Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Bwana Yesu Asifiwe. Tusifike mbali maisha ya machimbo ya dhahabu yasikie tu kwa jirani kama unampenda mtoto wako huwezi ruhusu akatafute maisha machimbo sisemi kwamba watu wasiende ila naandika hapa siwezi rudi tena machimbo kwangu mimi ni heri saidia fundi lakini sio maisha ya solovea maporini.

Ilikuwa ni mwaka 2007 nilipelekwa na mdingi wangu Kwenda kuchimba machimbo ya dhahabu CHUNYA Mbeya kufupisha stori ile nimefika tu kijiji napokelewa na watu walio choka balaa wamekunywa pombe na wengine sigala yani mtu ukimuangalia nguo alizo vaa zilivyo chakaa duh nilivyo ona tu hivyo pale kijijini mbona nilianza kudata na Nguvu zilianza niishia kidogo.

Sikueleza jina la kijiji hapo nyuma kijiji nilichofikishwa kilikuwa Kinaitwa Igundu Ila kazi tulikuwa tunafanyia mapori fulani mbali kidogo yani kuna kijiji kingine unakipita Kinaitwa mwankonyonto ndio unafika sasa kwenye Eneo tuliko kuwa tunachimba haya tuendelee.

Basi Baada ya kukutani na zile sura ngumu of course Nguvu ziliniisha Nikaanza muona dingi kama vile kaja kunileta matesoni maana story nilizo kuwa nasikia vijiweni ni kwamba watu wa machimbo wanapesa lakini nilivyo Kutana ni tofauti na mategemeo yangu nilitegemea nitawakuta wapo kawaida na sio kwa kuchakaa waponcha kiukweli walikuwa wamechoka balaa nasikia tu harufu Za sigala basi bwana

Kutokana Na mda nilio kuwa nimefika ulikuwa ni jioni jioni kama saa 11 Au kumi na mbili jioni hivi nikaomba wanipeleke nikampumzike maghetoni mwao basi jamaa mmoja hivi jina nimpe Kibakuli akanipeleka mpaka wanapolala maana ilikuwa ni hapo hapo kijijini Igundu ila pembeni kidogo porini ndio walikuwa wanalala hapo lakini mimi hapo akilini mwangu wakati Kibakuli akanipeleka gheto nikapumzike nikajua ni gheto chumba KIZURI cha kawaida tu kama nilivyo zoea tu Vya mjini.

Basi bwana nikiwa njiani na Kibakuli kuelekea ghetoni sasa Nikakuta huyu mshikaji mbona kama tunatembea mpaka tunaanza kukiacha kijiji cha Igundu na tunaanza ingia porini nikajiuliza gheto gani hili lipo porini hivi basi bwana baada ya kukiacha kijiji cha Igundu kama km moja ndio Nikakuta washikaji kumbe wametengengeza kambi la turubai porini duh hapo ndipo nilipo choka Zaidi maana baada ya kufika hapo kambini yani pale palikuwa hakuna godolo wala branketi nilikuta Chini wametandika mabox na yenyewe yamechakaa balaa na vipisi Vya sigala Vya Kutosha.

Nilivyoyaona Hayo kiukweli nikachoka sana nikasema Hapa ni pa moto aise na hapo ndio mwanzo tu malazi Yapo hivi je hiyo kazi ya kuchimba itakuwaje kiukweli nilichoka na kukata tamaa basi baada ya Kibakuli kuniambia ndio Hapa mwanangu gheto akaniacha Akaniambia dagaa hizo mwanangu na ugali Huo kiberiti hicho kuni utaingia porini humu humu zipo nyingi tu aise kimoyo moyo nikasema Hapa nimefika ni pamoto nikamjibu tu fresh mwanangu mimi kamanda nitaungurumisha.

Lakini kiukweli Nguvu Za kupika nilikuwa sina maana nilikuwa nawaza sijui nirudi nyumbani Au nikiamka kesho Niseme naumwa ili nirudi home maana haya maisha kwa mwanzo tu huu yamenishinda anyway nikawaza waza giza likaingia nikaona nilale tu na wakati Huo mimi Nipo peke yangu hapo porini washikaji wapo kijijini wanakunywa pombe hofu ikaanza niingia Kutokana ndio mara yangu ya kwanza kukaa peke yangu vile Afu porini nasikia kelele Za vyura tu.

