Maisha ya depo

Maisha ya depo

MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 13

Tuliondoka zetu mdogomdogo kama songi lisemavyo mpaka tukazikata kilomita zipatazo mbili tukapoza injini kwa tuliotangulia huku tukiwasubiri wenzetu.

Wakati tunajiandaa kurudi tulihesabu tena namba kwa kurudiarudia na tulisisitizwa kwa mara nyingine kuzikariri namba hizo ambazo idadi ilionekana kupungua ikilinganishwa na ile ya mwanzo UWANJA WA DAMU.

Tulihoji uhalali wa namba tulizohesabu awali tukiwa kikosini tukaambiwa tuachane nazo na tukariri hizi za wakati huu.

Hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kukubaliana nao ila mpaka muda huo tulishahesabu namba zaidi ya mara kumi hivyo haikuwa rahisi kuzisahau na kukariri nyingine kila wakati.

Tuliianza safari ya kurejea kikosini na nyimbo mbalimbali na wakati tunakalibia MAHANGANI wimbo ulibadilika ukawa unasikika uliotoholewa kwenye ule maaruufu wa “Jua lile literemke mama” ikawa kama hivi,

“Mwanzilishi: Ewii
Wote: Ewaaa

Mwanzilishi: Ewii
Wote: Ewaaa

Mwanzilishi: HANGA lile literemke mama
Wote: HANGA lile literemke mama

Mwanzilishi: Ayaya iya iya mama
Wote: Ayaya iya iya mama

Mwanzilishi: Ndo lile HANGA ndo lile, ndo lile HANGA ndolilema
Wote: Ndo lile HANGA ndo lile, ndo lile HANGA ndo lile mama

Mwanzilishi: Ndo lile HANGA ndo lile, ndo lile HANGA ndolilema
Wote: Ndo lile HANGA ndo lile, ndo lile HANGA ndo lile mama”.

Tulifika MAHANGANI tukiwa tumechoka vya kutosha, tuna majasho, mavumbi na matongotongo machoni hivyo basi ratiba iliyopo mbeleni ilikuwa ni usafi ingawaje siyo wote tulioizingatia.

Kwa kuwa nilishaanza kujiona nimekuwa mwenyeji sikujisumbua kwenda kupanga foleni nilijituliza kitandani kupunguza uchovu uliotokana na MABIO kama ilivyokuwa Baraka.

Nikiwa nakaribia kupata usingizi ghafla nikastuliwa na filimbi zilizokuwa zikipulizwa mfululizo MAHANGANI walikuwa ni waheshimiwa wa jeshi la akiba waliokuwa wakitusisitiza kuelekea KOMBANIA.

TULIFOLENI tukiwa na mafagio pamoja na ndoo tukagawanywa kwenye maeneo mbalimbali kwenda kufanya usafi na tulipomaliza tulirudi MAHANGANI kwa ajili ya usafi binafsi.

Nilifika moja kwa moja sandukuni na kutoa mswaki na dawa ya meno nikaenda KUFOLENI kwenye mabomba kwa ajili ya kuteka maji kwa ajili ya kusafisha uso.

Bombani hali haikuwa nzuri kwani mabomba yalikuwa ni machache na maji yalikuwa yakitoka kwa kasi ndogo hali iliyopelekea kuwepo kwa msururu wa watu mabombani.

Kwa sisi ambao hatukuwa na uhitaji wa maji mengi yaani tulikuwa na vikombe tu kwa aajili ya kunawa uso tuliruhusiwa kukinga pasi na kupanga foleni japo tulipokuwa wengi ikawa kero kwa wale wenye ndoo kwani ndoo zao zilikuwa hazipati muda wa kukingwa badala yake ilikuwa ni toa kikombe weka kikombe.

Baada ya kuumaliza mchakato huo nilirudi zangu sandukuni na kurudisha nilivyovitoa na kuitwaa simu niliyoikuta na missed calls 12 zote zikitoka kwa Linda na meseji karibia 7 huku zikitoka kwa Linda, 1 ya wasafibet, 1 kutoka sportpesa, 1 kutoka ofa kabambe, 1 ya 15572 na nyingine kutoka 15570 kifupi simu yangu ilipendeza.

Nilifungua meseji za Linda ya kwanza ilisomeka, “Hello K mbona hupokei simu mpenzi wangu?” na nyingine ilikuwa ikisema,

“Najua simu zangu unaziona ila hutaki kupokea vibaya ivyo hata kama hunipendi ndo usipokee simu zangu, sawa bana mimi nimeshaanza safari nakuja huko nikuletee nini”.

Huwezi amini mwanaume bila kujifikiria nikajikuta namjibu “Eat some more na Pepsi ya take away kubwa” yaani nilikuwa kama kichaa mwenye rungu mkononi niliagizia kana kwamba nimempa hela mdogo wangu Uledi akaninunulie dukani.

Hali ilikuwa ni mbaya maana chakula cha MZABUNI nilianza kukikinai hivyo basi nilipokutana na fursa kama hiyo ya kubadili radha kidogo kutoka mtaani sikutaka inipite.

Mara baada ya kutoa majibu hayo akili ikakaa sawa nikapata nafasi ya kuangalia muda niliyotumiwa ujumbe nikagundua kuwa ile ya kwanza ni zaidi ya nusu saa limepita ila hii ya pili ndo kwanza ina dakika mbili.

Nikiwa natizamia hilo ghafla simu iliita namba niliyosevu “Linda Babe” nikapata kigugumizi kuipokea mpaka pale ilipo kata ila hakukata tamaa baada ya kukatika simu ile alipiga tena.

Nilipokea nikakutana na maneno yaliyoniacha kinywa wazi kwani ni kama alikuwa akinisuta mana aliniambia,
“kwahiyo kisa nimekwambia nikuletee nini ndo umeamua kujibu ila simu zangu na text nyingine wala hukuziona”.

Nilijikaza na kamuelezea hali ilivyokuwa kwamba simu ilikuwa sandukuni na mimi nilikuwa kwenye FATIKI hivyo sikuwa nayo ndiyo maana sikupokea.

Alinitaka niwe nayo muda wote mpaka pale atakapofika kikosini nilipomwambia tunakatazwa kutumia tukiwa kwenye FATIKI aliniambia nijiibe aliamini kuwa kama iliwezekana kufanya hivyo tukiwa shule basi huku nako inawezekana kabisa.

Kifupi alikuwa ni king’ang’anizi balaa ilinibidi nimkubalie kwa lengo la kumzuga akate simu mambo ili mengine yaendelee, aliikata simu nikaizima na kuitupa sandukuni na kulifunga.

Muda ulipowadia zilipigwa filimbi za kutosha tukamiminika KOMBANIA ambako afande wa zamu alikumbushia namba zake wakati wa kurudi kwenye MABIO akadaka watu wake aliowarusha kichurachura na adhabu nyingine ndogondogo mpaka pale tuliporuhusiwa kwenda saiti kubeba vifusi.

Safari hii tulikuwa na Afande mmoja aliyekula chumvi ya kutosha jeshini aliyefahamika kwa Jina la Mtalibani kama a.k.a yake kikosini hapo.

Mtalibani yeye alitutaka tupeleke vifusi ndoo zipatazo tano na akateua WAZALENDO ambao walikuwa kama makarani yaani waliandika majina na kutuhesabia idadi ya ndoo tunazomwaga.

Afande huyo ambaye cheo chake ni Mteule wa jeshi kule saiti kunakochimbwa vifusi aliwaachia SERVICE MEN na huku kunakomwagwa vifusi alisimamia shoo yeye mwenywewe.

