Maisha ya Nigeria

Maisha ya Nigeria

Mchambuzi Mzuri hawezi kuandika hivi:

Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao.

Duniani kwa Ujumla???? WTF ameshindwa hata Ku Google.
Alimaanisha population density
 
Hujaelewa. Ni 'moja' ya nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani.

It means kwenye top populated countries in Africa ipo. Pia 'inawezekana' hata duniani kwa ujumla ni miongoni mwa nchi zenye watu wengi. Top 20 naamini Nigeria haikosekani duniani. Hajasema ni ya kwanza.

Soma uelewe Kiswahili sio unakurupuka mkuu.
Kingine ni kuwa naijiria haijawahi kuwa na published data za census maana Sensa yao huathirika na suala la dini na ukabila! Hii inatokana na inji hii kuwa na rushwa isiyo na mfano! Pole sana Mzee Mrema kwa kufiwa na nke yako kipenzi
 
Mleta mada tambua kuwa mafuta ya Nigeria yanakua refined na makampuni ya kigeni, Shell ikiwemo. Hawa ndiyo wanufaikaji wa mafuta ya Nigeria.
 
Mchambuzi Mzuri hawezi kuandika hivi:

Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao.

Duniani kwa Ujumla???? WTF ameshindwa hata Ku Google.
inaweza kuingia top 10 kweny the world's most populous countries
 
Ndio maana ile mechi tumepigwa, kumbe wengine walienda kuandika Makala badala ya kujikita tunashindaje ile game?

Shwaini kabisa.
Eddoh yupo kamati gani pale Utopolo,alienda kama mwandishi wala sio mwandishi wa Yanga😂😂😂😂
 
Hapa kwetu hakuna vya kuandika. Kila kitu kiko sawa. Makala ndeefu kuhusu Naijeria sisi inatusaidia nini. Ungeandika haya kuhusu serikali yetu ya hovyo ingesaidia kidogo
 
Mchambuzi Mzuri hawezi kuandika hivi:

Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao.

Duniani kwa Ujumla???? WTF ameshindwa hata Ku Google.
Wameshindwa kuichambua content wanakazania eti muandishi mzuri.
 
Edo ukisoma kalamu yake utapenda ila ukimsikiliza anavyoongea sasa utajuta kupoteza muda wako..

Hivi alisoma chuo gani
 
Hapa kwetu hakuna vya kuandika. Kila kitu kiko sawa. Makala ndeefu kuhusu Naijeria sisi inatusaidia nini. Ungeandika haya kuhusu serikali yetu ya hovyo ingesaidia kidogo
Kaamua kuandika yeye wewe unampangia cha kuandika.

Mke mdogo wa mudi una gubu sana mbona mudi humpangii?
 
Mbona kwenye filamu zao wanaonekana wako njema sana,hasa kule lagos?
 
Huwezi kutumia neno 'Kama sio Duniani' wakati Nigeria inashikiria nafasi ya 6. Ukitumia neno hilo unajaribu kutupa maana kwamba Nigeria Kama sio nchi ya Kwanza kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu basi ni nchi ya Pili.
Hapo pana shida sema mashabiki wake watakupinga. Mi nimeshangaa kuweka kidadi ya wanigeria 112m
 
Mchambuzi Mzuri hawezi kuandika hivi:

Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao.

Duniani kwa Ujumla???? WTF ameshindwa hata Ku Google.
Hata mimi nimeshangaa. Halafu hakuna reference aliyoweka.
 
Hujaelewa. Ni 'moja' ya nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani.

It means kwenye top populated countries in Africa ipo. Pia 'inawezekana' hata duniani kwa ujumla ni miongoni mwa nchi zenye watu wengi. Top 20 naamini Nigeria haikosekani duniani. Hajasema ni ya kwanza.

Soma uelewe Kiswahili sio unakurupuka mkuu.
Mwandishi mzuri wa makala huwa anaweka reference.
 
Mambo muhimu ya kujua kuhusu Nigeria kwa kuongeza kwa faida ya wanajukwaa:
1. Nigeria ndo taifa linaloongoza barani Afrika kwa uwingi wa watu kwa sasa inakadiriwa kuwa na watu milioni 201.(That's Africa's demographic giant)
2.Nigeria ndo taifa
linaloongozakuwa na watu weusi wengi duniani.
3.Katika Nigeria makabila makubwa ni matatu ambayo ni Yoruba,Igbo na Hausa-Fulani na ndo yamedominte almost kila kitu katika nchi hyo. Yoruba amedominate civil service,Igbo amedominate biashara(Hawa wawili ndo wasomi zaidi Nigeria na ndo wengi kuliko makabila yote na wote no kutoka kusini) na Hausa-Fulani yeye amedominate jeshi(Hawa ni wafugaji toka Kaskazini)
4. Jiji la Lagos na Abaekuta yaliyopo kusini yote yako kwenye influence ya Wayoruba na kidogo Waigbo wanaoendesha biashara kubwakubwa.
5.Jiji la Abuja lililopo Kaskazini lilianzishwa na majenerali wa Kaskazini (Hausa-Fulani) kuwa mji mkuu ili kipunguza influence ya Wayoruba na Lagos yao.
6.Rais wa Sasa Rtr.Gen.Muhamadi Bihari anatoka Kaskazini na aliwahi kuwa kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo.
7.Yoruba na Igbo wengi no wakristo wa madheebu ya Anglikani na Hausa-Fulani ni waislam.
8.Watu madhibuti nchini jump na wanaotajika ulimwenguni kote wengi wametokea kusini Kama Woke Soyinka,Oluseguni Obasanjo,Fela Kuti(Yoruba) na Chinua Achebe(Igbo).
 
