Maisha ya mfalme Bolkiah wa Brunei yanatisha

Maisha ya mfalme Bolkiah wa Brunei yanatisha

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Jina lake halisi ni (Sultan Haji Hassanal Bolkiah Mu'izzaddin Waddaulah ibni Al-Marhum Sultan Haji Omar Ali Saifuddien Sa'adul Khairi Waddien Sultan and Yang di-Pertuan) wa Brunei taifa lilopo mashariki kusini mwa bara la Asia.

Amekuwa sultan wa 29 wa Brunei yenye mji wake mkuu uitwao Darussalam kwa miaka 52 sasa tangu alipoingia madarakani mwaka 1967 kwa kumrithi baba yake.

Mwaka 1980 alitajwa na gazeti la Forbes kuwa mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dollar Bilioni 12.

Mbali na kuwa Sultan pia ni waziri mkuu wa Brunei, pia ni waziri wa ulinzi, amiri jeshi mkuu, waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nje na biashara.

Anamiliki magari mengi zaidi duniani. Kwenye yadi yake Kuna Ferrari 452, Koenigeggs 134, BMWs 209, Jaguars 179, Aston Martin 11, McLaren F1s 11, Lamborghini 21 na Rolls Royals 600. Kwa hivyo pia ana garage kubwa zaidi duniani.

Anamiliki na kukaa kwenye jumba kubwa zaidi duniani lenye ukubwa wa ekari 49, Vyumba vya kulala 1788 na mabafu ya kuogea 257.

Ni msomi wa hali ya juu akijikusanyia jumla ya shahada za awali (bachelor degree) 6, shahada za uzamili (Masters degree) 6 na shahada za uzamivu (PhD) 2.

Ameifanya nchi yake kuwa ya kwanza kwa wananchi kutokulipa kodi. Huduma zote za afya ni bure kwa watu wote. Hazina ya mafuta na utalii ndizo zinalisha nchi nzima.

Anamiliki ndege iliyotengenzwa kwa dhahabu yenye thamani ya pesa za kitanzania Shilingi Bilioni 520. Ndege hiyo ina sebule, vyumba vya kulala na bafu na choo. Yeye mwenyewe ndiye rubani wa ndege hiyo.

Anamiliki viwanda vya kusafisha mafuta zinazomuingizia kiasi cha Dollar 6,000 kila dakika sawa na Shilingi milioni 13 za Kitanzania.

1618381571830.png
 
Huyu sasa ndiye Sultan anaye stahili kuliliwa anapofariki! Siyo yule Sultan mwingine wa Darissalam aliyewaacha wananchi wake katika dimbwi la umaskini kwa sababu ya ukaidi, ubinafsi, ubaguzi na maamuzi yake ya hovyo!

Halafu kuna kenge eti wanamliliia baada ya kufariki!
 
Back
Top Bottom