Katika moja ya tukio ambalo sijalisahau moja ya MZALENDO aliyekuwa karani alimjazia jamaa yake kuwa keshamaliza ndoo zote tano ilihali wengine ndo kwanza tumejaziwa ndoo mbili mbili.

Mtalibani pale tu alipoishika ile karatasi na kuligundua hilo aliichana akamkamata yule karani akaanza kumpa mibanzi na ngwala mfululizo na kwa vile palikuwa na vifusi visivyoshindiliwa eneo hilo itoshe kusema vumbi lilitimka.

Hakukuwa na wakugombelezea kutokana na gap la cheo cha Afande huyo na sisi japo tulimhurumia MZALENDO huyo ambaye muda wote alikuwa akishambuliwa bila kujibu mashambulizi.

Ilikuwa ni mfano wa litakavyokuwa pambano baina ya Karimu Mandonga-Mtu kazi dhidi ya Selemani Kidunda-Jini Makata.

Kwa bahati eneo tulilokuwa tukimwaga vifusi lilikuwa karibu na ofisi za mapokezi zilizokuwa karibu na zahanati ya kikosi hivyo afande mmoja alisogea na kugombelezea ugomvi ule na kumwambia MZALENDO yule akimbie waliko wenzie yaani kule vinakochimbwa vifusi.

Afande yule ambaye alimtuliza Mtalibani na kutuambia kuwa tukamwambie jamaa abaki kulekule na asipandishe mpaka FATIKI ile itakapoisha. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

******Itaendelea……………………………………………...
MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 14

Habari hizi zilipofika kule saiti SERVICE MEN walitusimulia taarifa kuhusu mzee yule ambaye inasemekana alipigana vita ya Kagera dhidi ya Ndui Iddi Amini.

Lakini pia alihudumu katika kikosi cha mizinga achana na kile cha wakina Songa na Kalapina hapana alilitumikia jeshi katika kitengo cha milipuko yaani kikosi cha kulipua mizinga ama mabomu kwa lugha nyepesi.

Nilirejea matukio aliyokuwa akiyafanya kweli alionekana ni mtu aliyewehuka kitu ambacho si ajabu kwa wale wanaoishi katika mazingira yanayokumbwa na vita ama kwa wanajeshi wanaohudumu vikosi kazikazi haswa vile vya milipuko.

Ulipofika muda wa chai tulienda kunywa na baadaye tukajipeleka KOMBANIA kama ratiba ilivyokuwa ikitaka.

Safari hii lilitambulishwa kundi jipya la WAZALENDO waliokuja na Afande Mbega ambalo ndani yake alikuwepo mwanadada ustadhati aliyejitambulisha kwa jina la Rehema ambaye alikuja KOMBANIA akiwa amejisitiri yaani ile stara ya Zanzibar kabisa achana na hii ya Magomeni-Kagera au Ubungo-Riverside.

Afande Mbega alitukuta tukiwa na Afande Rashidi ambaye alimhoji “kulikoni” Afande Mbega akamjibu kuwa wamemshauri na kumshawishi sana lakini juhudi zao zimegongaa mwamba kwahiyo ni muda wa maafande wa zamu nao kwa wakati wao.

Afande Rashidi akamwambia “kama nyie mmeshindwa sisi ni nani tuweze kozi itakavyomnogea atabadilika mwenyewe tu”.

Tulibaki kumshangaa Ustadhati huku wengine wakinong’ona juu yake na kumuona mwamba kabisa kwa misimamo yake mana si kazi rahisi kwenda kambi ya jeshi na kuwapangia vile utakavyo haswa kwenye mavazi.

Tulipiga soga za hapa na pale na baada ya muda alikuja Afande wa zamu ambaye alikuwa ni BAKABAKA naye alipofika alionekana kutabasamu na kucheka kutokana na kuwepo kwa mwanadada mwenye msimamo wake alimsimamisha na kuongea naye mambo kadhaa na baadaye akamruhusu kukaa chini.

Afande yule wa zamu aliyekuwa katika sare yenye munekano tofauti na zile nilizoziona mpaka kufikia siku hiyo alituambia kuwa kutokana na kikosi kupata Askari kama huyo ambaye kwao ni kama Malaika aliyeletwa kuja kutukumbusha kuacha maovu na kutenda mema basi wameamua kutupatia UTAWALA BINAFSI.

Baada ya kusema hayo Afande huyo aliondoka na kutuacha na Afande Rashidi ila wote tulishikwa na butwaa tusijue ni kipi kinaendelea.

Tulimuuliza Afande Rashidi alichomaanisha Afande yule wa JWTZ alitushangaa na kutujibu,
“MANANGA nyie ina maana mpaka leo hamjui maana ya UTAWALA!”.

Akaendelea kusema “Kumbe ndiyo maana Afande aliposema hivyo hakuna hata mmoja aliyeshangilia ajabu”.

“Tuambie basi Afande ili siku nyingine ikitokea tushangilie” mmoja wetu alimwambia Afande Rashidi.

Afande alituambia “UTAWALA BINAFSI kwa Askari yeyote haitofautiani na kile kipindi pendwa kwa mwanafunzi yeyote aidha wa chekechea ama wa chuo kikuu sijui mmenielewa?”.

Afande alituacha njia panda kila mtu akiwaza lake juu ya fumbo alilotuachia nilimkumbuka mwalimu wangu wa Baiolojia kidato cha tatu Mwalimu Msuya ambaye kuna topic moja alikuwa akiita topic pendwa.

Nakumbuka ilikuwa kama kuna kipengele cha topic fulani (mfano Excretion) anakifundisha siku hiyo na kimeelezewa pia kwenye hiyo topic pendwa basi anakigusia juu juu halafu utamsikia, “tutakuja kukisoma vizuri kwenye topic yetu pendwa” yaani Reproduction.

Si mimi tu bali wengi wao akili zetu ziliwaza hivyohivyo japo si wote, bado tulibaki na maswali ni vipi sasa huo uzalianaji (yaani Reproduction) unahusika hapo jeshini ina maana hicho ni kipindi cha kuwekana mapedeli nini.

Kwa kuwaza hivyo tayari nishaanza kumuona Abdala Kichwa Wazi (yaani K mdogo) ameanza kupandisha mnara na kwa wakati huo ulikuwa ukisoma H+ ama kweli upwiru ni mbaya.

Afande Rashidi naye ni kama alianza kushtukia jambo baada ya kusikia minong’ono ile ikabidi atuulize kuwa ni nani angeweza kutuambia kipindi hicho pendwa ni kipi ndipo nikajikuta naropoka kwa sauti ya nne “Reproduction” aliposikia hivyo Afande Rashidi aliangua kicheko kilichowapelekea na wengine kucheka pia.

Afande Rashidi alisema “Duuh yaani nyie ndo mmefika huko kipindi pendwa si Mapumziko jamani au hamjawahi kumsikia Bwakila na Mkude Simba, mnawaza ngono tu huo ugwadu wenu utawauwa mbona umewashika mapema hivyo wakati mmetoka kwenu juzi tuu hapo”.

Nikamsikia mtu akidakia na kumjibu “Ndiyo utuambie sasa afande umeona watu wameanza kufukua makaburi”.

Afande sasa akafunguka “Yaani mkiambiwa UTAWALA BINAFSI kwa maana fupi hamuendi kwenye FATIKI badala yake mnapumzika bila ya kufanya kazi yoyote.

“Hivyo basi mtaenda zenu MAHANGANI mkapumzike mwenye kufua akafue wa kuoga akaoge kama utaenda kulala kalale na wale wenzangu na mimi wenye miwasho sehemu zao wanaruhusiwa kwenda kuzikuna, yaani muda huo jeshi halikupangii cha kufanya”.