Lakini nikajipa moyo kwamba washkaji watakuja hata saa tatu usiku lakini ikafika saa tatu usiku hola kimya saa NNE hola pia saa tano hola mpaka saa 6 NA nusu ndio nikawa nasikia kama watu wanaoongea Afu wanakuja upande wangu kwanza wenge likanishika nikawa na mashaka lakini kwa kadili walivyo kuwa wanasogea na Maongezi yao nikawasoma tu kwamba Ni Kama watu waliolewa pombe na kweli baada ya sekunde kadhaa watu hawa Hapa "dogo vepe umelala mimi sikuwajibu Kitu ila mwisho Kutokana Na kelele zao nikawajibu kama mtu alie kwenye usingizi ndio nimelala"

Basi Baada ya kuwajibu wakaanza story zao yani kesho tunapiga hela na mgeni amekuja pale lazima tuwashe mkanda "maana ya Kuwasha mkanda ni dhahabu Kutoka nyingi" Basi wakapiga story sana mimi zile story zao zikanipa Nguvu nikasema moyoni yesi kesho siondoki kumbe tunaenda Kuwasha mkanda Lakini mimi siku hiyo sikulala maana usingizi haukuja Kutokana Na sehemu ile panavyo minya aise.

Basi kulivyo kucha asubuhi mapema masela walikuwa wameamka walikuwa watatu jumla na huyo Nilie mpa jina Kibakuli basi tukasalimiana maana hapo wote walikuwa na akili zao na sio Za pombe basi wakasema tufanye fasta ili tukachukue kipimo kijijini Igundu na sululu na makoleo sehemu wanapoachaga vyombo basi tukabeba unga wa ugali kwenye vile vibegi vyeusi wanaita vibobu na dagaa kidogo mimi sasa nikaawambia mbona mnabeba unga mwingi sana hivyo na mimi sili sana chakula basi wakacheka wa kaniambia we wa Town tu.

Basi tulivyo Fika kijijini Igundu tukachukua kipimo na sululu na makoleo na kipimo fulani kidogo Kinaitwa Fisher gold Bug 2 kina kasahani kadogo sana Basi bwana baada ya kuchukua hivyo vifaa tukanunua na mafuta ya kupikia ya mia tano safari ya kuelekea kazini ikaanza aise tulitembea sana kama km 3 hivi maana ni Mbele ya kijiji fulani Kinaitwa mwankonyonto ukivuka hicho kijiji kwa Mbele ndio Unakuwa umefika na hapo ni umebaba sululu na koleo kila mmoja

Basi Baada ya kutembea sana tukafika Eneo la kuchimba tukawakuta na baadhi ya watu wanachimba basi Yule mjomba mwingine tumpe jina sekesa Akaniambia Wewe dogo utachimba Hapa nikasema poa tena kwa Nguvu yote basi bwana nikaanga kuchimba aise ile kazi ni Ngumu Kuliko kazi zote maana nilichimba mpaka Nikaanza kuona kizungu zungu na hewa nakosa basi nikauliza kwa sauti Kubwa jamani maji Yapo Hapa mmoja wa wale Jamaa tulio wakuta Akaniambia yale pale kwenye mti aise nikaenda fasta nikanywa yale ndio kujisikia Nafuu.

Basi sasa ikawa nikichimba kidogo naenda kupozea na maji kidogo maana nilikuwa nikipiga ile sululu ndefu iliyofulishwa (chongwa) kifua kilikuwa kina pata moto mpaka wale Jamaa wengine tulio wakuta wakasema huyu atamaliza kweli hii kazi basi nikaenda na mwendo Huo lakini kazi haisogei Jua linapiga balaa aise kazi ya kuchimba ni ngumu sana nikaenda nayo wee mpaka saa tisa kazi imesogea kidogo udongo nilio chimba ili kipimo kije kinipimie ulikuwa mdogo sana na nimechoka balaa basi akaja Jamaa wa kipimo akazungushia ule udongo wangu wanaita kibongo Bongo hola hakuna cha dhahabu wala nini Akaniambia nianze kusambaza ili wapime kwa kusambaza aise nilisambaza udongo ule lakini hola hakuna cha dhahabu wala nini Mpaka namaliza kusambaza hakuna cha dhahabu wala nini nikapolola (kukosa) dhahabu.

