Maisha ya Bernard Morisson ni Miujiza, unapomchukia ndiyo anazidi kukuboa

Maisha ya Bernard Morisson ni Miujiza, unapomchukia ndiyo anazidi kukuboa

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Kama ningalifuata usemi wa "Ya Kaisali Muachie Kaisali" basi ningebaki na donda lenye kudumisha deni la Roho yangu, na kama ningaliweza basi ningeenda pale Colombo Sri Lanka kwenye Kaburi la Sir Arthur Clarke mwanasayansi na mwandishi wa Tamthilia.

Aliyewahi kusema kuwa Magic is just a science that we don’t understand yet” kwamba miujiza ni sayansi tusiyoielewa" Huenda haya ninayowaza yakawa ni ndoto pia, tena ndoto ya kisayansi nisiyoielewa,

Naiwaza ile Tarehe 20 Mei 1993 kule Ghana Vijijini katika Familia ya wakulima alipozaliwa Benard Morison.
Natahamaki na kujiuliza ni wapi Walifukia kitovu chake, maana ana Nyota sana huyu, Nawaza nikifika kijijini Kpandu (Alipoanzia soka) nimuulize nani kuhusu BM3?

Au Niende Ashanti Gold alipocheza msimu mmoja kisha Niende AS VITA kwa Ibenge, Huenda akanipa Siri ya kumuelewa BM3, au niende Orlando Pirates na Dc Motema Pembe alipowika? Laa hasha, Huko kote nitapoteza muda.

Ni kheri niishi Kwenye ukweli wa Francesca Lia Block, mwandishi wa Kimarekani aliyewahi kuandika kuwa "Magic can be found in stolen moments.” "miujiza hupatikana kwenye nyakati za wizi" ni kweli maisha ya Morison ni Miujiza, jamaa anatuibia

Mwandishi Morgan Rhodes katika kitabu chake cha "Frozen Tides" aliandika Magic will find those with pure hearts, even when all seems lost.” yani miujiza huwapata watu wasafi au hata wale wanaooneka muda wote wamepotea, hapa namuona kabisa Benard Morison.

Maisha ya Morison ni Miujiza, unapomchukia ndiyo anazidi kukuboa, Licha ya Kashfa nyingi zilizomchafua, nyakati ngumu alizopitia, lakini Dhahabu imeng'aa mchangani, BM3 ni Soka na soka ni yeye.

Unapozungumzia wachezaji 5 hatari Simba huwezi kumuacha, awapo Tanzania, hujisikia Nyumbani, si kwa utalii, bali ni kwa kipaji cha soka alichorithi kutoka kwa baba zake, ama kweli Kitanda cha Mzee Morison, Hakikuzaa Haramu. The Time is For Morison, lets enjoy his Beats.

bm3gh-___CNXu6oeAtEJ___-.jpg
bm3gh-___CMrE30ZAeR5___-2.jpg
 
Morrison wala jamaa hana kashfa kama utopolo wanavyotaka aonekane.... Mie namuona tu ni mtu anayeishi maisha yake halisi to the fullest!
Hapendi kuonewa na anafanya kazi anayolipwa kuifanya. Period!
 
Chombo ya Fundi. Naskia simba wanataka kumperish away this season. Nawaambia watakua wametupa thahabu iliyokuwa ktk mikono yao.
 
Chombo ya Fundi. Naskia simba wanataka kumperish away this season. Nawaambia watakua wametupa thahabu iliyokuwa ktk mikono yao.
Kama kuna ukweli itakuwa kosa kubwa sana.

Tokea kaenda simba naona nidhamu ipo kiasi chake
 
Me namkubali sana huyu mwamba pamoja ni mjinga mmoja, ni mchezaji mzuri ila yuko emotional sana, na anahitaji uangalizi maana anaweza kuicost team mda wowote.

Simba impe mi5 tena ikifaa.
 
Morrison ni Fundi huwa napenda san wachezaj wenye mauwezo ya kuuchezea mpira na kuucheza, kwenye dribble na kutoa pas za kushtukiza pia yupo poa achilia mbal kutupia magol
 
Simba kumejaa wezi na vibaka tu! Huyo Morrison ni mwizi wa magari, Manara alifukuzwa kwenye cheo chake ccm kwa sababu ya wizi, yule aliye waita mbumbumbu, alipigwa mvua tatu kwa sababu ya wizi, maiko wambura nae mambo ni yale yale! Aveva na Kabulu!

List ni ndefu kweli kweli!!!
 
Simba kumejaa wezi na vibaka tu! Huyo Morrison ni mwizi wa magari, Manara alifukuzwa kwenye cheo chake ccm kwa sababu ya wizi, yule aliye waita mbumbumbu, alipigwa mvua tatu kwa sababu ya wizi, maiko wambura nae mambo ni yale yale! Aveva na Kabulu!

List ni ndefu kweli kweli!!!
Duh Ee bana ee....! Yaani huyu huyu Morrison aliyekuwa Mfalme pale Utopoloni Sasa Wana Utopolo Wanamnadi 'Eti Mwizi Wa Magari' Sasa Subiri akisikia hizi kashfa zenu Uto...Mtajuta kumfahamu 2nd leg VPL...!
 
Back
Top Bottom