Alituzungusha vya kutosha mpaka anatupatia maana ya neno hilo, nilikuwa na swali ila nikasita kuuliza maana nilishaanza kujiona sasa nimekuwa NANGA LA DEMO haswa nikifikiria tukio nililotoka kulifanya na kupelekea KOMBANIA nzima kucheka.

Nilikumbuka pia ule usiku wa kwanza nilipokuwa kituko na kuvunja mbavu raia wakati wa kuhesabu namba walipoitwa MADAWILI na mimi nikaenda kuhesabu nao hivyo ikanijia hofu mana kila tukio ninalolifanya mbele za watu linaisha kwa kuniaibisha.

Baada ya muda kupita Afande alituruhusu na kututaka tukutane baada ya mlo wa mchana yaani “Kila baada ya kula ni KOMBANIA” haijalishi mna UTAWALA BINAFSI au laa maana hakuna UTAWALA BINAFSI mrefu hivyo na ukitokea basi mtakula nusu na nusu nyingine mtaenda kuipatia KOMBANIA.

Basi tuliubonda zetu UTAWALA mpaka pale ulipoisha na kuelekea tunakostahili kuwepo ambako idadi ya watu ilizidi kuongezeka si tu kadri siku zilivyokuwa zikisogea bali kila dakika iliyokuwa ikiondoka ndivyo watu walivyokuwa wakiongezeka. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

**************Itaendelea……..……………………...
 
EPISODE 15

TULIFOLENI tukiwa na Afande Rashidi aliyekuwa akisaidiana na Afande Devi, tukiwa tunasubiri maelekezo ni kipi kifanyike Afande Devi alianza kuwatoa mbele waliokuwa na nywele ndefu.

Afande Rashidi alituambia,
“Yaani mmepewa UTAWALA badala ya kwenda kufanya usafi wa mwili mkaenda kukuna AMALA zenu” walicheka wachache miongoni mwetu ila wengine tulikaa kimya maana tulisikia msamiati uliokuwa mpya kwetu.

“Mkipewa UTAWALA nyie WAZALENDO kitu cha kwanza ni kwenda kufanya usafi wa mwili wako na mavazi kulala na hayo mengine ni baada ya kumaliza usafi” aliongeza afande Rashidi.

“Hembu fikiria siku zote hizo zilizopita kuna siku afande yeyote aliwaambia nendeni mkaoge au mkafue WAZALENDO, eti nyie si nawauliza”.

“Hapana Afande” tulimjibu akaendelea kusema,
“Haya waoneni wenzenu kule na rasta zao kichwani kama wajamaika” tuliangua vicheko aliposema hivyo maana hao wanaoambiwa wana rasta kichwani walikuwa na mipara ya kwenda.

“Mnacheka WAZALENDO zile nywele huku jeshini ni rasta yaani kama umenyoa leo baada ya siku tatu unatakiwa unyoe tena zishakuwa rasta hizo”.

“Niwaulize swali WAZALENDO”
“Uliza afande”
“Kipara kimoja hunyolewa kwa dakika mbili, je vipara vitatu vitanyolewa kwa muda gani?” alituuliza swali hilo la kizushi afande Rashidi huku akiwa anatabasamu.

“Atakayetoa jibu sahihi badala ya majawabu namtandika UTAWALA BINAFSI aende akajitawale HANGANI” aliendelea kukazia afande huyo.

Kwakuwa tulishaonja radha ya UTAWALA na kuufaidi utamu wake kila mtu alinyoosha mkono kutaka kujibu ili akale zake bata kwenye deka za jeshi.

Afande Rashidi kuona wingi wa mikono iliyonyooshwa akasema,
“Ina maana swali langu limekuwa jepesi kiasi hicho sawa ila nataka jibu siyo mnipe majawabu”.

Afande Rashidi alianza kuyapokea majibu ambapo watu wote watano waliochaguliwa walijibu sawa kuwa “Kipara hakinyolewi”.

Afande akatuambia “Ina maana nyie wote jibu ni hilohilo moja hakuna lingine, oya na nyie wajamaika huko mnakubaliana na hawa jamaa zenu huku”.

Marastafari wale kwa pamoja wakajibu “Ndiyo afande”.

Afande akasema “nyie kweli MANANGA na form six yenu basi mnajikuta mnajua kuchemsha bongo haya bana, hakuna mwenye jibu la tofauti na hilo lililokuwa sahihi nimtandike UTAWALA?”.

Kaukimya kalitawala sijui nikapatwa na nini nikajikuta nanyoosha mkono juu afande akaniuliza kama nina jibu jipya ama ni lilelile nikamjibu ni jipya akaniruhusu kujibu.

Nikamwambia “Vipara vitatu vitanyolewa kwa dakika sita afande” umati wote wa WAZALENDO uliangua kicheko ndipo akili zikanirudi eeh kumbe nimetoa boko tena.

Afande aliniuliza kama nina uhakika ikabidi nikaze na kumjibu kwa herufi kubwa “NDIO”.

Aliendelea kuulizia kama kuna jibu lingine ndipo akanyoosha dada mmoja na kujibu kama nilivyo jibu mimi nafsi ikapata Faraja kwa kuanza kupata wafuasi.

Kukawa na pande mbili sasa hivyo afande aliuliza wanaounga mkono jibu la mwanzo ama langu.

Tulikuwa wanne pekee katika umati ule ambao tulisimama na jibu nililolitoa na kati yetu mwanaume nilikuwa peke yangu na MADAWILI watatu ilibidi afande atutenge.

Afande alichokoza mjadala na kusema,
“Kwahiyo nyie mnafikiri kama mtakuwa mmepata tutawapa UTAWALA wote na kwenda kwenye FATIKI na hawa wanne”.

“Why not” ilisikika sauti ya kwanza kutoka kwenye kundi lililokuwa likiliunga mkono jibu la kwanza.

“Eeh UTAWALA kidogo tu mshaanza kuongea na kizungu” nilijikuta nimeropoka na kuwafanya wacheke kana kwamba wameiona nanihii yangu.

Afande akaniuliza “hivi jibu lako umelipataje hembu tuambie”.

“Anhaa of course yes nimechukua vipara vitatu nikazidisha na dakika mbili nikapata dakika sita ndiyo nikanyoosha mkono na kukupatia jibu” nilianza kugain momentum kwa wakati huu nikawa mchekeshaji pale KOMBANIA mana niliendelea kuwavunja mbavu.

“Kwahiyo umetumia table ipi ya pili au ya tatu?” aliniuliza afande Rashidi.

“Ah hapo ni table ya tatu si tatu mara mbili ni table ya tatu afande”.

Walizidi kucheka wanazengo afande Devi nayeye akauliza “We mwanangu ni kombi gani kwanza?”.

Nilisita kidogo nikamjibu “EGM mwanauchumi kabisa”.

Nikasikia mngurumo wa sauti ya nne ukisema “tangu lini tena” alikuwa ni Ambrose niliyekuwa nikisoma naye HGK tulipokuwa advance.

Nilimsikia afande Rashidi akisema,
“Apo sawa kumbe umesoma hesabu ndiyo mana umetoa jibu la kimahesabu hesabu mana hawa HGK na HKL wametoa majawabu na wanaungana pamaja”.

Hakugundua tu ila moyoni nilimmaindi kwa kusema vile maana hata mimi mwenyewe nimesoma HGK nilimdanganya tu pale kuwa nimesoma EGM hivyo niliona kama katusema ma HGK kuwa hatuna akili.

Afande alituchanganya kwa wenzetu akatuamuru tuketi chini kwenye zulia la jeshi akatupangilia kwa kusema “WAZALENDO chukueni hii kipara kinanyolewa, asikudanganyeni mtu kuwa kipara hakinyolewi jeshini ni sehemu pekee ambayo vipara vinanyolewa”.

Tayari nilishakumbwa na furaha mpwite mpwite maana kwa mbaali nilishaanza kuinusa harufu ya UTAWALA.

Afande aliendelea kunena kwamba, “Ndiyo maana tukawaambia wale,wajamaica kule waende wakanyoe mana vile ni vipara kweli ila nywele zimeshakuwa kubwa mno hakuna namna ukakaa na nywele zaidi ya siku tatu jeshini haswa kwenye kozi bila kunyoa hilo ni kosa kubwa”.

Afande aliendelea kukazia,
“narudia tena jeshini ni sehemu pekee ambayo vipara vinanyolewa na ndiyo maana namtangaza swahiba yangu pale mwana uchumi na mahesabu kuwa mshindi wa challange yetu nyie wengine endeleeni kukalili hadithi za Kinjektile Ngwale na Chifu Mkwawavinyika wa vita ya majimaji”.

Baada ya Afande kusema hivyo nilisimama na kunyoosha mikono juu mfano wa mchizi wangu Mrusi bingwa wa mapambano asiyepigika Boyka anavyofanyaga ulingoni baada ya kushinda pambano.

Nilizunguka pande zote za dunia mikono ikiwa juu mithili ya sanamu wa konyagi nikajikuta nawaambia “pigeni makofi basi” nafikiri ni wale tu watatu waliokuwa wakiniunga mkono ndiyo waliofanya hivyo maana niliyasikia kwa uchache mno.

Nilimsikia Afande Rashidi akisema “Kumbe mchumi wetu naye mwehu haya mpigieni makofi mwenzenu achene wivu” hapo niliyasikia ya kutosha namimi nikawa nayasindikiza kwa kutingisha kichwa yaani kama ni upele ulimpata mwenye kucha kazi ikawa ni kujikuna tuu.

Mwisho wa pongezi hizo nilikaa chini afande Rashidi akasema “Ila mwanangu unafaa sana twende kwenye FATIKI ukatuchangamshe mana kazi ikiwa ngumu tukafurahi kama hivi inakuwa nyepesi kabisa”.

Aliendelea kusema “Leo waache hawa wadada wakalale we twende tu kwenye FATIKI”.

Nilimjibu kwa sauti ya huruma “Aaah afande nipe UTAWALA wangu kumbuka nimeutolea jasho” watu waliangua vicheko lakini mwisho wa picha tukaruhusiwa na wale wadada na kwenda kuubonda zetu UTAWALA tukiwaacha wenzetu KOMBANIA wakijiandaa na mauzauza ya vifusi. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

*************Itaendelea……………………………...
 
EPISODE 16

Nilipofika HANGANI nilizingatia aliyoyasema Afande Rashidi nilikoga zangu na kufua kabla ya kujitupia zangu kitandani maana mazingira yaliruhusu kufanya hivyo kwani hakukuwa na foleni ya kuteka maji hivyo ikawa rahisi kuyafanya hayo.

Nilifika kitandani nikaitwaa simu yangu nikawa nachati na mtoto Linda ambaye bado alikuwa safarini na muda huo alikaribia kufika maana alikuwa keshashuka kwenye basi la mkoani na alibakiza gari moja afike kambini.

Nilijipakulia minyama na kumwambia kuwa nimejiibaiba sijaenda kwenye FATIKI ili niwasiliane nay eye kumbe mlume nilikuwa najitawala zangu.

Nilibonda usingizi wa tani za kutosha ambao ulikuja kusitishwa na makelele ya wanangu waliotoka kupigika kwenye FATIKI wana walikuwa wakihangaikia maswala ya usafi nikawa nawazoom kwa mbali kwani nilishafanya hivyo karibia masaa mawili nyuma.

Alikuja kunitania Baraka nilivyokuwa najichetua tulipokuwa KOMBANIA akisema kuwa ananionaga mpole siku zote hakutegemea kama ningekuwa mcheshi kiasi kile, alinisimulia pia jinsi nilivyokuwa nikizungumziwa kwenye FATIKI.

Mchizi Ambrose naye ambaye aliyekuwa akikaa HANGA tofauti na nililokuwa nikikaa alinitembelea hakutaka kusubiri muda wa KUFOLENI kwenye msosi wala KOMBANIA.

Mzigua huyo swali lake kubwa lilikuwa ni lini na wapi huko nilikosomea EGM, nikamuelekeza jinsi nilivyoumia tulipoambiwa kuwa HGK ni vilaza ila ilibidi nishikilie bomba tu kuwa nimesomea uchumi.

Stori zilinoga mpaka ulipofika wasaa wa MZABUNI tukasogea kwenda kupata kilichoandaliwa na kwenye foleni ya chakula sikukaa sana maana nilishakuwa maarufu kila mtu alitaka kuniongelesha ama kunipa mkono na wengine walikuwa wakinipisha kwenye foleni.

Nilichukua zangu cha mtume na kwenda kukifinyia kwenye MESI ya KIZALENDO ambayo haikuwa na jengo wala viti yaani chini ya miti.

Tukiwa tunakula nikaliona kundi la WAZALENDO lililokuwa limebeba magodoro, kwa uzoefu wangu wa siku mbili zile nilijua ni wageni ilibidi niwazingatie huenda ningefanikiwa kumuona Linda ila sikumuona.

Nilipomaliza niliosha vyombo vyangu na kuvirejesha HANGANI tulikopumzika kwa muda mpaka pale muda wa filimbi ulipofika tukajazana KOMBANIA.

Kunako KOMBANIA utaratibu ulikuwa ni uleule tulipiga makofi na kuimba nyimbo mbalimbali kama wanafunzi wa chekechea waliokuwa wakisubiri muda wa uji ufike.

Wakati huu tulikuwa na afande maarufu kwa jina la Afande Maku ambaye alituimbisha kasongi haka,

“Afande Maku: Malela Malela lela msondo eeh, Malela Malela lela msondo eeh, Malela na Msondo eeh Malela na Msondo eeh Malela na Msondo Mayasa

Sisi: Malela Malela lela msondo eeh, Malela Malela lela msondo eeh, Malela na Msondo eeh Malela na Msondo eeh Malela na Msondo Mayasa

Afande Maku: Siwezi kusimamisha mnazi eeh tapigwa na afande eeh tapigwa na afande Mayasa

Sisi: Siwezi kusimamisha mnazi eeh tapigwa na afande eeh tapigwa na afande Mayasa

Afande Maku: Ewiii
Sisi: Ewaah
Afande Maku: Wiii
Sisi: Waah
Afande Maku: Camon baby kiss me camon
Sisi: Oooh
Afande Maku: Camon baby kiss me camon
Sisi: Yaah”.

Afande alikuwa akiimba wimbo huo huku akiwa ameinyanyua pisi moja yenye upara wake na kucheza naye staili fulani hivi miondoko ya bluzi, mwanadada naye aibu hazikuwa shida zake sijui kujiamini kule alikutoa wapi nahisi alishakuwa mwenyeji aliyezoea maisha ya pale kutuzidi wengine.

Wakati yanaendelea hayo tuliingiliwa na ugeni kutoka ngazi za juu ukiongozwa na makamu mkuu wa kikosi Matroni Neema Ndunguru yeye alikuwa akijiita “daboli N” akimaanisha double N.

