Maisha ya mwana JamiiForums nje na ndani ya JamiiForums

Maisha ya mwana JamiiForums nje na ndani ya JamiiForums

Acheni kufuatilia maisha ya watu hayawahusu. Pambaneni na hali zenu. Si kila mtu humu ni muongo wa kujikweza. Niliobahatika kuwafahamu humu ni watu bomba sana na wengine wana maisha mazuri sana kwa kuchakarika kwao kwenye elimu na biashara.

Mbona kuna wengi humu wanakuja kuomba misaada ya aina mbali mbali na wanasaidiwa!? Mbona hao hamuwasemi!?

Mambo ya Ngoswe mwachieni Ngoswe. Si kila mtu humu ni muongo au mtu wa kujikweza wengi wako kimya mpaka mpate bahati ya kufahamiana kwa karibu.
 
Asalaam wanajukwaa!!

Katika kutumia mtandao huu ( jamiiforums) mzuri na ninaoupa kipaumbele sana nimepata uzoefu na maswali mengi yakinizunguka akilini mwangu kuhusu members wa hii familia ya jamiiforum.
Kutokana na maswali hayo yalinipa hitimisho ama uzoefu mpya kabisa!!

Kiukweli namna watu wanavyojipambanua humu, ni tofauti kabisa na hali zao zilivyo, nafafanua kwa kila kundi ama jinsia kama ifuatavyo:-

1 KUNDI LA WANAUME WA JF.
Wanavyojisifu:-
I/wengi kama sio wote wana miliki magari au usafiri mzuri, yaani wengi hawapandi daladala kwenda kazini ama majumbani Kwao

ii/ wengi kama si wote wana kazi nzuri zenye mishahara mizuri, hapa utakuta watu wanabeza hasa wenzao wanaolipwa mfano laki Tatu au mbili kwa mwezi.
iii/ wengi kama sio wote ni watu wa vitengo ( usalama wa taifa na wanajeshi)[emoji23] [emoji23] [emoji23]
iv/ Hakuna asikari polisi hata mmoja humu jamiiforum, huwezi kukuta mtu akijipiga kifua humu kuwa yeye ni polisi ila tuna wajeda karibia wote humu[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87]

v/ Humu walimu wanadharaulika kwa sababu wanalipwa kidogo. Hivyo hatuna member ambao ni maticha humu labda tupate Leo.
vi/ wanaume wote wa jamiiforum hawatumii TV za chogo majumbani/ maghetoni Kwao, wao wana flat screen TVs ( smart TV) za bei kubwa hivyo yeyote anayetumia TV ya chogo huhesabiwa mlalahoi wa jf.

2.KUNDI LA WANAWAKE.
I/wote ni warembo, yaani vibinti vibichi.
ii/ wote wana K mnato.
iii/ wote ni wahitimu wa kuanzia shahada ( degree). Humu jf hakuna mwanamke mwenye elimu darasa la saba au form four.
iv/ kuwahonga mademu wa humu jamiiforum labda uanzie laki mbili na si chini ya hapo.
v/ wengi kama sio wote wamepanga nyumba nzima yaani apartment.
vi/ vinywaji vyao ni saint Anna, savanna, Grants, na castle lite kwa Mara chache.
vii/ Hakuna majimama humu jamiiforum, wote ni vimwana wazuuri.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]

HITIMISHO.
Kijana mwenzangu usijaribu kushindana na mazuri ya jamiiforum, kwani huu ni ulimwengu wa waliofanikiwa ( the world of granted).
Ingia shambani lima, fundisha, cheza italipa zaidi.

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Hahaaaaaaa haaaaa haaaaa... Daaah!! Hapo kwa wanawake wa JF kiboko
 
Sasa wee jamaa unachoshangaa ni kitu gani? Unataka tutumie ID fake lakini tuwe halisi? Mtaani kunabaki kuwa mtaani na JF yanaishia JF.

Hata hivyo iwe mtaani au JF, usijilinganishe na mtu mwingine. Usimchukie bila sababu anaekuzidi, chukulia kama changamoto ufanye vizuri zaidi yake.

Hali kadhalikabusimdharau unaemzidi, ongeza bidii usirudi huko.
Hahaaa mjomba mie sio hater ni jamaa simple sana mwenye kupenda furaha, tuko pamoja sana
 
Acheni kufuatilia maisha ya watu hayawahusu. Pambaneni na hali zenu. Si kila mtu humu ni muongo wa kujikweza. Niliobahatika kuwafahamu humu ni watu bomba sana na wengine wana maisha mazuri sana kwa kuchakarika kwao kwenye elimu na biashara.

Mbona kuna wengi humu wanakuja kuomba misaada ya aina mbali mbali na wanasaidiwa!? Mbona hao hamuwasemi!?

Mambo ya Ngoswe mwachieni Ngoswe. Si kila mtu humu ni muongo au mtu wa kujikweza wengi wako kimya mpaka mpate bahati ya kufahamiana kwa karibu.
Anaongelea aliokutana nao lazima.
 
Hata Insta Facebook SnapChat mambo ni haya haya. Unakuta mdada anapost kila siku yupo Cape town Fish Market ila hata pa kuishi hana anaishi kwa mashoga. Ukiishi kwa kutegemea maisha wanayoishi wengine kwenye social media unaweza ukawa shoga au punda au malaya. Turidhike na tulipo. Tupiganie maendeleo kwa faida yetu sio kwa sababu ya fulani.
Kweli kabisa mzigua
 
Hiyo nambari 5 (v) inaonekana umgeni humu.kuna waalimu kibao na wala hawajifichi kuna mpaka nyuzi ya waalimu kubadilishana vituo vya kazi.

Cha msingi nakushauri usipoteze muda kuwatafakari na kutaka kuwajua watu.haitakusaidia lolote.we ingia jadili hoja/mada zilizopo ukimaliza kafanye mambo mengine
 
Alichoshindwa kuelewa mtoa mada ni kwamba. Kwenye jamii yoyote hao aliowataja wapo. Wapo watu wana sifa zote humu alizozitaja na kweli ndo maisha yao halisi hawaigizi. Na wapo watu sio maisha yao wanaigiza. Kwenye mitandao yote tunao hao watu. Sio humu tu.
 
Hata Insta Facebook SnapChat mambo ni haya haya. Unakuta mdada anapost kila siku yupo Cape town Fish Market ila hata pa kuishi hana anaishi kwa mashoga. Ukiishi kwa kutegemea maisha wanayoishi wengine kwenye social media unaweza ukawa shoga au punda au malaya. Turidhike na tulipo. Tupiganie maendeleo kwa faida yetu sio kwa sababu ya fulani.

Cape Town Fish Market mimi naendaga kweli.
 
Acheni kufuatilia maisha ya watu hayawahusu. Pambaneni na hali zenu. Si kila mtu humu ni muongo wa kujikweza. Niliobahatika kuwafahamu humu ni watu bomba sana na wengine wana maisha mazuri sana kwa kuchakarika kwao kwenye elimu na biashara.

Mbona kuna wengi humu wanakuja kuomba misaada ya aina mbali mbali na wanasaidiwa!? Mbona hao hamuwasemi!?

Mambo ya Ngoswe mwachieni Ngoswe. Si kila mtu humu ni muongo au mtu wa kujikweza wengi wako kimya mpaka mpate bahati ya kufahamiana kwa karibu.
Asipokuelewa kwa ulichoandika basi ana lake jambo.

Ila BAK inabidi na Emmy umfundishe kuandika gazeti sababu sio kwa gazeti hili. Lol [emoji85]
 
Hahaaa mjomba mie sio hater ni jamaa simple sana mwenye kupenda furaha, tuko pamoja sana

Sijasema ni hater mkuu..namaanisha mambo ya huku ni ya hukuhuku na mtaani ni ya mtaani. BAK ametoa maelezo mujarab, inategemea na mtu anataka nini JF, kwangu cha kwanza ni kupata burudani, napunguza nyongo za stress zangu, pili elimu na updates za mambo mbalimbali.

Pia kuna watu wenye uzoefu wa kada mbalimbali huku, huwezi kupata hiyo fursa kwingine kwa wakati mmoja.
 
Back
Top Bottom