Usisahau hakuna mtu utampata perfect Mswati..!
Carleen;
Unajua hapo juu nilikuwa ninawaweka sawa lkn bado sijatoa mtazamo wangu katika mapenzi.
Ukweli ni kwamba hautapata mtu sahihi wala mkamilifu.
Mpenzi bora hutengenezwa
Mke bora hutengenezwa na mme wake
Mme bora hutengenezwa na mke wake.
Mimi mwanzo wa maisha yangu kitaa.
Niliwahi kuajiriwa na boss mmoja alikuwa mkubwa flani katika taasisi maarufu ya mke wa namba moja Tz.
Alinifunza kitu.
Walikutana na mme wakiwa kapuku skwea.
Walipanga chumba kibovu na hawakuwa hata na gororo walikuwa wakilalia box yaani makasha ya vifungashio.
Mke ndiye alikuwa mfariji mkuu na mtia moyo mkuu.
Kuna wakati wakati Mungu akawaonekania.
My dear kwasasa ni miongoni mwa wabarikiwa hatari.
Ndoa yao ni bora hatari.
Nini nataka kusema; kutafuta mwenza hasa kwa wasichana wa siku hizi ni changamoto.
Mnasngalia ana future?
Bila kujua future bora mtaitengeneza wawili na hii ndio itakuwa ndoa bora.
Wanaume nao macho juu..wanasska Salha type..mwishowe mkaa na bunduki zinahusika.
Buddy... mme wako ni jamaa flani kitaa hana nyuma wala mbele but anakusubiri wewe mke bora ukamfinyange.
Kadhalika wanaume....mkeo ni kadada flani shape less super flat screen flan, inakusubiri ukailishe iote hips ipendendeze.
Ukaipige sopu sopu ing'ae hakika umepewa na Mungu...itakuheshimu na kukufanya mume boraa aaah
Carleen
financial services
Darlin