Maisha ya ndoa anayo pitia ndugu yangu ni mateso, je amelogwa?

Chief bakupa pole sana. Ulikosea nwanzi kabisa ulipo amua kuishi kwake.

Ni kosa kubwa sana na si uana ume inapotokea mwanamke hakutaki ukawa unang'ang'ania. Ondoka chief ondoka. Tena ikiwezekana hapo baadae tafuta uhamisho ukapambane mbele ya safari yaani usionane naye.

Lakini nakukumbusha tu wewe hukuwa na MKE bali ulikuwa una mwanamke uliyefunga nae NDOA.

Jingine ukiachilia mbali hilo, je hakuna ambayo ulikuwa una mkosea mwanamke wako ? Aidha manyanyaso hapo kabla au kuchepuka au ushirikina na mfano wa haya.

Natamani ningesikia upande wa pili nao una yapi ya kusema.
 
Jamaa yupo kwenye hizi traps.. financial traps, woman traps na ushamba traps!!.. akitoka kwenye hizo traps hatakuja kujuta.

Ushamba ninaouzungumzia sio ushamba wa kawaida ila ni ile kushindwa kuangalia vitu kiundani zaidi!
Hii nondo muhimu saana,umezungumza.
 

"nina umri wa miaka 33 na mke wangu ana umri wa miaka 31.Ndoa yetu ina muda wa miaka mitatu"

Bado mdogo hivo unateswa na mwana mke hata ningekua sina mshahara kabisa kwa umri huo siwezi kulala hata siku moja hapo, na ondoka nanguo tu naanza maisha mengine mapya kwanza huyu mwana mke ni mkubwa sana kwako sio wa kuoa
 
Kodi ya single room=40 to 50k.
Unga 25kg= 20k
Gas ndogo=20k (naamini mtungi anao)
Mafuta ya kula=5k
Mchele 5kg=8k
Maji+umeme=8k
Sabuni+mafuta=15k
________
JUMLA. =130k.
Mwambie aondoke, hiyo pesa inatosha sana kufanya maisha ya kujibana. Kama alizoea bata+ mbwembwe kwa wananzengo, basi imekula kwake. Akijifanya kugoma, asubiri kuletewa kidume hapo ndani.
NB: vitu ajitahidi ahamishe kwa kichwa maana sio mbali. Mita 100 tu sio parefu kwa mwanaume.
 
Ondoka kaanze maisha upya mapema
 
Sometimesbin life a man has to be a man no matter what....

Hukukosea kuhamia kwake ila ulikosea ku focust future yako na mahusiano kwa ujumla..
Katika maisha usipende kumruhusu mtu mwingine asimame katika nafasi yako hasa hasa MWANAMKE.

Usimuachie nafasi ya kichwa cha familia
Usijenge kwenye kiwanja alichojinunulia au hata kuhamia anakoishi
Jifunze namna ya kuongeza kipato ili ujitofautishe naye..

HAMA KAANZE UPYA kama unampenda unaweza kuhama nae ..Kuanza upya sio kazi kazi ni kwa wewe kuchukua maamuzi ya kiume

Kuwa MWANAUME BRO
 
Kikubwa aikubali hali yake aliyonayo, akaanze upya kuliko mateso anayopitia kwa sasa. Ukisasa utatutesa sana, mnatongozana asubuhi alafu kesho asubuhi mnafunga ndoa. Alikosea tangu mwanzo ameingia kwenye mahusiano hayo.
 
moja kati ya vitu ninavyoviogopa maishani mwangu ni kuchuma mali pamoja na mwanamke .... kutokana na sheria zetu hizi za haki sawa kwa wote, unaweza jikuta unapukutishwa kila kitu unaachwa na pumbu tu .... kama hajachuma chochote na huyo mwanamke ni vyema angesepa tu akaanze maisha yake mapya ....
 
Niligharamia harusi kwa asilimia 80,ni kipindi ambacho ilinilazimu kuingia kwenye mikopo mirefu,Maana yeye pia nilimkuta ana mkopo. Nilichukua mkopo wa muda wa miaka 7,kiasi cha pesa kiliweza kutumika kwa ajili ya sendoff.



Duh [emoji849] pole sana, wenzie wanachukua mikopo na kufanyia maendeleo yeye akakopa kwa ajili ya sendoff?! Real!
 
Huyo ni yeye wala hujakosea ila tokana na stigmatization iliojaa hapa jukwaani ukisema huna kazi au mkasa wowote unaokusibu watu wanaamua ku impersonate watu wa jirani kwa niaba yao. Ila Mchizi toka alivyopost mkewe kaanza kiburi i thought he must be in deep shit!
 
Amtafute witnessj huyu mrembo hana shida na watu wenye vipato vidogo cha muhimu upendo kwake ila pia cariha alisema yeye hababaiki na ma star kama domo so pia anaweza kumfaa mtoa mada.
 
Chief,mimi visa vyangu vyote nilivileta humu..jaribu kufuatilia nyuzi zangu za kutendwa tangu mwaka 2016 mpaka 2018.
Vyote niliviwasilisha kama vilivyo..(Ruksa kupitia hizo nyuzi maana hazijafutwa).
By then mimi bado sijaoa na nina maisha yangu,na sijaajiriwa..ingawa niliwahi kuajiriwa.
 
Unaweza kushangaa karogwa kumbe anamatatizo yake kingine m naona muachane nao kwanza kitendo cha hyo mama kukaa kazin miaka yote hyo ndo anaolewa sa hv n hatar kiufupi wote wana matatizo ko achana nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…