Maisha ya Chuo na Kujitolea

Maisha ya Chuo na Kujitolea

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ni Moja kati ya Vyuo nchini Tanzania ambacho unaweza kusoma na kujitolea kufanya kazi pia.

Kwa wale waliosoma UDSM-SJMC watakuwa wananielewa kuwa kutokana na ile Televisheni,Radio na Gazeti wanafunzi wanaojitolea kufanya kazi hapo huwa wanapata kipato kinachowasaidia katika matumizi madogo madogo.

Mimi ni shahidi na walimu walikuwa wakisisitiza kujitolea kufanya kazi pale kwa ajili ya kupata uzoefu lakini pia kupata kipato.

Sasa wanafunzi wengi wakifika chuo wanataka maisha ya starehe, kwa pesa kidogo walizonazo.
Nimeshuhudia wengi waliokuwa wanajitolea pale wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa wako kwenye kampuni mbalimbali binafsi na serikalini.

Naomba nitoe ushauri kuwa mwanafunzi wa chuo unaweza kuanza kutafuta fursa ukiwa chuoni ili upate pesa ya kujikimu kimaisha.

Kuna kazi nyingi mfano hata kwenye baadhi ya mabasi ya mikoanj huwa yanatoa kazi ndogo ndogo ile mida ya jioni na huwa wanalipa vizuri tu kwa siku.

Lakini pia ukapita pita kwenye baadhi ya kampuni kuomba kujitolea baada ya muda wa masomo.
Usikae kizembe ukisubiri ajira zikufuate zitafute.
 
Shida ya kujitolea. Unakuta mtu yupo willing kujitolea, ila kampuni ikishaona huyu mtu kaja kujitolea ndio inakuwa kujitolea kweli.

Shida nyingine mtu kamaliza chuo, hana A wala B.
Yupo tayari kujitolea ili apate uzoefu ila mpaka nauli ya kwenda kujitolea hana.
Mtihani huo.
 
Wanapaswa kutoa nauli jamani
 
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ni Moja kati ya Vyuo nchini Tanzania ambacho unaweza kusoma na kujitolea kufanya kazi pia.

Kwa wale waliosoma UDSM-SJMC watakuwa wananielewa kuwa kutokana na ile Televisheni,Radio na Gazeti wanafunzi wanaojitolea kufanya kazi hapo huwa wanapata kipato kinachowasaidia katika matumizi madogo madogo.

Mimi ni shahidi na walimu walikuwa wakisisitiza kujitolea kufanya kazi pale kwa ajili ya kupata uzoefu lakini pia kupata kipato.

Sasa wanafunzi wengi wakifika chuo wanataka maisha ya starehe, kwa pesa kidogo walizonazo.
Nimeshuhudia wengi waliokuwa wanajitolea pale wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa wako kwenye kampuni mbalimbali binafsi na serikalini.

Naomba nitoe ushauri kuwa mwanafunzi wa chuo unaweza kuanza kutafuta fursa ukiwa chuoni ili upate pesa ya kujikimu kimaisha.

Kuna kazi nyingi mfano hata kwenye baadhi ya mabasi ya mikoanj huwa yanatoa kazi ndogo ndogo ile mida ya jioni na huwa wanalipa vizuri tu kwa siku.

Lakini pia ukapita pita kwenye baadhi ya kampuni kuomba kujitolea baada ya muda wa masomo.
Usikae kizembe ukisubiri ajira zikufuate zitafute.
Wakat niko mliman campus nimefanyaga kaz sana pale mliman. Nimepiga pale cinemax century nje kabisa ya taaluma. Kipato na experience mda uko chuo ni vigum sana kwemda sambamba. Unawz kupata kimoja kati ya hivyo!
 
Udsm iko vizuri sana.Sema inabidi tukomae
 
Safi wazo zuri.

Naomba kuongezea, sio lazima ajitolee.. aanzishe pia biashara ambayo anaweza kuimudu nje na masomo kutokana na kipato ambacho anacho au anaweza kuhifadhi.

Nilipokuwa chuo nimefanya kazi za ufundi wa computer na kuuza bidhaa ambazo wanachuo walikuwa wanahitaji. Ilinisaidia na kunipa ujuzi wa kufanya biashara pia kufahamu tabia za watu.
 
Safi sana. Tena ukiwa unajituma inakuwa vizuri zaidi.Mtu anaweza kuwa hata mpiga picha.
 
Hii sasa umeitaja kubwa.

Nilikuwa na camera naichezea kabla, baadae nikaamua kuitumia kwa business kwenye mahafali, birthday, matukio mengine na kupiga passport inalipa.
 
Back
Top Bottom