Maisha yamekuwa magumu sana awamu hii

Maisha yamekuwa magumu sana awamu hii

Siamini kuwa wanaolalamika kuwa maisha ni magumu wote walikuwa mafisadi.

Hembu tulete ushuhuda kama wewe
- Mfanyakazi
- Mkulima
- Muuza hoteli
- Muuza nguo
- Muuza genge Nk.

Tunaomba viongozi waweze kuchukua hatua hali mtaani ni worse.

Ushuhuda:
Nina kakibanda ulipaji wa kodi ni tabu mno kila siku wapangaji wanadai hawapati hela hivyo niwavumilie.
Ujamaa and dictatorship philosophy " wafanye wawe masikini ili uweze kuwatawala wanyime elimu, wabane kwenye kodi wasifirikirie zaidi ya kula tu.
 
Hizi ni akili za fukara sio masikini. Na pili sijui kama hata shule ulienda, kama ulienda ulienda kukua mpk kidato cha nne ulipo feli ukaanza kuganga umasikini.

Kuna uhusiano mkubwa wa pesa kuwa katika mzunguko na kilio kilichopo mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app

sasa kama kwa mwezi unalipwa kile kile au zaidii maisha yanakuaje magumu? mtaani inflation sio kama zimbabwe useme kua mkate utauzwa trillion moja the next morning, kiuhalisia mnacholalamika hakina mashiko! mm naona tu watu bado wanadunda na ndinga kali na wanaendelea kua matajiri
 
Pesa ipo nyingi tu, tena hata wengine wanaichezea.

Juzi nilisikia kwenye redio moja eti kuna kampuni moja huko Dar imeitisha Watu wapigwe picha wapewe elfu tano nasikia Mji mzima wakahamia hapo...sasa uliona wapi pesa inatolewa kimchezo hivyo kama sio pesa kuchezewa?

Na ili iwe fundisho hii Kampuni ilazimishwe izunguke mikoa yote ili isionekane kama Dar inapendelewa.
una umri gani? kama una umri chini ya miaka 10 nitakusamehe kukudharau ila kama upo above 10 na unaonge fact kama hii, wewe ni masikini wa fikra
 
Kwa fursa zilizopo Tanzania kama huzioni basi utaishi kwa shida sana. Tanzania ni kati ya nchi chache zenye fursa lukuki unaanza biashara kwa mtaji mdogo ndani ya miaka kumi unakuwa milionea. Tatizo kubwa kwa watanzania walio wengi hamtaki kubadilika kutokana na wakati uliopo mumekalia kulialia tu maisha magumu hamtaki kushirikisha ubongo.
Hata kama unafanya kitu ila haimaanishi kuwa hakuna utofauti wa awamu hii na awamu iliyopita,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wengi wana fikra za kimasikini huwezi ukasema maisha mugumu kwenye nchi yenye soko la watu zaidi ya milioni 55 na ardhi ya kilimo ya kutosha tena yenye rutuba na upatikanaji wake ni rahisi. Tatizo watu wengi mnataka mpate pesa bila kujishughulisha. Watu hawataki kubadilika kutokana na wakati. Watu wanatoka Kenya kuja kulima miti ya mbao na parachichi Tanzania sisi tupo tu tunasema maisha magumu. Kwa sasa mnasema nyanya moja shilingi 500, kupanga ni kuchagua wewe uliwekeza kununua iPhone Mimi niliwekeza kwenye kilimo cha nyanya matokeo yake ndiyo hayo, hivyo hutakiwa kulalamikia bei ya nyanya nakusema maisha magumu.
Acha kupotosha kijana kilimo Tanzania tena cha miti utavuna lini Mkuu?
Hivi mfu anayelima tangu enzi za babu zetu kwa jemba la mkono atatoboa linj?
Mvua ikikatika asilimia kubwa ya wananchi wanaotegeme kilimo nijobless tu CCM nahaadi za kuanzisha kilimo cha umwagiliaji wameshindwa hata kutekeleza

Tanzania ya viwanda iko wapi base yake ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom