mHAMAS-shaji
Member
- May 31, 2024
- 63
- 177
- Thread starter
- #41
MAISHA YA DEPOMAISHA YA DEPO
SEASON-2
EPISODE 07
Kimya hicho kilichodumu kwa muda mfupi kilivunjwa na maneno ya afande Mvamba ambaye alisema
“Anhaah kumbe mnapenda umbea lakini hamuutaki ukweli, ukweli unauma eeh!”
“Sasa ni hivi ile migomba mnayoiona pale tumeipanda baada ya kuwazika wenzenu ambao nao ni WAZALENDO wa mujibu wa sheria kama nyie wapo wa miaka ya nyuma na wengine ni wa mwaka jana tu hapo”.
“Kwahiyo mjiandae kama mmekuja 200 msijihakikishie mtarudi wote, lazima form six kama 180 hivi wafe alafu wahitimu kama 20 hivi”.
“Na katika hao wazima wanaweza wakawa wanne au watano mana katika mazoezi mtakayokutana nayo kama siyo kifo basi kuna wengine watakuwa vilema”.
"Utakuta huyu kavunjika mguu mwingine hana sikio mara anayefuata shingo imekaa upande mara ukute macho yote anayo ila hayaoni vizuri ama hayaoni kabisa au mwingine akili anazo ila anakuwa hana akili yaani kawehuka ili mradi tu tuwapunguze msimalize wote”.
“Alafu mjue bahati mbaya sana huku hatuna mitihani ya kuwapunguza idadi kama wanavyofanya necta, mitihani yetu huku ni mazoezi na kwenye mazoezi hakunaga chabo wadogo zangu si eti afande Kapanda”
“Ndiyo afande na kama wamefika form six kwa chabo aisee imekula kwao, huku ni bidii tu mazoezini ndo kutakufanya uvuke vikwazo ukiwa legelege mgomba wako utawekwa huku mwanzoni mwa shamba la migomba” alijiubu afande Kapanda.
“Na kitu kingine ambacho hamjui ni kuwa serikali imewaleta huku ili mfe, mbaki wachache ila nyie hamjui tu”.
“Unakuta lijitu linaandaa 50,000 ya nauli linafunga safari mpaka kambini ili lifuate kifo ukiangalia limesoma mpaka form six sasa elimu itakuwa imemsaidia nini”.
“Sasa za ndani ni kuwa baada ya serikali kuona mahitimu yamekuwa mengi mtaani halafu inatupiwa lawama hawayaajiri serikali yetu pendwa vile haitaki kulaumiwa ikaona iwalete jeshini”.
“Mnajua huku jeshini kinatokea kitu gani WAZALENDO?” aliuliza afande Mvamba tukabaki kimya asiwepo hata mmoja wa kumjibu wala kukohoa.
“Anhaah mnakaa kimya ili nisiwaambie ukweli, sasa ukweli ni kuwa huku mnakuja wengi ila mtakufa na kuhitimu wachache kwa maana nyingine wachache sana tena saaaana ndio watakaokwenda chuo”.
“Kule chuo mtapunguzwa kwa mitihani kama kawaida japokuwa watu wa chabo hamtakosekana haswa wale waliostuka wakaacha kuja ila watakuwa wachache mana wengi wao mtakuwa tushawapunguza hukuhuku kwenye shamba letu la migomba”.
“Nina uhakika miaka kumi baadaye wahitimu wasiokuwa na ajira mtaani watakuwa wachache ama hawatakuwepo kabisa na hapo serikali yetu tukufu itakuwa imefanikiwa kuzikwepa lawama nyingi kama ilivyo sasa” aliendelea kututisha afande Mvamba.
Tulibaki kimya kwa muda na hakuna aliyekuwa akinong’ona kwa wakati huo, woga ulituvaa miongoni mwetu kwa kile tulichokuwa tukiambiwa.
