Kacheda mjasiliamali
Senior Member
- Apr 12, 2017
- 184
- 149
Aisee naweka nukta hapa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchawi muda rafiki yangu tunakimbizana na majukumu hata huu ninaoubahatisha najitahidi sana kuutumia kuandika siyo jambo ila maandalizi ya kuandika ndiyo yananifanya nichelewe kuandikaUnachelewesha sana Story we kijana 😜 ila haya mambo yangenipata kule Songea kama ningeenda 🤭
Uliogopa kwenda 😛Unachelewesha sana Story we kijana 😜 ila haya mambo yangenipata kule Songea kama ningeenda 🤭
Usijali. Huenda tungekutana mimi nilipangiwa Bulombora.😊Mchawi muda rafiki yangu tunakimbizana na majukumu hata huu ninaoubahatisha najitahidi sana kuutumia kuandika siyo jambo ila maandalizi ya kuandika ndiyo yananifanya nichelewe kuandika
Mimi wangenimaliza 😅Uliogopa kwenda 😛
Mnnnh ulipangiwa bhulombora au Songea unatuchanganya ujue mamyUsijali. Huenda tungekutana mimi nilipangiwa Bulombora.😊
Unachelewesha sana Story we kijana 😜 ila haya mambo yangenipata kule Songea kama ningeenda 🤭
MAISHA YA DEPO
SEASON-2
EPISODE 25
Basi ulifika muda wa MABIO tukaenda eneo mahsusi nikiwa na Shukrani kwaajili ya mission yetu ila cha kushangaza binti hatukumuona na kwenye simu hatukumpata.
Shukrani alimaindi na akasema kuwa ndivyo inavyokuwa ukifanya mission za hatari na wanawake na ndiyo maana tangu yuko shule hajawahi kutoroka na wanawake zaidi ya masela.
Nilimtuliza na kumwambia inabidi tujue kwanza kilichomkuta kabla ya kumlaumu hivyo angetulia kukuche tutapata majibu ilimradi hatujashtukiwa hakuna sababu ya kujiogopesha.
Shukrani alikuwa akiwaza sana maana kuna bodaboda tulimpanga amchukue binti huyo kwa lengo la kumfikisha mjini mapema kabla hata maafande hawajaanza kusafiri.
Amini usiamini hili dili tulilisuka haswa tulichukua kila tahadhari iliyostahili.
Bodaboda akawa anatupigia kupitia simu ya Shukrani ambaye aliogopa kuipokea, niliichukua na kuongea naye nilimdanganya kuwa binti alishtukiwa kipindi anatoka hivyo mchongo umebuma.
Nilimtoa hofu kuwa asijali hata kama akitutaja sisi yeye hatutomtaja kabisa hivyo aendelee kula mtori kwa mbege.
Mshikaji alielewa ingawaje alisikitika kupoteza dili la shilingi kumi na tano za kibongo ambazo alisema
“Daah wanangu mmenikosesha hesabu ya bosi ya siku mbili, leo nilikuwa nalala zangu saa tano asubuhi”.
Kulipambazuka vizuri na tukaelekea zetu KOMBANIA ambako nilimtafuta binti wa wakili na sikumuona.
Afande Jala alikuja kuchukua lokoo akiwa na afande Mbega ambaye alituambia kitendo cha kupangwa KIKOMBANIA ni ishara mbaya mno hivyo tujiandae kwa ajili ya siku inayoitwa “Introduction to the camp”.
Neno hilo lilinikumbusha nikiwa mdogo kwenye banda la video nilipokuwa nikitizama muvi za kivietinam zilizotafsiriwa na nguli mwamba kabisa Lufufu Mkandara.
Kwenye lokoo aliyochukua afande Jala alichukua list ya walinzi wa HANGA na wagonjwa ambapo taarifa za Wini ziliangukia upande wa wagonjwa kumbe bwana dada wa watu alishikwa sana usiku.
Usiku tuliporuhusiwa nilimpandia hewani Matron Anna ambaye aliniambia tukutane sehemu nami nikaenda matroni alinipa sweta lake na kanga ambayo sikuivaa alisema nijifunike mabegani chini nikabaki na suruali yangu ya track.
Kwa upande wa matron alikuwa na tisheti yake maarufu kama GREEN VEST basi tukatiririka zetu mpaka yalipo MAHANGANI kwao ambayo hayakuwa mbali na UWANJA WA DAMU.
Tulifika MAHANGANI na hatimaye chumbani kwake ambako niligundua kuwa MAHANGA yao yalikuwa tofauti kabisa na ya kwetu maana ya kwao yalikuwa hadi na vyumba.
MAHANGA ya kiume tuliyokuwa tukiitwa NGORONGORO yalikuwa ni bwalo lisilo na chumba na hata hivyo kuta zake zilikuwa zimejengwa kwa mabati.