Kufupisha stori nikakomaa machimbo na hali ya kupolola ilikuwa Kubwa Japo siku Zingine tunapata point tatu Au tano na kipindi hicho point moja ni ilikuwa Elfu 8 kwa Kifupi hali ya machimbo ni ngumu maana unga mda mwingine ulikuwa unakata na mpo polini chawa zikaanza kunitesa maana mda wa kuoga ukaanza kuwa hadithi kwangu Kutokana Na mda ninao rudi mbovu na hela sina mfukoni nimepolola chakula mda mwingine hamna labda ukaombe kambi lingine maisha ya kushindia matunda ya porini matoo na michongoma ndio yakawa kawaida yetu Nikaanza Kushinda vilabuni na wale masela kwa Kifupi kipindi KILE nawaona wale masela wamechoka hawachani nywele wamevaa nguo zimechanika chanika yani mimi Na wao tukawa sawa tu.

Maisha yakawa ni Kushinda VILABUNI Lakini asubuhi mapema unajikaza uende kazini ukipata point moja mbili sawa Japo kukosa ilikuwa ni mara nyingi sana ukifika kijiji ni kushindia pombe Au na viazi Vya kugongea ili baki kidogo tu nianze kuvuta sigara na bangi kwa Kifupi nilichakaa kuzidi wale Jamaa nilio wakuta KUMBU KUMBU YA MWISHO WALITUMWA NDUGU TU KUJA KUNICHUKUA MAANA.

Katika Wale Jamaa Watatu Wawili Nilikuja Kusikia Walipata Ukimwi Na Yule Mmoja kibakuli sijui aliishia Wapi.

MIMI KWA SASA NASHUKULU NI MZIMA NA POMBE NILIACHA NAENDELEA NA MISHE ZANGU TU HAPA MBEYA TOWN ILA NIMALIZE TU KWA KUSEMA MACHIMBO YA DHAHABU NI ZAIDI YA JESHI LA TALIBANI SIJI KURUDI.

Bonge la stori
 
2007 ni kitambo sana, kipindi cha hapa kati, njia za kisasa za ku extract gold zilikuja, yale mabaki yaliyokuwa yanaachwa kipindi cha nyuma yalitajirisha sana watu, walikuwa wanayaacha wakidhan hayana dhahabu kumbe yana dhahabu za kutosha, kwa sasa hivi ni tofauti ila waliwekeza wanaotumia njia za kisasa wanapata pesa mno, kwa average pale soko la dhahabu wanauza kilo 300-400 kwa mwezi
We unazungumzia saineti ambalo linaitwa rudio.

Hicho kipindi ambacho yeye alikuja shughuli za uchimbaji madini zilizokuwa zinafanyika miaka hiyo ilikuwa ni uchimbaji wa kusambaza.

Maeneo machache sana yalikuwa yanafanya extraction ya madini kutoka kwenye mawe.

Nakupa mfano mmoja Chunya Mjini kulikuwa kuna wazungu eneo fulani karibia na Kanisa la Mashahidi wa Yehova.

Hao wazungu walikuwa na mitambo ya kusaga mawe ndio waliokuwa wanatoa dhahabu za kwenye mawe.

Miaka ilivyosogea sogea ndio watu wakaanza kushtuka nao wakaja na makarasha wakawa wanasaga na profit kwa mwenye mashine alikuwa anategemea kwenye cash ya mteja anayo mchaji kwa ajili ya kumsagia mawe yake.

Lakini ilivyokuja hiyo tech ya kukamua tena ile rudio naskia wameshusha gharama huku wengine wakifanya free kusaga, kwasababu wanajua at the end watakuja kunufaika kwenye rudio.
 
