Maisha ya Dar vs Maisha ya mikoani


Kuhusu vyakula jitahidi uhudhurie masokoni maisha ni simple tu
 
Mjini pia ni shule bro
Nina brother ambaye alikuwa ni kama raw model wangu pale kijijini
Nilikuja town bila kurudi home kwa miaka mitano ndiyo bro akanitembelea siku moja nilimuona mtu aliyechelewa sana kwa karibu kila kitu
 
Baada ya maisha ya dar kunichapa kisawa sawa, siku niliyopata kaupenyo ka kuchomoka nakumbuka usiku huo sikulala nilikuwa nawaza kutakucha saa ngapi niukimbie huu mji.

Ila dar nikijaliwa uzima lazima nirudi tu, kwa tabu nilizozipata lazima nizifidie tu
 
Ahsante sana,Uzi umeumaliza kabisa
 
Ukiwa smart dar kuna maisha yakutoka chap
 
Mi naona pesa ya TASAF wapewe watu wa Dar. Hawana assets, nyumba za kupanga, mikopo ya magari. Mikoani wana nyumba zao hata kama za udongo. Wana ardhi za kulima na kupata chakula!
Kwahio hizi nyumba wanazopanga wamiliki wako mikoani? Kwa taarifa tu ni kwamba Dar ni mkoa wenye kiwango cha chini cha umaskini Tz nzima. Mikoani huko ndio kuna umaskini wa kutupwa.
Zaidi ya 80% ya pato la nchi linatoka Dar, mazao mengi ya chakula mikoani soko lao Dar. Dar hawalimi ushawahi kusikia kuna njaa? Njaa iko huko mikoani wanapolima chakula.
 
Hapa naona ni maelezo ya dar na vijijini mkuu umeambiwa mkoani we umeenda mkoani ukachagua vijiji ndo ukawa una vielezea
Hakuna mkoa wowote wa kuufananisha na Dar Tanzania hii acheni kujipa moyo pambaneni na maisha.
 
Dar chumba kimoja elfu 70
Umeme elfu 20
Maji elfu 10
Usafi na taka elfu 5
JUMLA KWA MWEZI 105,000
Kipato 220,00

Mikoani chumba kimoja elfu 30
Umeme elfu 5
Maji 2000
JUMLA KWA MWEZI 37,000
Kipato 350,000.
Watu wa mikoani Kwa kujipa moyo! Kwahio mkoani mishahara ni mikubwa kuliko Dar?!
 
Maisha ya dar starehe haziepukiki hali ya hewa sio nzuri kwa watu wanaoishi uswahilini ila mzunguko wa pesa ni mkubwa
 
Dar chumba kimoja elfu 70
Umeme elfu 20
Maji elfu 10
Usafi na taka elfu 5
JUMLA KWA MWEZI 105,000
Kipato 220,00

Mikoani chumba kimoja elfu 30
Umeme elfu 5
Maji 2000
JUMLA KWA MWEZI 37,000
Kipato 350,000.
Mkuu..NAKATAA

1. sio rahisi mtu wa 220000 kukaa room ya 70k kwa mwezi..Asilimia kubwa wanakaa vya 30, 40 au 50
2. Umeme 20k Dar na 5k mwanza sijajua kama ni uhalisia...Kwani price/unit kwa dar na mza inatofautiana?...Kuna watu wanalipa 5k au 10 umeme kwa mwezi.
3. Maji...10k ni ndefu sana..
 
Inaonekana wewe ni team mkoani...
 
Umeongea kwa hasira sana
 
Its over!. Case closed
 
Dar ni mkoa ambao unafunza watu maisha namna ya kuzisaka pesa.kila siku watu wanaamka mapema kama popo ili ilimradi siku isimpite bila tonge.
Dar maisha ni magumu iwapo utakuwa mtu wa kuamka kulala bila shughuli.
Dar hata kama ulikuwa mnene utapungua kwani kuna wakati utashinda njaa ili kuhakikisha watoto wanakula.
Dar ni jiji la mipango kama wewe hukuzoea kuumiza kichwa tafadhali enedelea kulala.
Dar watu wengi wanaishi kuijanja janja tu.
Hili jiji kwa kweli limenifundisha mengi maana niliacha elimu yangu baada ya kumaliza chuo nikaingia mtaani kusaka noti.
Asante sana dar umenilea japo udogoni mwangu umeifanyia mabaya mpaka leo hayatafutika.dar utaelendelea kuishi ndani ya moyo wangu kwa kuwa nina kumbukumbu mbaya na wewe.
Asante na tena shukrani dar.
 
Mpaka sasa hivi naona Maisha ya mikoani yanapigwa KO na maisha ya Dar...sasa wale ndugu zetu wanaosemaga vijana tutoke Dar twende mikoani ambako life ni easy mbona siwaoni?
 
Ukiweza kuishi DSM vizuri, basi unaweza kuishi popote pale nchini bila tatizo ikiwemo huko mikoani
Hyo ni Arusha mkuu ukiweza kuishi chuga popote unatoboa dsm maisha ni mchele ila hali ya hewa ndo ya kipumbavu kabsa
 
Bro...umeandika kwa hisia sana...pole kwa kumbkumbu mbaya za utotoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…