Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Yaani Kuna mambo lazima akili Yako ifanye kazi kwasababu unakuta huko unakoenda na unaambiwa Kuna utajiri, utawakuta watu wanauza machungwa na biashara ndogo ndogo . Bado hujiulizi kama utajiri hupatikana kwa kutumia nguvu tu je, Hawa wanashindwaje?
 
2007 ni kitambo sana, kipindi cha hapa kati, njia za kisasa za ku extract gold zilikuja, yale mabaki yaliyokuwa yanaachwa kipindi cha nyuma yalitajirisha sana watu, walikuwa wanayaacha wakidhan hayana dhahabu kumbe yana dhahabu za kutosha, kwa sasa hivi ni tofauti ila waliwekeza wanaotumia njia za kisasa wanapata pesa mno, kwa average pale soko la dhahabu wanauza kilo 300-400 kwa mwezi
 
Kutafuta huwa mambo yanatokea.
Pale Nzuguni pembeni ikulu Chamwino iliibukaga dhahabu miaka hiyo.
Niko na binamu zangu wasela mavi Dom nzima inawajua enzi zao.
Tukabeba sululu,majembe,beleshi twenzetu.
Nna miaka 14 hapo.
Ule Msoto kule niliopata Mungu anajua.
Ila Wajomba wao life walikua ni watu wa bata tu.
Ni kila siku bwii, madem wale jamaa.😁
Sasa sielewi walikua wanapora au vp.
Mi nasota shimoni nikicekecha hola .
Wao wako mabanda ya gongo wanalewa.
Nikaona hapa ntakufa.
Nilitoka na buku 15 tu kule.
Nikala boda pori sio pkpk hadi main road
Panda nyuma ya pick-up imetoka mpwapwa.
Ndo pona yangu.
Kilizuka kipindupindu
Wote wakafukuzwa kule.
Ndo mazee wakarudi home.
 
mulemule mwanangu ,hilo life ulilo liacha 2007 lipo mpaka leo ,mm nimetoka majuzi juzi tu itumbi,matundas, mkwajuni ,saza kwenye maduara,plant na karashani yote ni kanda hio hio ya chunya mpaka mkoa wa sngwe.


mm naongezea niliyo yaona vibarua hudhulumiwa na maboss zao, mauaji ya kiholela na uharifu, starehe na ngono za kupindukia.


the same to me nilipata msaala nikalala mahabusu wiki mbili mkwajuni, ndugu wakaja wakanitoa kutokana na ishu ya kuuza dhahabu feki(kakumba)


vijana tunakata kona ambazo hazikati kutafuta ridhiki,japo sijatusua naimani jah atablesi tu
 
Kooma usikate tamaa

Maisha ubish

Ova
 
Yaani Kuna mambo lazima akili Yako ifanye kazi kwasababu unakuta huko unakoenda na unaambiwa Kuna utajiri, utawakuta watu wanauza machungwa na biashara ndogo ndogo . Bado hujiulizi kama utajiri hupatikana kwa kutumia nguvu tu je, Hawa wanashindwaje?
Mfumo ndiyo uko hivyo

Ova
 
Nljichanganya nkaenda mwakitolyo bila mtaj nkasema ntakomaa asee🙌 kwanza jua n kal sana kulko sehem yoyote tanzania dhahabu kupatikana nikwa mbinde sana yan unachakaa mpaka unajisahau siku ukitaka kwenda mjin inabid upumzke hata siku mbil kwanza unyoe uoge mara mbil mbil il kesho hata ukienda mjin uonekane n mtu. Machimbon maisha ni ghal sana na hela ni ngum sana kupatikana
 
To be honest, hakuna baba ambae anaeweza kumpeleka mtoto wake aliye mzaa kwenye kazi ya machimbo madogo madogo.
Hii kazi ni ngumu sana, hatarishi sana na sio ya uhakika ziaidi ya matumaini.
mjomba yangu mbona alimpeleka mwanae motipwezi na akatoboa na ni mwanae wapekee shida ni moja ninyi wengine mumelelewa kwa mfumo wa upinde....tupo wadogo tunazingua kutoenda shambani mama yako anakunyima chakula au kukuambia haulali ndani na kweli haulali
 
To be honest, hakuna baba ambae anaeweza kumpeleka mtoto wake aliye mzaa kwenye kazi ya machimbo madogo madogo.
Hii kazi ni ngumu sana, hatarishi sana na sio ya uhakika ziaidi ya matumaini.
Acha uongo, Kwa hiyo wanaoifanya kazi ya machimbo ya dhahabu ni wale wasio kuwa na baba zao wa kuwazaa.
Loh! Mnaleta uongo humu jukwaani ambako Kuna watu wanajua stories zote za machimbo.
Machimbo ni Kwa yeyote, na siku hizi hadi wakinamama nao ni wasaka fursa za machimbo ya madini mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…