Ajenda yake kuu ilikuwa ni kutukaribisha kikosini na kuzijua changamoto tunazokumbana nazo kikosini hapo.

Matroni aliambatana na Koplo Jose ambaye yeye alikuwa kitengo cha dukani kama utamkumbuka vizuri ni yule aliyetugawia pipi mara baada ya kutupa adhabu ile siku niliyowasili kikosini hapo.

Baada ya kutupa maneno ya faraja kulingana na changamoto zetu sasa ulifuata wasaa wa biashara mana kwa sisi tuliosomea uchumi ingekuwa ni ajabu meneja mkuu wa kampuni kuambatana na meneja masoko kwenye hadhira yeyote halafu wasijipigie pande kwa kutangaza bidhaa zao.

Makamanda hao walianza kuulizia wasiokuwa na ndoo tukanyoosha mikono juu, wasiokuwa na vyandarua sikukosekana mkono ukapanda juu tena wakauliziwa wasiokuwa na mafagio nikavunga maana nilikuwa nalo.

Wakaulizia wasiokuwa na viatu vya mvua (Rain boot) bado nikawemo na vingine vingi vikauliziwa kwa sehemu kubwa nikajikuta nanyoosha mkono kila mara kana kwamba ule wimbo wa mkono juu wa wale jamaa kutoka kundi la maandishi matatu niliimbiwa mimi.

Baada ya kutuuliza hivyo wakataka kujua sababu zilizopelekea kutokuwa navyo wakawepo waliolipia vitu hivyo lakini hawakupatiwa kwa kuwa viliisha dukani ila majina yao yaliandikwa kwenye daftari la kumbukumbu.

Wakawepo wengine waliopotelewa, tukawepo sisi tulioibiwa na wale wasiokuwa na hela ya kununulia wakidai kuwa wametumia kwenye nauli na kununulia vitu vingine.

Suluhisho likawa waliokwisha lipia na hawajapatiwa walitakiwa waendelee kusubiri na pale vitakapofika watafahamishwa ila pia walitakiwa kwenda dukani mara kwa mara kuulizia kama vitakuwa vimekwishaletwa.

Kwa sisi tuliopotelewa ama kuibiwa tuliishia kupewa pole na kuambiwa kuwa makini na wepesi maana jeshini wizi hauruhusiwi na atakayegundulika atafurushwa mara moja haijalishi yeye ni nani.

Matroni alituambia kuwa kitu ambacho kinachoruhusiwa jeshini ni kuhamishiana na ndiyo maana tunatakiwa kuwa wepesi na kuongeza umakini.

Kwa kiasi kikubwa matron alikuwa akikazia mno neno wepesi kwa waliokuwa na akili za kuku ni vigumu kumuelewa labda kwa wale jamaa zangu wa Cuba wangeweza kumuelewa.

Neno hilo linakuja kueleweka vizuri pale aliposema “jeshini hatuibiani ila tunahamishiana” kifupi alimaanisha ukihamishiwa na wewe tafuta mnyonge wako umhamishie ila usionekane.

Matroni aliendelea kuwaambia wale waliodai kuwa wamemalizia hela kwenye matumizi mengine waendelee kuwasiliana na wazazi wao nyumbani wawatumie ili wanunue vitu hivyo maana ni muhimu sana kuwa na vifaa hivyo wakati kozi inaendelea kama vile chandarua.

Maafande hao waliokuwa wakiongea kwa kupokezana kama washereheshaji wa Sinema Zetu Filam Festival waliendelea kusisitiza kuwa kama yupo ambaye ataomba hela nyumbani na asitumiwe kutokana na changamoto za kiuchumi nyumbani basi asijali aende dukani atapewa bure kabisa.

Msaada huo uliambatana na sharti kuwa mtu huyo anatakiwa aliorodheshe jina lake kwenye daftari kwa lengo la kutunza kumbukumbu kusudi ya kuwa isije onekana wauzaji wanalihujumu duka.

Ama kweli usilolijua ni usiku wa giza huu ulikuwa ni mtego ambao ulihitaji akili nyingi kuugundua ila kwa kifupi ni kuwa hakuna cha bure chini ya jua.

Maafande hao waliendelea kusisitiza umuhimu wa kuwa na chandarua maana mbu waliopo kikosini hapo nao wameenda kozi tukifanya masihara tutakwenda na maji kwani wapo waliokatishwa uhai na mbu hao.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

**************Itaendelea………………….....
 
Mbona umerudia hiki kipande tyr
 
EPISODE 17

Baada ya kumaliza nilimsikia afande Jose akiniita nikamuitikia “Nipo afande” akaniambia “DABO” nilibaki kuduwaa nisielewe alicho kimaanisha.

Baada ya kusita kwa muda nikamsikia akisema “Acha MAPUUZA MZALENDO kamanda wako anapokuita inakubidi utii bila shuruti au unadhani umeitwa na Bambo”.

Kauli hiyo ilinifanya niamini kuwa alinitaka niende pale alipo ikanibidi nisimame na kwenda kumfuata ambapo pia alikuwa akinisisitiza kwa kusema “FANYA GHAFLA”.

Nilifika pale alipo na kunitaka nipunguze urefu nikafanya hivyo, alinihoji kuwa kwanini nina MAPUUZA ninapoitwa na afande nikamjibu kuwa sikumuelewa alichokuwa amekisema.

Akaniangalia kisha akasema ni kipi sijaelewa nikamwambia sikumuelewa aliposema DABO akaendelea kunitizama kisha akanitaka nisimame na kuniambia “KUNJA NGUMI”.

Kichwa kilianza kupata moto nikajiuliza kwanini nifanye hivyo anataka tupigane tena, sikuwa na jinsi ikanibidi nizikinge usawa wa uso kuonesha kuwa tayari kwa lolote.

Nilimsikia afande akisema “unataka tupigane sawa nipige mimi siwezi kupigana na wewe kwanza ni makosa kupigana na msomi” WAZALENDO wakawa wanacheka baada ya afande kusema hivyo huku nikiwa nimeukinga mkono huku nimepandwa na jazba kutokana kejeli zake.

Afande aligundua kuwa nimeshapaniki hivyo alimuita ST. Fred na kumwambia “hembu tuoneshe DEMO mana hili NANGA naona lishajaa gesi lisije likanipasua macho”.

Koplo alimwagiza Fred afanye kama alivyoniambia ndipo akazikinga na kuziweka juu ya ardhi mithili ya mtu aliyekuwa akipiga pushapu.

Afande alikuwa akimwambia “juu” akawa anaupandisha mwili juu na alipokuwa akimwambia “chini” akawa anaushusha mwili wake chini na baadaye akamwambia “inatosha MZALENDO umeshaiva ngoja tulione na hili LINANGA LA DEMO”.

Fred alirudi na kuniacha na KOPLO huyo wa jeshi akaniambia “Haya wewe NANGA mwenye MAPUUZA ni zamu yako sasa KUNJA NGUMI” awamu hii nilizikinga na kuziweka kwenye mgongo wa ardhi.

Nikapigwa juu chini za kutosha mpaka mikono ikaisha nguvu ikafika kipindi akiniambia juu siwezi kuamka na mwishowe nikajikuta nimelala.

Nilimsikia koplo akisema “Amka wewe nisije nikakuua wakaja kunipigia kelele wazazi wako” niliamka na kukaa kitako nikasikia vicheko kutoka kwa WAZALENDO na hata afande Jose naye alikuwa akicheka.

“Vipi baba” nikamjibu kwa sauti ya unyonge “Duuh utaniua baba” basi vicheko ndo vikazidi kushamiri mahala hapo.