Baada ya kumaliza mazungumzo hayo afande Mvamba alituamuru tuhesabu namba.
Tulihesabu kwa usahihi na umakini wa hali ya juu tofauti na awali, afande Kapanda na afande Shadi walihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili kwani walituelekeza namna ya kuhesabu na wakasimamia pia zoezi lote mpaka mwisho.
Tulihesabu wote tukiwa tumekaa chini isipokuwa waliohesabu namba 10 wao walisimama na hakukuwa na namba kubwa zaidi ya 10 maana kila ilipofika 10 aliyefuata alianza upya yaani 1.
Tulishangaa namna ilivyokuwa rahisi kuhesabu na hatukujua ni kipi kilichofanya tushindwe hapo mwanzo ila nafikiri ilikuwa ni kitete tu kuwepo eneo lile, eneo ambalo kombati ya jeshi haikuwa tofauti na shamba dress tukiwa mabwenini.
Afande Mvamba aliwaamuru waliosimama wahesabu namba isipokuwa wa mwisho kabisa ambaye aliitika namba 8, walikuwa 23 ambao ni 230 na yule aliyehesabu 8 maana yake tuko 238 namba ambayo haikuwa tofauti na mwanzo.
MADAWILI waliitwa tena mbele wakahesabu namba kwa mara nyingine, walihesabu na walikuwa 47 na kipindi wanaenda bado kidogo na mimi niende ila kuna jamaa alinitonya kuwa mademu ndiyo wanaohitajika.
Akili yangu bado ilikuwa inaniambia kuwa MADAWILI ni wageni na wala sikujua kama tunatofautiana kimaumbo maana sehemu tuliyopo mwanga ulikuwa hafifu na wote tulivaa suruali ya truck na shati kitu ambacho kinafanya tuonekane tunafanana.
Kulibainika kuwepo kwa upungufu wa WAZALENDO watano kama ilivyo mwanzo ila wakati huu aligundua kuwa katika MADAWILI 49 waliosajiliwa wawili hawapo hivyo katika wale watano wasiokuwepo watatu ni wanaume.
Katika kujiuliza wako wapi wengine ndipo afande Shadi alipowaza na kusema huenda wasio kuwepo wakawa ni walinzi wa HANGA, wakateuliwa wanne kati yetu yaani wawili kutoka kila upande wakaangalie idadi ya walinzi waliopo huko.
Nilivuta kumbukumbu ni wapi nilisikia neno hilo nikakumbuka ni kipindi tupo kule ambako tuliacha vitu vyetu tukafuata magodoro afande Shamte aliwaita hivyo wale tuliowakuta nilikumbuka hawakuwa wengi maana wengine walipoulizwa kuwa ni walinzi wa HANGA walikataa.
Niligundua kuwa walinzi wa HANGA ni wale wanaoachwa kutazama usalama wa mali zilizopo mabwenini kwani jeshini bweni hufahamika kwa jina la HANGA.
Tukiwa tunawasubiri waliokwenda kuangalia idadi ya WALINZI WA HANGA masimulizi yaliendelea kama kawaida na kama ilivyo mwanzo afande Mvamba ndiye aliyekuwa msemaji mkuu.
Aliuliza kama kuna swali na ndipo afande Shadi akalirudisha swali la mwanzo lile linalohusu supu kwa atakayevujisha siri za jeshi uraiani.
Afande huyo mzee wa vitisho alisema
“Jeshi linaamini kuwa siri ama habari zinasambaa kwa haraka pale zinapowasilishwa na mwanamke tofauti na mwanamume, kwahiyo kwa sababu wewe kiumbe umetoa siri zetu huko chegani kwenye kusuka ama kwenye kijimeza chenu cha kasusu na sisi tunaamua kuchukua sehemu zako siri ili tuone je, siri iliyotoka ni yetu au ni yako”.
