Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Kama ningalifuata usemi wa "Ya Kaisali Muachie Kaisali" basi ningebaki na donda lenye kudumisha deni la Roho yangu, na kama ningaliweza basi ningeenda pale Colombo Sri Lanka kwenye Kaburi la Sir Arthur Clarke mwanasayansi na mwandishi wa Tamthilia.
Aliyewahi kusema kuwa Magic is just a science that we don’t understand yet” kwamba miujiza ni sayansi tusiyoielewa" Huenda haya ninayowaza yakawa ni ndoto pia, tena ndoto ya kisayansi nisiyoielewa,
Naiwaza ile Tarehe 20 Mei 1993 kule Ghana Vijijini katika Familia ya wakulima alipozaliwa Benard Morison.
Natahamaki na kujiuliza ni wapi Walifukia kitovu chake, maana ana Nyota sana huyu, Nawaza nikifika kijijini Kpandu (Alipoanzia soka) nimuulize nani kuhusu BM3?
Au Niende Ashanti Gold alipocheza msimu mmoja kisha Niende AS VITA kwa Ibenge, Huenda akanipa Siri ya kumuelewa BM3, au niende Orlando Pirates na Dc Motema Pembe alipowika? Laa hasha, Huko kote nitapoteza muda.
Ni kheri niishi Kwenye ukweli wa Francesca Lia Block, mwandishi wa Kimarekani aliyewahi kuandika kuwa "Magic can be found in stolen moments.” "miujiza hupatikana kwenye nyakati za wizi" ni kweli maisha ya Morison ni Miujiza, jamaa anatuibia
Mwandishi Morgan Rhodes katika kitabu chake cha "Frozen Tides" aliandika Magic will find those with pure hearts, even when all seems lost.” yani miujiza huwapata watu wasafi au hata wale wanaooneka muda wote wamepotea, hapa namuona kabisa Benard Morison.
Maisha ya Morison ni Miujiza, unapomchukia ndiyo anazidi kukuboa, Licha ya Kashfa nyingi zilizomchafua, nyakati ngumu alizopitia, lakini Dhahabu imeng'aa mchangani, BM3 ni Soka na soka ni yeye.
Unapozungumzia wachezaji 5 hatari Simba huwezi kumuacha, awapo Tanzania, hujisikia Nyumbani, si kwa utalii, bali ni kwa kipaji cha soka alichorithi kutoka kwa baba zake, ama kweli Kitanda cha Mzee Morison, Hakikuzaa Haramu. The Time is For Morison, lets enjoy his Beats.