Afande aliendelea kusema,
“Ntakua kweli sijaja jeshini kuuza sura yaani upo kikosini wiki nzima hujui maana ya DABO nakwambia ukunje ngumi nako hujui sasa unajua nini KUBASTI au KIJOGOO rudi zako kakae huko”.

Nikiwa narudi zangu nikamsikia akiniuliza “kwanza una chandarua we NANGA” nikamjibu “Hapana afande” akaniambia “Kesho uje kuchukua dukani hela ushalipiwa”.

Kwa mbali nikaanza kuyakumbuka maneno ya afande Shamte aliyenionya kuwa kutokana na kulifahamu jina langu afande huyo atanisumbua sana na kweli nimeanza kuamini maana sikuona sababu ya msingi ya kunifanyia yote hayo.

Inasemekana afande huyo ni mtu wa kumaindi vitu vidogovidogo na mwenye jazba ilikuwa ni vigumu kuyaepuka hayo maana niligundua kuwa ni mtu mwenye kigugumizi watu ambao hasira zao zinakuwa ni za karibu sana.

Nikiwa najitafuta ni wapi nilikaa mara ya mwisho ghafla nikajikuta kuna mtu amenishika mkono akisema “K njoo ukae hapa”.

Jina hilo pekee lilinifanya nigundue ni nani aliyekuwa akiniita maana ni yeye tu aliyezoea kuniita hivyo mbali na wale niliowaacha nyumbani.

Ndiyo sijakosea kama ilivyo kwako alikuwa ni Linda pisi ya Kichaga kutokea chuga alinivuta nami sikuwa na hiyana nikajisogeza na kukaa karibu yake.

Tulipiga stori mbili tatu pamoja na kuhojiwa ni kwa nini sipatikani kwenye simu wakati nilijua kuwa yupo safarini ilihali anawaona wengineo hapo wako na simu zao ina maana hazikatazwi.

Nilimpanga kuwa simu yangu inakaribia kuisha chaji na kule MAHANGANI tunakolala hakuna sehemu ya kuchajia hivyo nimeizima ili tuwasiliane baadaye muda wa kulala kama ilivyokuwa jana yake akaridhika na majibu hayo.

Tukiwa katika soga hizo tayari Matroni alikwishaondoka na hata Koplo naye hakuwepo hivyo tulikuwa kwenye uangalizi wa SERVICE MEN Rashidi na Devi.

Afande Devi yeye akawa anatuhimiza na kutupa tafsiri ya rejesta zitumikazo jeshini, kumbe DABO maana yake ni njoo na KUKUNJA NGUMI maana yake ni kupiga pushapu.

Tuliendelea hivyo mpaka pale yalipofika majira ya saa nne tukapata ugeni wa afande Moses akiwa ameongozana na Sajenti Pastima.

Walikuwa ni maafande wa zamu na kama kumbukumbu zitakuwepo afande Moses yeye ndiye aliyetupatia UTAWALA asubuhi akidai kuwa ni kwa sababu ya ujio wa Ustadhati Rehema.

Afande Pastima naye haikuwa mara ya kwanza kumuona alikuwepo ile siku nilipojichanganya kundi la MADAWILI kuhesabu nao namba.

Afande Pastima alimhimiza Ustadhati kesho yake avae kama wengine na akubaliane na mazingira maana hatofanya hivyo milele muda utaisha na ataendelea na utaratibu wake.

Baada ya Afande Pastima na Moses kujiridhisha na idadi iliyopo walituruhusu na kwenda zetu MAHANGANI.

Nikiwa kitandani niliongea na Linda aliyeniuliza ni muda upi ningependa anipatie zawadi zangu nikamwambia kama zitakuwa chache zikatosha kwenye mifuko basi anipatie asubuhi muda wa MABIO vinginevyo anilatee jioni baada ya kula tukiwa KOMBANIA.

Nilimtahadharisha simu inakaribia kuzima chaji akaniambia nimuazime mwingine pale ya kwangu itakapoisha chaji nilimuitikia ila sikufanya hivyo kwanza nilishukuru mno kuimaliza siku ndefu kama hiyo.

“Kama unataka kulala ungebaki kwenu hakuna aliyekulazimisha kuja huku”
“We lala tu siumekuja kulala huku”
“Hilo unalokumbatia siyo shuka ni sanda kama unabisha angalia kama hujalala kwenye jeneza”.

Nilishtuka nikajikuta naamka kwa kukurupuka ila baadaye nikagundua kuwa walikuwa ni maafande waliokuja kutuamsha kuianza ratiba ya siku nyingine tulikuwa tukiwaita wazee wa mauzauza maana hawajawahi kuwa romantic wakituamsha.

Tulienda zetu KOMBANIA ambako tulihesabu namba tukapanga mistari yetu mitatu MABIO yakaanza.

Masare akalianzisha tukaondoka zetu ila uelekeo ulikiwa sehemu tofauti na ile ya siku zote na mambo yakawa hivi,

“Masare: Ewiii
Sisi: Ewaaa
Masare: Ewii
Sisi: Ewaaa
Masare: Elewii
Sisi: Elewaa
Masare: Yalayalayala mama
Sisi: Yala kidole changu
Masare: Yalayalayalaa
Sisi: Mama kidole changu
Masare: Haya kidole changu
Sisi: Kinauma
Masarei: Mama kidole changu
Sisi: Kinauma
Masare: Kidole changu
Sisi:Kinauma.” ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

**************Itaendelea…………….........…….....
 
EPISODE 18

Tulifikia kwenye uwanja wa mpira wa miguu uliokuwa karibu na nyumba za raia kifupi na sisi tulikuwa uraiani ambako japo hatukuona raia hata mmoja maana walikuwa wamelala labda waamke kutokana na makelele yetu.

Tulishangaa kwa muda na baadaye tukahesabu namba na kurudi zetu kikosini nderemo na vifijo havikukosekana kwenye BOGI la mchizi Masare alikinukisha kama kawaida.

“Masare: Zaina Zaina
Sisi: Zaina
Masare: Zaina mwana mama
Sisi: Zaina
Masare: Toto la kitanga
Sisi: Zaina lete raha Zaina
Masare: Ukimuona Zaina
Sisi: Zaina
Masare: Mwambie nampenda
Sisi: Zaina
Masare: Ananikosesha raha
Sisi: Zaina
Masare: Usingizi sipati
Sisi: Zaina lete raha Zaina
Masare: Alee dada Zaina
Sisi: Anainama
Masare: Huyoo
Sisi: Anainuka
Masare: Huyoo
Sisi: Anaona haya huyoo”.

Tulifika HANGANI na vibe la dada Zaina tukaendelea na ratiba nyingine na baadaye tukaelekea zetu KOMBANIA ambako siku hiyo ilionekana barabara zote ziko sawa hivyo hatukwenda kwenye vifusi.

Tulienda kwenye majukumu tofauti tofauti ambapo binafsi nilipangwa kwenda kuchimba shimo la taka lililokuwa karibu na sehemu iliyokuwa ikiuzwa vyakula ambayo kwa lugha ya kwao wanakuita KIWANI.

Hapa KIWANI ni tofauti na MESI kule kwa MZABUNI na tofauti ni kuwa MZABUNI anakuwepo kwa ajili ya kulisha kikosi kwa ratiba maalum na na mwisho wa siku hulipwa kulingana na mkataba wake kifupi anakuwa na bajeti yake kutoka kwenye bajeti ya kikosi.

Tukiwa mtaani naweza kusema KIWANI ni kama kwa mama lishe ambaye yeye unampa hela ndiyo akupatie huduma yaani hana bajeti maalum wala muda maalum wa kutoa huduma.