Acha uongo, Kwa hiyo wanaoifanya kazi ya machimbo ya dhahabu ni wale wasio kuwa na baba zao wa kuwazaa.
Loh! Mnaleta uongo humu jukwaani ambako Kuna watu wanajua stories zote za machimbo.
Machimbo ni Kwa yeyote, na siku hizi hadi wakinamama nao ni wasaka fursa za machimbo ya madini mbalimbali.
Kwa simulizi ya huyu mwamba maana yake alipelekwa kwenye small mining scale/uchimbaji mdogo/uchimbaji wa kienyeji.
Ukweli ni kwamba kwenye mining industries, hakuna mzazi wa mtoto anae weza akakubali kumpeleka mwanae akachimbe kwa sururu pasipo kujua kama anauhakika wa kupata hata 1 point, ukiacha 1 gram
 
Kutafuta huwa mambo yanatokea.
Pale Nzuguni pembeni ikulu Chamwino iliibukaga dhahabu miaka hiyo.
Niko na binamu zangu wasela mavi Dom nzima inawajua enzi zao.
Tukabeba sululu,majembe,beleshi twenzetu.
Nna miaka 14 hapo.
Ule Msoto kule niliopata Mungu anajua.
Ila Wajomba wao life walikua ni watu wa bata tu.
Ni kila siku bwii, madem wale jamaa.😁
Sasa sielewi walikua wanapora au vp.
Mi nasota shimoni nikicekecha hola .
Wao wako mabanda ya gongo wanalewa.
Nikaona hapa ntakufa.
Nilitoka na buku 15 tu kule.
Nikala boda hadi main road
Panda nyuma ya pick-up imetoka mpwapwa.
Ndo pona yangu.
Kilizuka kipindupindu
Wote wakafukuzwa kule.
Ndo mazee wakarudi home.
Kwenye shughuli ya machimbo unabeba zana ya jembe?

Basi hiyo ardhi ni soft sana

Nenda Chunya utaoneshwa sululu zilizopinda baada ya kukutana na hardcore rocks na vijana hawataki kukubali kuwa imeshindikana.
 
mulemule mwanangu ,hilo life ulilo liacha 2007 lipo mpaka leo ,mm nimetoka majuzi juzi tu itumbi,matundas, mkwajuni ,saza kwenye maduara,plant na karashani yote ni kanda hio hio ya chunya mpaka mkoa wa sngwe.


mm naongezea niliyo yaona vibarua hudhulumiwa na maboss zao, mauaji ya kiholela na uharifu, starehe na ngono za kupindukia.


the same to me nilipata msaala nikalala mahabusu wiki mbili mkwajuni, ndugu wakaja wakanitoa kutokana na ishu ya kuuza dhahabu feki(kakumba)


vijana tunakata kona ambazo hazikati kutafuta ridhiki,japo sijatusua naimani jah atablesi tu
Itumbi napasikia sikia tu sikuwahi kufika, ukanda wa kusini maeneo ya matundasi, makongorosi na mkwanuni sijawahi kufika.

Ishu ya kudhulumiwa ipo sana ngoja nikupe kisa kimoja.

Kuna siku tulienda kuchimba Chunya mjini eneo moja linaitwa swiswi maeneo fulani hivi ya porini milimani kule karibia na minara ya simu.

Kufika kule nikakutana na wazee wengi waheshima nikawa najua hapa busara zipo.

Wakati naendelea kuchimba upande wa pili kuna mwana alikuwa tayari ameufikia mwala, so akaita kipimo kije kupima.

Kipimo kilivyokuja, kuna bro mmoja akatoka kwenye shimo lake akaenda kuangalia huyo mwana anavyopimiwa.

Katika kupima, kipimo kikatoa mlio ishara ya kuonesha kuna dhahabu au metal objects

Sasa ule wakati wa kuchota mchanga kugawa kwenye viganja kujua ni dhahabu au kibati, alikuja yule bro ambaye sio shimo lake, akachota mchanga kwenye viganja viwili akawa anagusisha kwenye sahani ya kipimo.

Kipimo kilivyopitishwa kwenye mkono mmoja alioshika mchanga hakikulia, akautupa ule mchanga.

Mkono wa pili kilivyopita kipimo kikatoa mlio, yule bro akasema "aaah kumbe ni kibati" halafu akaurusha ule mchanga mbali kabisa.

