Maisha ya Kamari yamefanya Vijana wawe wavivu, wazembe ,wasofanya kazi Kwa Bidii

Maisha ya Kamari yamefanya Vijana wawe wavivu, wazembe ,wasofanya kazi Kwa Bidii

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Vijana wakubet na Kamari wenyewe Hawa Cha kujishughulisha Tena na kufanya kazi. Atashinda Ndani Masaa 24 ni kula, kubet Kamari.

Wenye Kazi nao, wamejikuta hawana Juhudi Tena ya kazi zao,kazi wanafanya tu ilimradi.

Serikali ya Ovyo nayo inajisifu, Et Kamari imetengeneza Ajira asilimia.

Taifa linazidi Kudidimia, Taifa linaenda kua na Kizazi ambacho Ubongo wake haunguki, kizazi Cha wasopenda kazi, wavivu wazembe, wenye kupenda Hela ila hawapendi kazi.

Yaani Taifa ambalo Baba ni Mbetishaji, Mama Mbetishaji, watoto Kamari.
 
Kipindi cha zamani, ajira zilikuwa ziko njenje, ilikuwa vigumu kumkuta kijana anabeti, nowadays ajira hamna, ila pia vijana hawajajiandaa na circumstances za kujiajiri kwasababu wengi hawajatoka kwenye familia ambazo ziliamini kwenye kujiajiri.

So wanakuwa hawana choice zaidi ya kubeti licha ya wengine kubeti ili waongeze vipato wakiamini mshahara haujitoshelezi na pia kutokuwa na experience na biashara na kuogopa kupoteza.
 
hii kitu bila serekali kuingilia kati tunaenda pabaya km taifa

wapige marufuku aya matangazo ya kubet yamekuwa mengi mno ndo yanahamasisha watu kubet
 
Watakuja kukutukana sio mda
😂😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌
 
Kipindi cha zamani, ajira zilikuwa ziko njenje, ilikuwa vigumu kumkuta kijana anabeti, nowadays ajira hamna, ila pia vijana hawajajiandaa na circumstances za kujiajiri kwasababu wengi hawajatoka kwenye familia ambazo ziliamini kwenye kujiajiri, so wanakuwa hawana choice zaidi ya kubeti licha ya wengine kubeti ili waongeze vipato wakiamini mshahara haujitoshelezi na pia kutokuwa na experience na biashara na kuogopa kupoteza.
Umeongea Point sana
 
Vijana wakubet na Kamari wenyewe Hawa Cha kujishughulisha Tena na kufanya kazi
Mkuu betting ni kazi ngumu sana inayotumia maarifa mengi ili kukuza mtaji, vijana wanashinda siku nzima wakifuatilia muenendo wa timu mbali mbali ili kufanya ubashiri sahihi, hawa vijana wanaweza kuajiriwa TMA na kufanya ubashiri wa hali ya hewa kwa ufanisi mkubwa.
 
Donda la kwanza ni kuamini ukiajiriwa ndo umeyapatia
MUNGU ATUSIMAMIE ZAIDI
 
Vijana wakubet na Kamari wenyewe Hawa Cha kujishughulisha Tena na kufanya kazi ... Atashinda Ndani Masaa 24 ni kula, kubet Kamari!!.

Wenye Kazi nao, wamejikuta hawana Juhudi Tena ya kazi zao,kazi wanafanya tu ilimradi !!!.

Serikali ya Ovyo nayo inajisifu, Et Kamari imetengeneza Ajira asilimia !!!!!!!!!!!!! .

Taifa linazidi Kudidimia, Taifa linaenda kua na Kizazi ambacho Ubongo wake haunguki, kizazi Cha wasopenda kazi, wavivu wazembe, wenye kupenda Hela ila hawapendi kazi.

Yaan Taifa ambalo Baba ni Mbetishaji, Mama Mbetishaji, watoto Kamari !!!!!....
Uzuri ni kuwa hamna aliyetajirika kupitia kubet hivyo wanatusaidia sana kutuachia wigo mpana zaidi wa kutajirika kupitia rasilimali tofauti za nchi.
 
Vijana wakubet na Kamari wenyewe Hawa Cha kujishughulisha Tena na kufanya kazi ... Atashinda Ndani Masaa 24 ni kula, kubet Kamari!!.

Wenye Kazi nao, wamejikuta hawana Juhudi Tena ya kazi zao,kazi wanafanya tu ilimradi !!!.

Serikali ya Ovyo nayo inajisifu, Et Kamari imetengeneza Ajira asilimia !!!!!!!!!!!!! .

Taifa linazidi Kudidimia, Taifa linaenda kua na Kizazi ambacho Ubongo wake haunguki, kizazi Cha wasopenda kazi, wavivu wazembe, wenye kupenda Hela ila hawapendi kazi.

Yaan Taifa ambalo Baba ni Mbetishaji, Mama Mbetishaji, watoto Kamari !!!!!....
Kama ni rahisi na wewe beti, upate
 
hii kitu bila serekali kuingilia kati tunaenda pabaya km taifa

wapige marufuku aya matangazo ya kubet yamekuwa mengi mno ndo yanahamasisha watu kubet
Kwani Kubet kuna shida gani?
 
Kubet kumefanya vijana kuhisi MAFANIKIO ni kitu cha ghafla kama chafya vile, kijana akiaangalia mkeka unasoma 5 million kama ukitiki sasa anaanzaje kutafuta kazi na kazi tayari yupo nayo.

Ila kwa namna nyingine vijana nao hawaitumii nafasi nzuri ya kubet kujiendeleza kwa kufanya deep analysis ya team wanazozibetia na stakes zake au odds zinazotolewa ili kujipatia kipato zaidi badala yake wanafata mkumbo au mahaba.

Kijana fanya sasa betting ndio ajira yako let say ndio Duka lako (online shop) then mtaji wako ni 5,000 ndio umechora Mkeka wako pale na umefanya feasibility analysis week nzima kuchambua zile team zako angalau 5 as a minimum. Then boom umepiga 1 million au hata 300K tumia 50k nyingine wekeza sehemu hata fungua kiduka uuze vocha au tigopesa cha kujishkiza.

TATIZO kijana akimfumua muhindi pesa yote anaifanyia ujinga anatumbua YOTE pombe na madem sasa hapo betting itamsaidia.
 
Back
Top Bottom