KERO Maisha ya wanafunzi shule ya Sekondari Lyamungo hatarini, shule haitoi huduma ya chakula cha jioni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

abuu_Ayman

New Member
Joined
Jul 25, 2026
Posts
2
Reaction score
0
Kama mzazi na ndugu wa baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari LYAMUNGO iliyopo Wilaya ya Hai, Kilimanjaro; tungeomba TAMISEMI na Wizara ya Elimu wawe wazi kuhusu maisha halisi katika baadhi ya shule ili wazazi wawe na uhuru wa kuchagua wapi kijana wao patamfaa kupata taaluma bila wasiwasi.

Huduma ya chakula shuleni hapo inatolewa mara mbili tu kwa siku; asubuhi ni uji (tunauelewa uji wa shule ulivyo) na alasiri ni chakula cha mchana. WANAFUNZI hawapatiwi chakula cha jioni shuleni hapo isipokuwa huduma hiyo hutolewa na kantini ya shule kwa kununua (kama huna pesa siyo shida zao).

Mazingira kama haya ni hatarishi kwa hawa watoto, hasa kama nyumbani kwenu mambo siyo mazuri. Chakula ni miongoni mwa mahitaji ya lazima na muhimu.

Tusiwatafutie watoto vidonda vya tumbo vya lazima jamani. Tuwaeleze wazazi uhalisia kuwa shule haina chakula cha kutosha kulisha milo mitatu kwa siku ili wajue watakavyoweza kuhakikisha watoto wao wanakuwa well fed muda wote wanapokuwa shuleni hapo.

Kwenu,

#TAMISEMI na Wizara ya Elimu
 
Kwanini milo miwili? Kwa lyamungo je shule zingine vipi? Wanakula milo miatatu?
 
Imekuwaje?hiyo wa.kulaumiwa nimwalimu mkuu,muongozo ni milo mitatu na wizara inatoa pesa zote kwa ajili ya milo mitatu na hesabu ni robo kwa kila mlo wa mwanafunzi aulizwe mwalimu mkuu
 
Sizani kama hii jambo linaukweli.!
Halafu mnasubiri nini kugoma mpaka mlete ili swala Jf??
Mbona nyie madogo wa elfu 2 walaini laini sana???
 
sawa Mimi Nchimbi nimekusikia..

Nendeni mkapiganie chakula chenu
 
Kama mzazi na ndugu wa baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari LYAMUNGO iliyopo Wilaya ya Hai, Kilimanjaro; tungeomba TAMISEMI na Wizara ya Elimu wawe wazi kuhusu maisha halisi katika baadhi ya shule ili wazazi wawe na uhuru wa kuchagua wapi kijana wao patamfaa kupata taaluma bila wasiwasi.

Huduma ya chakula shuleni hapo inatolewa mara mbili tu kwa siku; asubuhi ni uji (tunauelewa uji wa shule ulivyo) na alasiri ni chakula cha mchana. WANAFUNZI hawapatiwi chakula cha jioni shuleni hapo isipokuwa huduma hiyo hutolewa na kantini ya shule kwa kununua (kama huna pesa siyo shida zao).

Mazingira kama haya ni hatarishi kwa hawa watoto, hasa kama nyumbani kwenu mambo siyo mazuri. Chakula ni miongoni mwa mahitaji ya lazima na muhimu.

Tusiwatafutie watoto vidonda vya tumbo vya lazima jamani. Tuwaeleze wazazi uhalisia kuwa shule haina chakula cha kutosha kulisha milo mitatu kwa siku ili wajue watakavyoweza kuhakikisha watoto wao wanakuwa well fed muda wote wanapokuwa shuleni hapo.

Kwenu,

#TAMISEMI na Wizara ya Elimu

hii kauli sioni ikiwa na uhalisia
Inawezekana ni mwanafunzi amemdanganya mzazi ili apatiwe hela ya kutumbua...
Mzazi jiongeze kwa kufanya mawasiliano na shule moja kwa moja...
 
Back
Top Bottom