ndio umejikubalisha muda utawale sehemu kubwa ya maisha yako?
Evaluate maisha yako kisha ujiulize;
- una muda wa kutosha kukaa na kubadilishana mawazo na familia yako? Unawasaidia watoto homeworks zao, kujua maendeleo yao kimaisha? ...vipi kutembelea ndugu, jamaa na marafiki?
- una muda wa kutosha na mpenzi/mke/mume wako, ...mwenza wako halalamiki hutulii nyumbani?
- umejiwekea muda wa kutosha kujiburudisha akili, hii ni recreational activities hata kama ni kwa kibustani cha mboga..., michezo etc? , una muda wa kutosha kufanya ibada?
- una muda wa kutosha kujiangalia afya yako, kufanya mazoezi, regular check ups? au mpaka uumwe ndio unakwenda hospitali?
- Una muda wa kutosha kufanya kazi zako bila kuelemewa na kurudi nazo nyumbani? Wengine 'hushikika' hata kula wanasahau. Nawe ni mmoja wao?
"You can have anything you really want but you cannot have everything you want."
"To know yourself is the first and most important step to pursuing your dreams and goals." – Stedman Graham
Liwezekanalo kufanyika leo, usilisubirishe. Ni wangapi kufumba na kufumbua wamejishtukia tayari retirement age ishawafikia ilhali hawakukumbuka kuwekeza?
Fainali uzeeni!....tusisubiri kukurupushwa ilhali kushakucha!...Hakuna awezaye kukupangia mkaisha yako ila wewe mwenyewe. Tuanze kujipangia maisha yetu kuanzia sasa kisha mtaona uwiano mzuri wa maisha, furaha, amani na mapenzi yanavyorudi tena majumbani mwetu. Otherwise,
kwanini unaamini hauna muda wa kutosha (ku balance maisha yako?)