Maisha ya Zanzibar yapoje? Nataka kwenda kutafuta ridhiki

Maisha ya Zanzibar yapoje? Nataka kwenda kutafuta ridhiki

Status
Not open for further replies.

Gemini_man

Member
Joined
May 15, 2023
Posts
17
Reaction score
44
Habari za mihangaiko wanajamii,

Hivi karibuni nafikiria kwenda Zanzibar kwaajili ya kuanza Maisha, pamoja na kutafuta kazi huko hasa zinazohusu tourism and hospitality.

Kwa wenyeji na wazoefu wa Maisha ya Zanzibar Je, Maisha ya utafutaji yapo vipi huko (ugumu na wepesi wa kupata kazi)?

Gharama za maisha (chakula na kodi ya chumba) zinakutaka walau uwe na kiasi gani cha fedha kwa mwezi?

1688509709327.png

​
 
Habari za mihangaiko wanajamii,
Hivi karibuni nafikiria kwenda zanzibar kwaajili ya kuanza Maisha, pamoja na kutafuta kazi huko hasa zinazohusu tourism and hospitality,
Kwa wenyeji na wzoefu wa Maisha ya Zanzibar,
Je Maisha ya utafutaji yapo vipi huko (ugumu na wepesi wa kupata kazi) ?
Gharama za maisha (chalupa na kodi ya chumba) zinakutaka walau uwe na kiasi gani cha fedha kwa mwezi.?
Usipende kuhadithiwa ingia field uyaone mwenyewe maana mengine hata ukiambiwa hutoamini mpaka uyaone kwa macho.

Karibu Zanzibar mkuu
 
Hapa Tanzania. Hakuna Sehemu nzuri Kama Zanzibar katika utafutaji na kutoboa Maisha watu wakarimu hamna rate kubwa ya umasikini ni Akili zako na kumuomba Mungu akuvushe kila hatua dua
Mleta mada naomba uchukue huu ushauri asikufiche mtu ukijiheshimu zanzibar unatoboa ww jitahidi upige kazi
 
Pesa ni rahisi sana kupata Zanzibar kuliko huku kwetu.
Na kuhusu kazi wanatabia flani ya ubaguzi kwa mtu alietokea Bara wanapaita, lakini Kama utakua refferd katika ofisi na mtu kazi unapata tu bila shaka.
Kuhusu Kodi na misosi sio bei sana na inatofautiana na misimu tu.
Kama unajua lugha za kigeni vizuri na una mtaji wako unaweza anzisha kampuni yako ya utali.
 
Asante sana kwa mwongozo wako ndugu
 
Unaijua Zanzibar gani mwenzetu!! eti chakula sio bei chakula gani hicho urojo ama. Zanzibar hapafai wabaguzi sana kuanzia kuingia mpaka kutoka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom