Maisha ya wasanii hawa baada ya kujitenga na clouds media...

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Nimekaa nikiwaza yani msanii akigombana na clouds kwanini inakua ngumu sana kusimama tena kimuziki? angalia

Jay dee karudi na ndindindi katamba kidogo tu kaja na ngoma yake mpya jiiiiiii imebuma haskiki tena.na ameanza kusahaulika tena

Wagosi wa kaya wakina mkoloni chaaliiiii

Mapacha nao hamna kitu kaaabisaaaaa

Dudu baya nae kuleee

Dan Msimamo kapuni

Rama D kajaribu kufulukuta wapiii

Rubby hata wimbo wake mpya haujulikani tu

Hawa jamaa wana hila gani wanafanya? daah kazi kweli kweli kwa mtindo huu wasanii acha waendelee kua watumwa tu maana njaa haina adabu......ila Ruge na wewe malipo ni hapa hapa duniani japokua mi siichukii clouds maana ndo Radio station bora kwa sasa Tanzania.
 
Umemtaja rama dee au sijaona vizuri..!we hufatilii mziki rama dee ameshinda had tuzo ya kili na wimbo wake wa subira na ngoma hazichezwi clounds ile power yao ya zaman kwa sasa imeshuka sana kina man fongo wamtolewa EFM zaman isingekuwa rahisi
 
Ukiangalia wote uliowataja hawabadiliki kimelody , sauti aliotoa wimbo wa kwanza ndio hiyo hiyo anaitumia nyimbo nyingine zifuatazo , anachokifanya ni kubadilisha mashairi tuu,kama wewe unafahamu vizuri muziki ona tune za dadu bovu anajiongelesha tuu na kuimba off key, kadhalika mabasi ya kale staili ya kufoka foka tuu haina nafasi kwa sasa , huyu land jaida yeye anachokua mamelody ya nyimbo za asili za kijita na kuweka maneno sio zote zinavutia. Kifupi mtamlaumu huyo mawingo lakini issue ni kwa wasanii wenyewe hawasomi alama za nyakati
 
Lady jay dee ana fanya vizuri na rama d

Ujue dhana ya nyimbo kuto skika ipo kwa wasanii wengi, mbona juzi hapa kiba na da prince wametoa wimbo mbaya hata hakuna aliye ujali!!

*wasanii wanavo pigana kujipatia maslahi mashabiki tusi waangushe mimi namsapoti yeyote anaye pinga unyonyaji wa cloudz na hata akitangaza show huwa naenda kwa kuwa najua mabadiliko yanaanza na mimi
Tupinge unyonyaji inawezekana
 
Bongofleva haiwezi kusogea mbele kama kunakuwa na migogoro katika ya media na wasanii. Wasanii wetu hawawezi kufika kimataifa
 
Jamani nielewesheni kidogo hapo,ukisema MAPACHA ni mapacha watatu akina khalid chokoraa na jose mara au ni mapacha gani?..
 
Mtoa mada kuna kitu hujakijua,mziki ni utoto tuu mtu akikua anafanya dili zinzzoendana na umri wake,masuala ya kugombania mic na watoto inakua sio poa,hao unaowataja karibia wote ni wakongwe naw wanafanya maisha mengine au wanaimba kwa prestige tuu,hali kadharika mashabiki,wale waliokuwa wanasikiliza bongoflava miaka ya 2000 hawawezi wakawa inspired na msanii aliyetoka miaka ya 2015
 
Rama dee na clouds waligombana nn ila Rama dee mpk leo anaendelea vzr napenda nyimbo zake mbili huwezi na jide na kuwa na subira ft mapacha
Hata mimi rama d kila akitoa nyimbo naziskia na znakuwa poa tuu
 
We utakua dada millarday tu sio bure,nani anasikiliza hiyo redio?na inaonekana we hujui mziki unalazimisha kuujua,yaani JD unasema hasikiki?rama d? we hamnazo aisee
 
Ujinga mtupu,wasanii wote waliovuma zamani hawasikiki saivi,sio kwa sababu hawapatani na kilauzi,ila ni sababu muda wao umeisha.Kwani wasanii wanaojipendekeza kwa kilauzi wale wa zamani wako wapi? Mr nice amegombana na kilauzi chenu? ,afande Sele je,O ten,Inspekta Haruni? Wapi Kr,Y dash,Snare,Sister P,Zay B,J.I,AT.........CLOuDS SIO MUNGU,hawawezi kumshusha mtu,na hata wakiweza kumpandisha kama ni Bomu atashuka kwa hiari yake.Mfano Ally nipishe,Amini,Marlaw n.k n.k.
 
Umemtaja rama dee au sijaona vizuri..!we hufatilii mziki rama dee ameshinda had tuzo ya kili na wimbo wake wa subira na ngoma hazichezwi clounds ile power yao ya zaman kwa sasa imeshuka sana kina man fongo wamtolewa EFM zaman isingekuwa rahisi
Mkuu hupo sahihi Clouds bado wana nguvu ndio maana huyo Man fongo kakimbilia Clouds kupitia Fiesta ili abunye..E Fm wanajitahidi ila bado kwa sababu wanasikika mikoa michache ukilinganisha na Mawingu fm
 
Rama dee???! Aaah hili dubwana liache mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…