Matroni alinisisitiza kutokujiachia wala kutotoa sauti kubwa kwenye chumba hichoambacho kilikuwa na deka iliyomaanisha kuwa wanakaa wawili ila mwenzie hatukumkuta.
Tulipiga stori kwa muda kisha akaniambia tuondoke kabla mwenzake hajarudi nilizuga sijamsikia nikamkumbusha kuhusu Katerero aliniambia atanionesha siku nyingine (elewa neno atanionesha siyo ataniambia siku nyingine😜) kwani siku hiyo hakujipanga.
Neno hajajipanga lilinipa ujasiri wa kumuuliza hajajipangaje wakati siku zote topic ilikuwa ni hiyohiyo akasema kuwa siku hiyo amefanya hivyo ili aone kama nina ujasiri wa kufika huko kwahiyo nimpe muda ataniita siku nyingine.
Siku iliyofuata tukiwa KOMBANIA tulikuwa na Wini msichana pekee kwenye picha letu la mission impossible alisema kwamba usiku ule lilimshika tumbo la period hivyo ilikuwa ni vigumu kuondoka katika hali ile.
Aliendelea kusema kuwa ilimbidi azime simu kwani kulikuwa na watu waliokuwa wakimuangalia hivyo aliogopa huenda wangemsaidia kupokea ukawa msala nilimpongeza mno kwa kujiongeza kwake.
Wini alini surprise kwa kuniambia kuwa ule mpango wa kutoroka nao ameufuta ameufungua moyo na yuko tayari kubaki kipindi chote cha mafunzo.
Kusema kweli alinifanya nimshangae nisijue kapatwa na kipi maana kuumwa tumbo pekee haiwezi kuwa sababu ya kupindua maamuzi kwa haraka hivi.
Aliponiona kwenye hali hiyo aliniambia “Worry out K najua unawaza kuhusu simu ila usijali nitakupa hela ukatafute nyingine mtaani I am so sory dear”.
Nilimjibu “Hapana Wini sikufanya hivyo kwa ajili ya malipo (nadanganya nilikuwa nalitaka tambo sana tu ☺)”.
Nikaendelea kusema “Nimefanya hivyo kutokana na kisa chako ujue hata mimi baba alinilazimisha sikupenda kabisa kuja huku na ile siku unaniambia ni kama ulikuwa unapakaza chumvi kwenye kidonda hivyo nikaona nikusaidie ili siku nyingine usije nitonesha kidonda change kinachokaribia kupona”.
Kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndivyo ndivyo mambo yalivyokuwa yanazidi kuwa magumu hali hii ilipelekea baadhi ya watu waliokosa uvumilivu kutoroka.
Ukaribu baina yangu na Wini ukawa unaota mizizi hali iliyomfanya kujisikia amani maana sikuwahi kumsikia tena akiropoka neno kutoroka hata tulipokuwa tukipewa kazi ngumu ingawaje alikuwa akisafiria sana upepo wa cheo changu.
Siku moja tulikuwa na FATIKI ya kuvuna mahindi ya shamba la kikosi ambalo lilikuwa liko umbali wa kilomita zaidi ya nane kutoka makao makuu ya kikosi.
Kwenye shamba hilo ilikuwepo na kambi ndogo ambayo nafikiri ilikuwepo kwa ajili ya kusimamia usalama wa mazao na mashamba kwa ujumla kwani wahuni siyo watu.
Tukiwa katika kipindi cha mavuno ya zao hilo mama la taifa tulikuwa tukiamka muda wa MABIO na moja kwa moja tunazikata kilomita tukiwa na ndoo zetu mpaka shambani.
Kule shambani mara nyingi tulikuwa tukienda na mzee mmoja aliyekuwa maarufu sana kwa jina la Halichachi wakimfananisha na kilichokuwa kifurushi cha mtandao wa tigo.
Sifa ya mzee huyo ambaye cheo chake alikuwa ni msimamizi wa maswala ya nidhamu kikosini alikuwa halazi kazi yaani ni mpaka iishe ndiyo aidha mpumzike ama mle.
Kitu kibaya zaidi chakula kilikuwa kikitolewa kikosini tu waliokuwa wakila hapo ni wale waliokuwa wakikaa kwenye kambi hiyo sisi wengine ilitulazimu kutembee tena hizo kilomita mpaka kikosini.
Kuna baadhi ya siku tulikuwa tukiinywa chai mishale ye saa saba yaani tunamaliza kazi saa tano alafu tunatakiwa kutembea mwendo wa masaa mawili tukisubiriana tufike wote ndiyo chai itolewe.