Pale tulipokuwa tunachimba shimo alikuwepo afande mmoja mmoja miongoni mwa wale waliokuwa wakitusimamia tulikuwa tukifahamiana, alikuwa ni afande Fadhili niliyesoma naye mpaka darasa la saba.

Kusema ukweli sikutegemea kukutana na mtu wa nyumbani kikosini hivyo nilipomuona ikanijia hisia kuwa niko nyumbani hali iliyopelekea kuongezeka kwa imani na amani kuwepo kikosini hapo maana angalau ninaye mtu wa kumkimbilia na kumlilia shida.

Tulipiga stori mbili tatu za nyumbani na hivyo ikawa ahueni kwangu kwenye kazi maana msimamizi nilijitenga naye pembeni tukupiga vigano.

Kazi hiyo iliendelea mpaka ulipofika muda wa chai tukatawanyika kwenda kunywa chai kabla ya kutawanyika afande John aliyekuwa akisaidiana na afande Fadhili akatuambia baadaye tutarudi kuendelea na kazi yetu ila atatupitia KOMBANIA hivyo akija akasema WALE WATU basi tumfuate.

Tulienda kunywa chai nikiwa kwenye foleni na Linda aliyekuwa akiniambia kuwa alinitafuta asubuhi anipe zawadi zangu ila hakuniona.

Nilimpanga anipatie mizigo hiyo usiku tukiwa KOMBANIA wala asijali alilalamika pia kuwa ana usingizi alafu amechoka sana kwa kazi alizofanya mpaka muda huo.

Nilimwambia “Kazana rafiki yangu si nilikwambia kabla hujaja ukasema utaweza haya sasa umejionea mwenyewe hujamaliza hata nusu ya siku umechoka ulifikiri unakuja kusolve log huku”.

Linda alishikwa na butwaa na kuniambia “duuh kweli umenichoka mineno yote hiyo ya kwangu” alikuwa akitia huruma usoni ila hakuna namna alitakiwa apambane tu.

Linda alizungumzia kilichotokea jana baada ya simu kuzima chaji ndipo nikapata wazo kuwa niende na simu kwa afande Fadhili akanibustie.

Kama alivyotupanga afande John alikuja KOMBANIA akaropoka tu wale watu tukatoka na kuungana naye Linda naye aliungana nasi maana nilimpanga kuwa kule hakuna kazi ngumu kama alikokwenda asubuhi.

Afande John alishtuka ikambidi atuhesabu ila Linda alijikausha kama siyo yeye hata hivyo haikuwa kesi kubwa maana kulikuwa na ongezeko la watu ambao walimaliza kazi zao asubuhi kabla hata ya muda wa chai.

Tukiwa kwenye FATIKI nilimpatia simu afande Fadhili ila aliniambia kuwa wanakochajisha huwa wanachajisha kwa jero nilijuwa ananipanga tu ila ilibidi nikubaliane naye.

Afande John alikuwa akituhimiza kutofanya kazi kwa uharaka sana ili tusimalize mapema turudi tena baadaye hii ilikuwa ni kama mbinu ya kutegea maana hata wao wenyewe wapo kwenye majukumu hivyo shimo likiisha wanaweza wakapelekwa kwenye kazi nyingine ngumu ama ya mbali hivyo ni kama walikuwa wanategea.

Tulimaliza na kwenda kula na baadaye tukarudi KOMBANIA awamu hii shimo lilikuwa bado halijaisha ila wengine tulipunguzwa haswa sisi tuliokuwepo tangu asubuhi.

Tulichukuliwa watu kadhaa tukaenda bustanini na afande Elisha ambaye alitupanga mistari mitatu iliyonyooka na kuanzisha wimbo.

“Afande Elisha: Ewiii
Sisi: EwaahAfande
Elisha: Ewiii
Sisi: Ewaah
Afande Elisha: Ewiiiiih
Sisi: Ewaaaah

Afande Elisha: Siuliutaka mwenyewe mchezo wa bolingoo tuliza boli mwanangu mpira umejaa

Sisi: Siuliutaka mwenyewe mchezo wa bolingoo tuliza boli mwanangu mpira umejaa

Afande Elisha: Haya Selina oooh Selina
Sisi: Haya twende
Afande Elisha: Haya Selina eeeh Selina Sisi: Haya twende
Afande Elisha: Hawee tunaondonda
Sisi: Haya twende
Afande Elisha: Ayaa tunaondoka
Sisi: Haya twende”.

Tulifika bustanini na kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kumwagilia, kuandaa vitalu na kuweka mbolea tafadhali sana hatukuchuma mboga usije ukawaza kuwa tulichumishwa tembele😉.

Wakati huu tulikutana na afande muungwana ambaye alikuwa akihahamasisha kufanya kazi bila kukwazana jamii ya watu hawa ukiwakuta ofisini ni wale wanaofanya kazi kwa sababu wanaipenda na sio wale wanaofanya ili wapate mshahara.

Tulifanya kazi huku akitupigisha stori za hapa na pale katika moja ya stori zake alituambia kuwa kazi ya bustani alikuwa akiifanya tangu akiwa mtoto nyumbani kwao.

Hii iliakisi nilichokisema kuwa ni kazi anayofanya kwasababu anaipenda maana si rahisi kufanya kazi tangu ukiwa mdogo halafu usiipende.

Mara nyingi kazi ama vipaji tunavyoonesha tukiwa wadogo zile ndiyo kazi zetu sema hapa kati kuna upepo unatupitia tunajikuta tunaangukia kwenye udalali na kupiga debe siwakejeli ila nina uhakika kama tunazifanya ni kwa lengola mkono uingie kinywani tu ingawaje ndizo zinazotuweka mjini.

Afande alituambia mambo mengi yaliyokuwa yakitushangaza tusiamini kama kweli yanaweza kutokea kipindi cha kozi haswa kipindi kile cha wiki sita.

Alisema kuwa ni kipindi ambacho hakuna muda wa kulala na mnaweza kukesha na afande usiku kucha mkifanya mazoezi mpaka asuhi na ikifika asubuhi mnabadilishiwa afande mwingine mnashinda naye na ratiba inakuwa hivyo mpaka ziishe hizo wiki sita. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

****************Itaendelea…...……........……....
 
EPISODE 19

Alituambia kuwa inafika kipindi unachoka mpaka unakosa hamu ya tendo yaani mwanamke anaweza akawa mtupu na usifanye wala kumtamani ukamuona ni kama msela mwenzio.

Afande alitutahadharisha kuwa tujitahidi mno kipindi hicho hata mtu akidoji asiwe peke yake kwani unapodoji ukaenda kulala unaweza kulala kwa muda mrefu na ukiamka unajikuta una njaa ya kwenda.

Alitusimulia kuwa kipindi wao wako kozi kuna mwenzao alidoji peke yake walimtafuta wiki nzima bila mafanikio.

Siku moja walimkuta shambani akiwa amelala walipomuamsha hakuweza kufumbua mdomo, kuongea wala kutembea mana hata walipomsimamisha alikuwa akitetemeka na kuanguka kutokana na njaa kali aliyokuwa nao.

Tulimpinga sana afande kwenye swala la kuchoka mpaka kutotamani kufanya tendo pendwa mimi nilikuwa kinara wa hilo sikukubaliana naye.

Ilifika hatua tukawekeana viapo maana aliniambia kuwa kuna kipindi walidoji na MADAWILI kadhaa sasa kuna doja mmoja alikuwa anawachezea wale MADAWILI na hawajawahi kugundua mpaka kozi inaisha.