So jamaa wakaendelea kupima kwenye mwala, ikaonekana jamaa amepolola akarudi home.

Yule bro alisubiria watu wote wameondoka akaruri kwenye ule mchanga alioutupa kumbe kulikuwa na dhahabu sio kibati kama alivyosema, jamaa akachukua dhahabu akasepa zake.
 
Kwa simulizi ya huyu mwamba maana yake alipelekwa kwenye small mining scale/uchimbaji mdogo/uchimbaji wa kienyeji.
Ukweli ni kwamba kwenye mining industries, hakuna mzazi wa mtoto anae weza akakubali kumpeleka mwanae akachimbe kwa sururu pasipo kujua kama anauhakika wa kupata hata 1 point, ukiacha 1 gram
Ilifika time watu wakawa wanapishana.

Yani watu wanatoka mikoa ya mbali kuja Chunya kuchimba madini, na wazawa wa Chunya wanapakimbia kwao wanaenda Zambia na Msumbiji kwenda kuchimba

Yale maisha asikuambie mtu ni msoto sana.

Huko Msumbiji walikoenda zilikuwa zinakuja story za kila aina aisee.
 
Ilifika time watu wakawa wanapishana.

Yani watu wanatoka mikoa ya mbali kuja Chunya kuchimba madini, na wazawa wa Chunya wanapakimbia kwao wanaenda Zambia na Msumbiji kwenda kuchimba

Yale maisha asikuambie mtu ni msoto sana.

Huko Msumbiji walikoenda zilikuwa zinakuja story za kila aina aisee.
Wachimbaji wadogo wengi sana walifia Zambia na Msumbiji kwa kisingizio cha uhamiaji haramu, uhalifu na kugologosha.
Na wengi waliofanikiwa kukutana na vikole (pure gold) ndio walikutana na majanga ya aina hii...
 
Wachimbaji wadogo wengi sana walifia Zambia na Msumbiji kwa kisingizio cha uhamiaji haramu, uhalifu na kugologosha.
Na wengi waliofanikiwa kukutana na vikole (pure gold) ndio walikutana na majanga ya aina hii...
Kule kulikuwa kuna sheria ngumu kwasababu mostly hawakuwa na passport

Na bado ilikuwa hairuhusiwi kuondoka na dhahabu kule.

Wachimbaji wa huku hawakuwa tayari kuuza dhahabu Msumbiji kutokana na kwamba soko lao ni dogo, wananunua kwa bei ndogo ambayo haiwafaidishi.

Kuna jamaa alikuja home akiwa na kidonda kikubwa, akatuambia hiki kidonda ni cha kujitakia maana bila hivi nisingeweza kuficha dhahabu.

Watu tukabaki hoi midomo wazi, maswali ya mshangao tukamuuliza ina maana mchizi ulijitoboa ili ufiche tu dhahabu. Akasema ndio kwa maana kule hata kipimo tu wakikukamata nacho wanapora.
 
Uchimbaji wa dhahabu ni mgumu sana kuna jamaa mwaka jana kaacha kazi Benki kaingia kwenye hizi mishe kule Kilindi Handeni kapoteza zaidi ya milion 25 na aliambulia 7grms tu. Kazi kapoteza, hela imeisha na familia yake imemdhrau na kumtenga yaani sasa hivi kachanganyikiwa kwa kifupi dishi limeyumba na kapoteza dira kabisa na sasa hivi kaingia kwenye kubet 😅
 
Ushaelewa nazungumzia labda hata hujazaliwa, 90 huko
Unaweza ukawa mkubwa kwangu hilo naliheshimu.

Ila unachoshindwa kuelewa ni matumizi ya maneno kulingana na eneo.

Ukiwa Chunya ukimuambia mtu ulikuwa unachekecha, hautoeleweka hata umuambie mzee wa 1930.

Ukimuambia ulikuwa unasekesa au kuosha hapo atajua unazungumzia aina gani ya uchimbaji

Kuna kusekesa, kuosha, kupiga makarai, kusaga mawe na kubinuka (kusambaza)

Hizo ndio slang za machimboni kwa Chunya
 
Back
Top Bottom