Waliporudi wale jamaa walioagizwa kwenda MAHANGANI walithibitisha uwepo wa walinzi wa HANGA watano kati yao wawili ni MADAWILI na waliobaki ni upande wa pili hivyo idadi ilikaa sawa.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
******Itaendelea……………………………………………...
SEASON-2
EPISODE 08
Baada ya kutimia afande Mvamba aliondoka na kutuacha na afande Kapanda pamoja na afande Shadi ambao walituimbisha mapambio ya jeshi kwa muda mpaka pale aliporudi kwa mara nyingingine.
Awamu hii alikuja na afande mmoja niliyesikia akimuita SAJENTI Pastima ambaye alikuwa na tumbo haswa sidhani kama ningekutana naye mtaani ningeamini kuwa na yeye ni mwanajeshi ama kweli usimdharau usiyemjua mana kwa mwili ule anafanana kabisa na meneja wa bar, cafeteria ama restaurant.
Afande Pastima naye alichukua lokoo na baada ya kujiridhisha kuwa tumetimia alimwambia afande Mvamba aturuhusu ambapo naye alituasa mambo machache kuhusu siku inayofuata na kukasimisha madaraka kwa afande Kapanda.
Afande Kapanda kabla ya kuturuhusu alituambia kuwa ratiba ni ileile watakuja kutuamsha usiku sana, TUTAFOLENI uwanja wa damu na kukimbia MABIO ikifuatiwa na usafi wa mazingira kabla ya kwenda kwenye FATIKI na ratiba nyingine hivyo tunatakiwa kulala macho.
Baada ya maneno hayo tuliruhusiwa kwenda kulala na wakati tunaelekea MAHANGANI kulikuwa na majadiliano mbalimbali haswa juu ya yale yaliyozungumzwa na afande Mvamba na mengineyo mengi.
Nilifika kitandani kwangu na kuweka mazingira sawa na nilipomaliza niliutwaa mwili wangu na kuutupa kitandani kwa ajili ya kuuchapa usingizi.
Mawazo yalikuwa ni mengi kabla sijapatwa na usingizi niliiwaza tangu safari ilipoanza nyumbani hadi kufika kambini pamoja na maswahibu niliyokumbana nayo.
Niliwaza sana kuhusu sehemu iliyoitwa UWANJA WA DAMU, akili ilitengeneza rundo la maswali kwa nini paitwe hivyo? Ama ndiyo sehemu yanapofanyika mazoezi magumu ya kijeshi na hatimaye damu humwagika na kupoteza uhai? maswali yalikuwa ni mengi pasi na majibu.
Sikuwahi kukutana na siku ndefu kuzidi hiyo hali iliyonifanya nitumie muda mrefu kuwaza na hatimaye kuupata usingizi licha ya ukweli kwamba nilichoka sana hivyo nilitegemea kuupata usingizi mapema ila ilikuwa tofauti.
Sikumbuki ni muda gani niliupata usingizi ila nilikuja kustuka majira ya saa 11 alfajiri na vipenga vilivyokuwa vikipulizwa MAHANGANI.
Walikuwa ni maafande waliokuwa wakitusisitiza kuamka haraka iwezekanavyo na kwenda KUFOLENI uwanja wa damu kwani tulikuwa nje ya muda.
Walikuwa pia wakiwakataza wale waliokuwa wakienda kupiga mswaki waliwaambia kuwa watapiga wakirudi kutoka MABIO kwani jambo muhimu kwa wakati huo lilikuwa ni kwenda UWANJA WA DAMU tu basi.
Nilikuwa na shauku kubwa ya kupajua uwanja wa damu hivyo basi ilinibidi nitii maagizo na kuacha kutandika kitanda ilinibidi niongozane na wenzangu kuelekea ilipo Allianz Arena.
Nilitoka nje nikawa naibia uelekeo wa wengi wao uliokuwa ni Kaskazini-Magharibi basi bila ajizi niliungana nao.
