Maisha ya Hamis Kichwa yanasikitisha sana baada ya kustaafu kazi ya Polisi

Maisha ya Hamis Kichwa yanasikitisha sana baada ya kustaafu kazi ya Polisi

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Angalizo:- Habari hii ni sanaa ya picha na haiendani na uhalisia wa maisha, Wala jina la mtu yoyote.

Hamis Kichwa, alikuwa maarufu sana hapo Oyster Bay Police akisifika kwamba ndiye Israel mahiri kwa majamba konki ambao inatakiwa tu watangulizwe.

Hamis Kichwa mtu wa Tanga, alikuwa anasifika sana kwa ndumba na mambo ya sayansi nyeusi, alimwekea Binti yake mkubwa tego, kijana yoyote atakauemla Binti huyo lazima afe kwa namna yoyote Ile. Na kweli ikawa hivyo, vijana wakawa wanamuogopa sana Binti.

Hamis Kichwa akastafu, akarudi kwao Tanga. Mkewe akaona isiwe shida, akakataa kwenda kuyaanza maisha ya Kijijini, akasema atakomaa hapahapa town hata kama atakaa nje ya mji.

Huko Tanga Hamis Kichwa maisha yamemchapa, ni kunywa mnazi kuanzia asubuhi hadi jioni huku akiwatishia wanakijiji wenzake kwamba atawachapa risasi.

Sasa Hamis Kichwa amekuwa ni mtu wa kupiga mizinga, usipompa hela atakutukana mwezi mzima kwenye simu.

Jamani tunapokuwa kwenye ufalme wetu, tuwe tunakumbuka na kesho.

Tusiache kutenda wema, cheo ni dhamana.
 
Back
Top Bottom