Na Edo kumwembe

Wanigeria wameshindwa kugawana vyema kile kitu kinachoitwa keki ya taifa. Inaonekana ni taifa la watu wajanja ambao kila mmoja anachukua chake mapema na kuwaacha raia wake wakiwa maskini ingawa inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi imara Afrika.

Hauwezi kuliona hilo kwa macho. Kwanza kabisa watu ni wengi. Kando ya barabara za Port Harcourt watu ni wengi na maisha ni vurugu. Hii inatokana na ukweli kwamba Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao. Vitongoji vya Port Harcourt vinaakisi idadi kubwa ya watu Nigeria. Kila kitu kimechakaa. Watu wamechakaa. Magari yamechakaa. Majengo yamechakaa na barabara pia zimechakaa.

Jiji la Port Harcourt linatajwa kuwa lenye utajiri mkubwa zaidi miongoni mwa majiji ya Nigeria. Hapa kuna utajiri wa mafuta lakini pia kuna bandari. Kinachoshangaza ni kwamba utajiri huo unabakia katika makaratasi au serikalini. Raia wake wamechoka, mitaa yake imechoka, barabara zake zimechoka. Naelezwa kwamba Abuja ndio mji ambao walau una majengo ya kisasa na barabara za kuvutia. Vinginevyo Nigeria imechakaa na ni wazi kwamba hesabu za wachumi Nigeria ni nchi tajiri haziakisi macho pindi utakapotembea vitongoji.

Raia wengi ni maskini na watu wachache ni matajiri. Kutoka katika hoteli ambayo Yanga walikuwa wamefikia ya Swiss Sprit kando yake kwa nyuma tu kuna nyumba zilizochakaa ambazo mabati yamewekewa mawe juu ili yasizolewe na upepo. Watoto wanacheza mpira mbele ya macho ya wazazi wao ambao wanapika chakula nje ya nyumba. Naambiwa hapo ndipo yanapoanzia maisha ya mchezaji wa Kinigeria. Kuondoka Nigeria na kwenda kucheza nje ya nchi kuna maana kubwa kwa mchezaji.

Kwanza mchezaji anaondokana na vurugu za jiji lake au mtaani kwake. Mchezaji yeyote wa Nigeria ambaye ataondoka Nigeria na kwenda kwingineko ghafla atajikuta katika jiji zuri, lisilo na vurugu kama ilivyo mitaa ya kwao. Pua yake itapumua vyema na masikio yataondolewa katika kelele zisizo na msingi.

Mtu yeyote ambaye ataondoka Nigeria atajikuta katika nafasi ya kuongeza kipato. Nigeria hii ina watu lukuki lakini ambao hawana ajira. Wengi kati yao wana elimu kubwa ambayo inawapa uhakika wa ajira mahala kwingine au uhakika wa maarifa ya kuishi.

Kwa wale ambao wamezaliwa na vipaji, soka inabakia kuwa njia kubwa ya kutengeneza maisha. Inawezekana katika umri mdogo wakapelekeshwa na mambo mawili. Kwanza ni kuona maisha ya kifahari ya mastaa wengi wanaocheza nje. Lakini pia msukumo kutoka kwa wazazi. Ni tofauti na nchi yetu ambapo baadhi ya wazazi hawaamini kama vipaji vya michezo na sanaa vinaondoa umaskini. Lakini pia mazingira haya magumu ninayoyaona Nigeria haishangazi kuona linamfanya Mnigeria aweze kuishi Shinyanga akicheza Biashara Shinyanga bila ya shida. Kwanza mji wenyewe Shinyanga kwake unakuwa mzuri tu kuishi tofauti na kelele za Port Harcourt.

Lakini, hapohapo Mnigeria hataki kutazama nyuma. Kwa nilichokiona hapa ni ngumu kwa Mnigeria kutazama nyuma kimaisha. Sawa nyumbani ni nyumbani, lakini nyumbani kunakuwa kutamu zaidi kama unaweza kurudi ukaishi kwa utulivu. Kwa nilivyoitazama Nigeria, nyumbani kunaweza kuwa kutamu kwa watu kama kina Jay Jay Okocha. Hawa wana majumba ya kifahari hapa na wana magari ya kifahari. Wanaishi kifahari. Nigeria hapawezi kuwa kutamu kwa raia wa kawaida ambaye hajafanikiwa nje ya nchi. Na haishangazi kuona hawarudi nyuma. Maisha ya Nigeria yana ushindani mwingi. Hakuna kazi ya mwanaume wala mwanamke. Nadhani idadi yao kubwa inasababisha watafute mkate katika ardhi nyingine nje ya nyumbani. Ni kama ilivyo kwa Wachina, Wahindi au Wabrazil. Mkate wa ardhi yao pekee hautoshi.
Hiyo ndio Afrika,watu wakiambiwa Tzn hii licha ya tabu zake ni nzuri mara mia kuliko nchi nyingi za Kiafrika .

Hiyo ndio sababu kuu ya wanigeria wengi kukimbia nchi yao , umaskini huko ni WA kutisha , serikali na watu hawaelewi washike wapi na waache wapi.
 
Back
Top Bottom