Kipindi tunaelekea huko nilikuwa nikiongea na jamaa mmoja ambaye alinifungua baadhi ya vitu na mazungumzo yetu yalikuwa hivi,
“Oya niaje”
“Fresh niambie”
“Poa, hivi huku ndiyo UWANJA WA DAMU”
“Ndiyo mzee si unaliona nyomi lote ndiko linakoelekea KUFOLENI hivyo”
“Anhaa sawa mwanangu mi mgeni nimeripoti jana usiku si unajua tena jeshini huku naogopa kuvamia kundi siyo langu kama yule mshikaji wa jana aliyekuwa anavamia kundi la MADAWILI muda wa lokoo”.
“Daah ila kweli yule mwana alizingua kwahiyo kama afande alikuwa anataka akawapige mashine na yeye angeenda” jamaa aliongea maneno hayo ya kejeli huku akicheka asijue kuwa mtu mwenyewe nilikuwa mimi ingawaje nilijikaza ila moyoni niliumia sikuwa na jinsi zaidi ya kuvunga.
“Ndo hivyo mwanangu na ndiyo maana nikaona nikuulize, hivi na wewe si ni MZALENDO”
“Ndiyo nimemaliza form six na mimi kama wewe”
“Anhaa umekuja jana au juzi”
“Mi nipo hapa tangu day one”
“Anhaah kumbe ushakuwa mzoefu”
“Hamna mwanangu wenyewe wanasema jeshi halizoeleki mambo yanabadilika kile sekunde”.
“Sawa ila siyo kama mimi, hivi MABIO ni kitu gani”
“Ni mbio za kawaida tu wala usiziogope”
“Hamna wala siogopi nataka kujua tu ili niwe na idea ya kile ninachokifanya”
“Sawa ni kama nilivyokwambia ni mbio za kawaida yaani hazina tofauti na mchakamchaka au jogging” alinijibu huku akianzisha mbio kuelekea waliko wenzetu.
Jamaa alinisisitiza tuwahi afande asije akatupa DOSO nilitaka kuendelea kumuuliza ila nikaona kama nitakuwa namkera hivyo nikaona ni muhimu nikafunga bakuli langu.
“Simameni hapo hapo nyie mnaojikuta mnaweza kulala sana” alisikika afande tuliyemkuta sehemu hiyo ambayo ilifahamika kama UWANJA WA DAMU.
Tulimtii na kufanya hivyo na zaidi ya hapo alitutaka tuchuchumae na kuruka kichura chura kuelekea walipo wenzetu waliofika kabla yetu.
Baada ya kusubiri kwa kitambo kidogo afande alituamuru tusimame na kuunda mistari mitatu iliyonyooka na baadaye akatuhesabisha namba.
Kulikuwa na mtiti kwenye kuhesabu namba yaani ni kama tumeanza nursery vile kila muda tulikuwa tukikosea, hesabu zilipokaa sawa tuligawanywa makundi yapatayo matatu.
Kundi la kwanza lililoongozwa na mmoja wetu ambaye nilifahamishwa kuwa alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuwasili kambini mapema siku ya kwanza na inasemekana ilikuwa ni asubuhi sana, kwa vile akili yangu haikupenda kujifikirisha sana niliwaza kuwa huenda kwao ni karibu na kambi hiyo.
Jamaa yule aliyefahamika kwa jina la Fred aliteuliwa kuwa kiongozi wetu yaani ST cheo ambacho kilinikumbusha utaratibu uliotumika kupata manahodha wa vilabu vingi vya kihispaniola na timu yao ya taifa.
Wao humteua yule aliyedumu na timu kwa muda mrefu kuliko wote pasi na kujali umri wala kiwango chake ingawaje mpaka inatokea mchezaji anadumu kwa muda wote huo inamaana kiwango kimo na umri unakuwa usogea pia. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
******Itaendelea……………………………………………...