Nilimwambia kama huyo mwenzao aliweza kufanya hivyo basi siyo kweli na kama ni kweli basi itakuwa hao wengine wanashida ya nguvu za kiume, afande Elisha aliniahidi kunitafuta wakati huo utakapofika.

Tulipomalizana na kipengele hicho tulirejea zetu kikosini na afande Elisha ndiye aliyekuwa akiliongoza bogi hilo.

“Afande Elisha: Ewii
Sisi: Ewaaah
Afande Elisha: Ewii
Sisi: Ewaaah
Afande Elisha: Ewii
Sisi: Ewaaah
Afande Elisha: Ee Shaa, Shangazi
Sisi: Usikate shanga
Afande Elisha: Zuu zungusha
Sisi: Zungusha nyonga
Afande Elisha: Aii mama nilikuwa sijui
Sisi: Nikipata demu mauno mpaka asubuhi”.

Tulifika salama MAHANGANI na kuyafanya tuliyostahili kuyafanya ila hali ya hewa kidogokidogo ikawa inaanza kubadilika.

Ukafika muda wa msosi tukaenda zetu kuwakilisha kwa MZABUNI na hatimaye tukaelekea KOMBANIA ambako nilikutana na mazagazaga yangu kutoka kwa mtoto Linda nikayapokea na kuyapeleka HANGANI.

Ilipofika mishale ya saa tatu iliporomoka mvua kama ya buku na mdogo wake ilibidi tutolewe sehemu ile iliyokuwa wazi na kupelekwa kwenye bwalo la chakula walilokuwa wakilitumia maafande wa JKT.

Tuliwakuta Service Man hao wa JKT wakiwa wanaangalia tamthilia za azamtv hivyo ni kama tulienda kuwaharibia kwani iliwabidi waamke kwenye viti nao wasimame na viti kuviweka sehemu moja kwa kuvibananisha ili kusudi ipatikane nafasi ya kutosha.

Usiku huu haukuwa usiku wa kuimba wala kusifu ila ule usemi wa “Burudani kwa wote” ndiyo uliokuwa ukitanua mbawa zake kwa usiku huo.

Ilifika saa nne muda muafaka wa tamthilia pendwa ya Sultan ambayo iliwafanya watu kutokujali kama kuna mvua ilikuwa ikinyesha walikuwa wakiongezeka.

Alikuwa akionekana mama wa himaya Bi Hulem Sultana akiwa na chawa wake aliyemjaza nyota za kutosha wakiwa kwenye mipango ya kumpelekea pumzi ya moto Waziri mkuu aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Pasha.

Kilikatika kipande cha kwanza kati ya vile vitatu kilipofika cha pili walikuja maafande wa zamu yaani afande Jamali aliyeongozana na afande Mpemba aliyekuwa na kifimbo chake mkononi kama cha afande Pastima.

Ilibidi runinga izimwe ili tuendelee na zoezi la lokoo lililochukua muda mrefu kutokana na kukosea kuhesabu maana tulikuwa hatusikilizani vizuri kutokana na makelele ya mvua na hata hivyo eneo lilikuwa ni dogo na tulikuwa wengi mno.

Hesabu zilipokaa sawa tuliruhusiwa na kwenda zetu MAHANGANI, asubuhi yake hakukuwa na mvua hivyo tuliendelea na ratiba nyingine.

Kipindi zinaendelea ratiba hizo nilipata kuuona umuhimu wa rainboot maana udongo wa sehemu ile haufai kabisa ulikuwa ukiteleza mno hata hivyo kulikuwa na nyakati nyingi za kukimbia hali iliyopelekea wengi wetu kwenda kuhiji Maka bila pasi na gharama yoyote ile.

Kwa kweli ardhi ya kikosi ilikuwa haitamaniki kabisa kuitazama maana kila sehemu ilikuwa imekanyagwakanyagwa utadhani watu walikuwa wakitengeneza udongo wa kufyatulia tofali za matope ama kujengea nyumba za ukuta wa udongo.

Ulipofika mchana mvua ikanyesha tena zaidi ya ile ya usiku hali iliyopelekea kupewa UTAWALA maana hakukuwa na kazi ingeweza kufanyika.

Tulifurahi na tukawa tunaomba iwe inanyesha mara kwa mara ili tusiwe tunafanya kazi kumbe tulikuwa tunajidanganya bila kujua wenyewe wana wimbo wao usemao “Haiwezekani kamanda maji kupanda mlima".

Kauli hiyo ilikuwa ikimaanisha kuwa kisichowezekana jeshini ni maji kupandisha kwenye mlima pekee na kama unakumbuka aliwahi kutuambia Afande Rashidi kuwa jeshini ni sehemu pekee ambayo kipara kinanyolewa hawa mabwana si ajabu wakatuaminisha kuwa inawezekana kabisa kuideki bahari😅.

Mvua hiyo iliyokuwa ikinyesha kwa heshima ilikuwa ikipungua na kukata kabisa ila ilikuwa tukifika KOMBANIA tu mawingu yalikuwa yakigongana na kumwaga cheche hivyo watu wakawa wanawapongeza babu zao kwa kazi wanayofanya.

Ustadhati Rehema alionekana kupata tabu na hali hiyo maana nguo zake zilikuwa zikikusanya tope la kutosha mbaya zaidi kuna kipindi tukiwa kwenye bwalo tulitakiwa kukaa chini hali iliyopelekea kukalia matope yaliyotokana na kukanyaga kwa viatu vyetu.

Asubuhi ya siku iliyofuata kulikucha shwari tukakimbia MABIO na kufanya usafi na kwenda zetu KOMBANIA tukaelekea zetu kwenye FATIKI ila tuliporudi tulijazana dukani kwa ajili ya kununua rainboot.

Siku hii hatukumkuta yule afande mnoko Koplo Jose ila tuliwakuta vijana wao wa JKT.

Wapo waliopata ila sisi wengine hatukufanikiwa maana ziliisha hivyo walichukua hela zetu na kutuambia tufuate baadaye mana waliendaa kufungasha kwa kawaida ilikuwa ni vigumu mno kuondoka dukani hapo bila ya kuacha hela.

Yaani ilikuwa ukienda ukakosa unachohitaji utawaachia hela tu labda uende ukaulizie kitu ambacho hawafungashagi ama kitu cha bei ndogo kama vile pipi ama biskuti hapo utanusurika ila si kwa bidhaa za msimu kama hizo.

Usiku ulipofika tukiwa KOMBANIA kuna dada mmoja alinifuata akiniomba nimsaidie kutoroka kikosini hapo maana alikuwa ameshapachoka.

Alikuwa ni Winifrida ambaye kama unakumbuka ile siku nawasili kikosini tukiwa maingate tunaandikisha PARTICULARS aliletwa dada mmoja na gari akisindikizwa na familia yake.

Kwanza nilimshangaa kwanini kanishirikisha jambo hilo lakini pia nilimuuliza ningewezaje wakati sikuwahi kufanya hivyo lakini niliogopa tusipofanikiwa huenda yakanikuta makubwa.

Aliniambia kuwa kwa anavyoniona ana uhakika kazi hiyo naiweza ila hata kama siwezi basi nimsaidie hata kwa mawazo.

Kwa kweli lilikuwa jambo gumu kwangu hivyo nilijaribu kumshauri asitishe na nilivyoona anang’ang’ania ilibidi nimwambie amtafute mtu mwingine. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

**************Itaendelea……….…………...

Alfagems
Kacheda mjasiliamali
Kujeni huku kimekwishapakuliwa
 
Back
Top Bottom