Maisha yakiwa rahisi sana hugeuka kero

Maisha yakiwa rahisi sana hugeuka kero

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Mtu ambaye hafanyi kazi yoyote,hafanyi usafi, lakini anapata mahitaji yake yote bure lazima ataanza kulala sana,kukesha kwenye tv,kuanza kunywa pombe,kucheza kamari,kutumia dawa za kulevya,kufanya starehe sana muda wote kwa sababu anakuwa anaishi maisha rahisi sana hivyo atalazimika kuishia maisha ya anasa na starehe kwa sababu hana kazi yoyote ya kufanya

Mwanamke huwa anapoteza hisia za mapenzi pale ambapo hana kazi yoyote ya kufanya kwa mwanaume wake.

mwanaume mstaarabu hana usumbufu wowote wakati mwanaume mlevi kupindukia, mcheza kamari, mhalifu, mwizi, msaliti wa mara kwa mara huwa anampa Mwanamke hekaheka zenye kumfanya Mwanamke kufanya uwekezaji mkubwa sana wa hisia wakati wa kutaka kumbadilisha tabia mwanaume wake.

Mwanamke anapofanya uwekezaji mkubwa sana iwe wa fedha,muda ,hisia ,kutaka kumbadilisha tabia mwanaume husababisha Mwanamke anakuwa na hisia kali sana za mapenzi kwa mwanaume huyo.

Mwanamke huwa mwenye kuthamini sana jasho lake tu.

Hivyo ikiwa Mwanamke amempata mwanaume mkamilifu bure bila kuvuja jasho hata kidogo lazima atamchoka mwanaume huyo haraka.

Mwanaume mwema sana huwa anaonekana kero kwa sababu anaomba msamaha haraka hata kama hajafanya makosa,anasamehe haraka jambo ambalo husababisha hasira kwa Mwanamke,huwa anakubaliana na mawazo ya Mwanamke saa 24 hivyo mwanamke anajiona ni kichwa cha familia hivyo anaona kero.

huwa anambembeleza mwanamke mara kwa mara jambo ambalo husababisha Mwanamke anakuwa hana kazi yoyote ya kufanya ili kuonyesha shukurani kwa mwanaume.

Mwanaume anapokuwa mwema sana kwa Mwanamke ndipo anapoteza mvuto kwa mwanamke huyo.

Mwanaume mwema sana ni tambara la deki kwa kila Mwanamke alieumizwa sana kwenye mapenzi kisha hugeuka daraja la kumrejesha kwa ex wake kisha akiumizwa tena anarudi kwa mwanaume mwema ili kupata faraja kabla ya kurejea tena kwa Ex wake ambaye hana malengo naye.
 
Mimi Kama raisi wa ma jobless pro max, naomba mtu pumzishe wakuu.

maana kila mfano mna tutumia sisi Kama case study.
wasemeni basi hawa majamaa😃.
FB_IMG_17362527162075074.jpg
 
Back
Top Bottom