realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ni Moja kati ya Vyuo nchini Tanzania ambacho unaweza kusoma na kujitolea kufanya kazi pia.
Kwa wale waliosoma UDSM-SJMC watakuwa wananielewa kuwa kutokana na ile Televisheni,Radio na Gazeti wanafunzi wanaojitolea kufanya kazi hapo huwa wanapata kipato kinachowasaidia katika matumizi madogo madogo.
Mimi ni shahidi na walimu walikuwa wakisisitiza kujitolea kufanya kazi pale kwa ajili ya kupata uzoefu lakini pia kupata kipato.
Sasa wanafunzi wengi wakifika chuo wanataka maisha ya starehe, kwa pesa kidogo walizonazo.
Nimeshuhudia wengi waliokuwa wanajitolea pale wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa wako kwenye kampuni mbalimbali binafsi na serikalini.
Naomba nitoe ushauri kuwa mwanafunzi wa chuo unaweza kuanza kutafuta fursa ukiwa chuoni ili upate pesa ya kujikimu kimaisha.
Kuna kazi nyingi mfano hata kwenye baadhi ya mabasi ya mikoanj huwa yanatoa kazi ndogo ndogo ile mida ya jioni na huwa wanalipa vizuri tu kwa siku.
Lakini pia ukapita pita kwenye baadhi ya kampuni kuomba kujitolea baada ya muda wa masomo.
Usikae kizembe ukisubiri ajira zikufuate zitafute.