Katika kitu cha kuhatarisha ni kuwa tulikuwa tukirudi na kiu kikali na moja kwa moja tulifikia kwenye matenki yaliyopo karibu na jiko na kufakamia mimaji kabla ya kunywa ingawaje maafande walikuwa wakitushauri kuwa tunywe kwanza chai lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
*************Itaendelea…………............................
😅😅😅Mnnnh ulipangiwa bhulombora au Songea unatuchanganya ujue mamy
Au kipindi unapangiwa Bhulombola ilikuwepo Songea😌

*************Itaendelea………….......…….........
Kwa jinsi unavosimulia kupitia location mbalimbali hii ,inaonesha moja kwa moja ni 838KJMAISHA YA DEPO
SEASON-2
EPISODE 26
Hali hiyo ilikuwa ikiwashinda watoto wengi wa kishua na siku moja Wini alinipa dili la swahiba yake mmoja waliosoma wote kuwa anataka kutoroka nilivyompelekea dili hilo Shukrani aligoma kulifanya.
Kiukweli nilikuwa na ukata hivyo nikaichukulia kama fursa nililipiga dili hilo nikitumia nondo zilezile za dili lililopita nikalitoboa na kujivutia tembo wawili.
Kifupi hiyo ndiyo ikawa kazi yangu ambayo haikunitupa kwenye maokoto na baada ya kufanikisha dili hilo Shukrani alianza kunielewa na tukawa tunapiga wote na malipo yakawa ni pasu kwa pasu kwa madili yaliyokuwa yanapitia kwangu.
Sifahamu kwa upande wa Shukrani maana kazi alizokuwa akizileta yeye zilikuwa ni za hela ndogo nilikuwa nikihisi ananipiga ila ulikuwa ni kama msimu wa maembe ambao ulikuwa ni adimu kumkuta inzi ama ngedere aliyekonda.
Hela hizo zilikuwa zikinipiga tafu kwenye shida ndogondogo na nilikuwa sikatiki KIWANI kulikokuwa kukiuzwa mihogo, maandazi na vitafunwa vingine.
WAZALENDO wengi tulikuwa tukijazana huko maana ule muda tuliokuwa tukisimuliwa ulikuwa umefika kwani tulikuwa hatushibi chakula cha MZABUNI kutokana na kazi tulizokuwa tukizifanya si kwamba walipunguza kipimo hapana ila ni matumbo yalikwishatanuka na kibaya zaidi hakukuwa na nyongeza.
Kipindi hiki ndicho kilichoikuza misamiati kama vile KUBASTI yaani kula zaidi ya mara moja ila kwa kujificha maana haikuruhusiwa kwani ukila zaidi ya mara moja ina maana wengine watakosa kwa maana hiyo ule msemo wa SIFA WEPESI haukucheza mbali wakati wa KUBASTI.
Msamiati mwingine ulikuwa ni KIJOGOO ambao unamaanisha kiporo ama chakula kinachohifadhiwa usiku kwa ajili ya kuliwa alfajiri kabla ya kwenda kwenye FATIKI ili upate nishati ya kuisogeza siku nyingine.
Ikumbukwe KIJOGOO ambacho nimekipiga sana si chakula kinachotolewa na MZABUNI ila ni wewe mwenyewe unakitunza aidha baada ya KUBASTI, kubakiza ama kununua KIWANI.
Siku zilizidi kukimbia huku idadi ya watu ikiongezeka hali iliyopelekea kuundwa KOMBANIA ya tano na pia majina ya KOMBANIA yalibadilika kutoka majina ya wanyama hatimaye zikawa herufi.
KOMBANIA ya chui chini ya ST Fred wao waliitwa ALPHA COY (A-Coy), nyingine ni ile ya ST Ustadhati Rehema yaani tembo ikaitwa BRAVO COY (B-Coy), simba ya akina Linda iliitwa CHARLIE COY (C-Coy) na ile ya kwetu ikaitwa DANGER COY (D-Coy).
KOMBANIA iliyoongezeka ilifahamika kwa jina la EAGLE COY (E-Coy) na katika kipindi hiki tukatakiwa tuanze kuvaa vipensi vifahamikavyo kama PICKSHORT na kukatishwa kuvaa suruali za track.
Katika moja ya watu walioathirika na mabadiliko haya alikuwa ni Ustadhati Rehema ambaye aliwagomea kabisa kuvaa nguo hizo.
MADAWILI wengine walikuwa wakiona aibu kuvaa nguo hizo ila iliwabidi wavae maana kila pale walipokuja KOMBANIA walikutana na adhabu.
Rehema yeye adhabu hizo zilionekana kutofua dafu ingawaje wakati mwingine alikuwa akitetewa na maafande.
Haijawahi kuisha nguvu misemo ya wahenga na pale waliposema “Hakuna marefu yasiyo nan cha” ndicho kilichokuwa kikitokea kwa Rehema ambaye alikuwa akibadilika kidogokidogo maana kuna baadhi ya siku alikuwa akifoleni KOMBANIA bila ya kufunika kichwa.
