Maisha yamekuwa magumu sana awamu hii

Sema wewe huna pesa si watu hawana pesa.
 
Kwa fursa zilizopo Tanzania kama huzioni basi utaishi kwa shida sana. Tanzania ni kati ya nchi chache zenye fursa lukuki unaanza biashara kwa mtaji mdogo ndani ya miaka kumi unakuwa milionea. Tatizo kubwa kwa watanzania walio wengi hamtaki kubadilika kutokana na wakati uliopo mumekalia kulialia tu maisha magumu hamtaki kushirikisha ubongo.
 

Dude, persevere or perish! ...Hii ndiyo shida ya kuishi kwa mazoea; new business or life environment requires new strategies! Crybabyish attitude is no strategy.
 
Kwahiyo ukiona mpangaji kabadilika maana yake mtu kafirisika? Ulivyoona nyumba inauzwa ukajua mwenyewe kashindwa kurejesha mkopo wa bank au? Mbowe mwaka huu kazi anayo sio ujinga wa wafuasi wake huu
 
Kwahiyo ukiona mpangaji kabadilika maana yake mtu kafirisika? Ulivyoona nyumba inauzwa ukajua mwenyewe kashindwa kurejesha mkopo wa bank au? Mbowe mwaka huu kazi anayo sio ujinga wa wafuasi wake huu
Ukiwa na Akili ndogo unadhani unaweza kuelewa kilichopo!!? Endelea kukaa kwa shemeji yako.
 
Alinipa ujasiri wa kupambana na maisha sasa hivi ubao umegeuka ananibembeleza turudiane nikawambia tubaki wazazi tu mambo mengine kila mtu apambane kivyake, natamani kuandika mwendelezo ttzo mwandiko wangu hua una utata sijui kupangilia paragraph kabisa mtu aelewe. Ila inshort muda ni mwalimu mzuri sana
We bullar yule mke wako mlisharudiana au mliishia wap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uchunguzi wangu usio rasmi bishara zote ambazo hazikuwa na mkakati wa 5/10 years na zimekuwa zikiendeshwa kwa mipango ya muda mfupi huku zikitegemea kudra za Mwenyezi Mungu zinapata msukosuko sana kipindi hiki.
Mzunguko wa hela kwenye sekta zisizo rasmi umekuwa mdogo sana na mahitaji yameongezeka.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Duh pole Sana kila mtu ana majanga yake haki,
Sasa ulishaoa?
 
anaebisha maisha sio magum ni mpuuzi, biashara sahivi haziendi yani ni tofauti na mwaka 2015, juzi nimekaa nanyoa nikawa namhoji kinyozi vipi maisha yanaendaje, ndo kwanza linafurahia eti uncle magu kasaidia siku hizi watu hawana dharau kama enzi za jk, sa nkamuuliza wateja kipind cha jk na sahivi wapi wengi, akasema jk, sasa namuuliza watu kutokua na dharau imesaidiaje life lako? Kimya, ndo nkaamini wengi wanaoshabikia ccm ni wanafki na wachawi, ni kama tu man u icheze na team kwny danger zone af ushangilie tim iyo, huo ni uchawi inshort, stupid !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo yamebadilika sana, kwa waliosoma Uchumi wanajua Duniani kote Government ndio inatakiwa iwe big spender ili fedha ziweze kuonekana kwa wanachi. Serikali yetu inakusanya hela nyingi sana na matumizi utasikia imelipa kampuni flani kutoka nje ijenge kitu flani. Mzunguko wa pesa unazidi kupungua kadri siku zinavoenda
TRA na polisi wamekua wakusanyaji wakubwa wa mapato
Serikali inatoa ajira kwa nadra
Wahitimu wengi wa chuo ndoto zao zimezimwa
Mtaani hakuahikiki mpaka baba zetu wanabeti
Vitu vinapanda bei mishahara iko pale pale

Ukijumlisha pesa zilizoenda nje
Ndege, 10% deposit ya Stiglers Gorge, SGR, Ubungo Interchange pesa zilizobaki haziwezi kuonekana kwenye mzunguko
 
Wanasema fanyeni kazi acheni kulalamika
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha! Nmecheka kama zuzu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…