Kutokana na mabadiliko hayo ya siku baada ya siku SERVICEMEN waliokuwa wakitusimamia kwa kipindi hicho walikuwa wakituambia “Kunyweni maji mengi mioyo ielee maana kozi inakaribia kuanza”.
Hatukuwaelewa walikuwa wakimaanisha nini kwani tulikuwa tukiona kozi imeanza kitambo kilichokuwa kimebadilika ni mavazi pekee.
Ratiba ya shamba haswa kuvuna haikuwahi kukoma kwa siku chache kutokana na ukubwa wa shamba na hata hivyo tulikuwa tukivuna kwa nusu siku hatukuwahi kushindia huko.
Siku moja baada ya kutoka shamba tulipewa jukumu la kuhamisha vitu vyetu kwa ajili ya kuishi kwenye MAHANGA ya KIKOMBANIA.
Yaani awali kipindi tunafika walikuwa wakitupeleka kwenye HANGA lolote lile lililokuwa wazi kwa kipindi hicho kabla ya kutuhesabisha namba na kutugawa KIKOMBANIA hivyo ukawa ni wasaa wa kuishi kwenye MAHANGA ya KOMBANIA.
Hali hiyo ilikuwa ikileta wepesi kwenye usimamizi kama ST nina ushuhuda nalo lakini pia haikucheza mbali na kauli ya kihenga isemayo “Ndege wafananao huruka pamoja”.
Tulikuwa tukipata ugumu pale karani akitaka kujua majina ya walinzi wa HANGA na pale anapokosekana mmoja wetu aidha kwa kudoji ama kuumwa tulikuwa tukishindwa kujua HANGA alilopo kwa ajili ya kujiridhisha kama uongozi wa KOMBANIA😆.
Tukiwa katika zoezi hilo tukufu tulisikia filimbi zikipigwa za kutosha kutokea UWANJA WA DAMU ambako kwetu tulishangaa maana haukuwa muda wa chakula na tuliambiwa TUFOLENI huko baada ya chakula cha jioni yaani tulikuwa na KAUTAWALA fulani hivi ka chinichini.
Kitu cha kushangaza ni kuwa waliokuwa wakipiga filimbi hizo walikuwa ni BAKABAKA ambao walikuwa na Matroni Neema na tulipojipeleka sisi tuliambiwa turudi maana yajayo hayatuhusu.
Basi WALIFOLENI askari wa JKT wakiwa na sare zao za KARANGA full combat juu na chini na walifoleni wakiwa na ndoo kila mmoja.
Walianza kupitishwa lokoo na baada ya muda akasikia Matron Neema akisema “Sikia kutoka kwangu, kwa yeyote asiyekuwepo hapa na anastahili kuwepo basi mfikishieni taarifa mwambieni kuwa awe na maelezo ya kutosha kwanini hayupo mahala hapa”.
Aliendelea kusema “Tukianzia kwenye lokoo ya jana tuliwataarifu kuwa leo asubuhi mnatakiwa kwenda shamba kwa ajili ya kutoa mahindi yetu ila nimesikitishwa sana na kiburi mlichokionesha sijui kama mnaweza kunieleza ni sababu zipi ziliwafanya msiende au hamkunielewa”.
Kilitawala kimya cha sekunde kadhaa na baadaye akaendelea “Kimya maana yake hakuna majibu sasa bila kupotezeana muda ambaye anajijua hajaenda naomba ajisogeze pale mwenyewe haijalishi ana sababu au hana tutaelezana tukiwa pale”.
Zoezi hilo lilifanyika na mchujo mkali ukachukua nafasi ambao ulizalisha makundi mawili ya waliosafi na wasiosafi yaani madoja wa kazi.
Baada ya hapo ilisikika kwa mara nyingine sauti ya Matroni Neema “Jana kipindi tunawaambia mkawa mnatuona kama Mchinga Sound vile tuko stejini tunatumbuizasiyo, sawa sasa leo nasisi tutakuwa tunawatizama ninyi mkitumbuiza naomba makamanda wangu kazi ianze”.
Ebwana eeh ilitokea shoo siyo ya kitoto yalikuwa ni masaa matatu yenye ujazo wa DOSO la machozi, jasho na damu.
Wale jamaa walivurugwa siyo kawaida nashindwa hata nisimulie lipi alafu niache lipi ila tulishaanza kuelewa ni kwanini walituambia tunywe maji mengi mioyo ielee.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
************Itaendelea………………………………...
😄Muhimu kakaNgurutu unapenda sana utawala,episode moja tu?!!
🤨Am not sure! Discuss??Kwa jinsi
Kwa jinsi unavosimulia kupitia location mbalimbali hii ,inaonesha moja kwa moja ni 838KJ