Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chase Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo

Pole sana kijana mwenzangu,kaa chini fikiria cha kufanya baada ya kuuza iyo gari,ukiuza gari angalia cha kununua kulingana na hela utakayopata kama ni pikipiki sawa na kama kwa bajaj sawa
 
Watu sik hzi wanakula mlo moja au mili tena miogo na pilipili na samaki wa 100 au kahawa na ndizi
 
Tatizo mnang'ang'ania mjini wakati huku shambani vyakula tele, njoo huku ipalamwa nikupe shamaba la buree ulime upate mahitaji yako,
 
Leo mbona hujatukumbusha tuwe wazalendo?
 
Kwa kutumia GX100 kama Taxi lazima maisha yawe magumu. Hujiulizi kwanini wenzio wanatumia IST, Raum, Vitz?
Hao wenye IST, Raum na Vitz maisha pia magumu kwao kwa maana mchawi ni Bajaj na sio ukubwa wa engine ya gari.
 
Hao wenye IST, Raum na Vitz maisha pia magumu kwao kwa maana mchawi ni Bajaj na sio ukubwa wa engine ya gari.
Kwasababu unaamini Bajaj ndio mchawi wako subiri ziishe au na wewe nunua Bajaj.
Siku moja nilipanda Taxi na jirani kulikuwa na Bajaj na bodaboda. Nikamuuliza Yule dereva wa taxi biashara vipi naona hapa mna ushindani na Bajaj na bodaboda.
Akaniambia kuna abiria wa Bajaj,wa bodaboda na wa taxi. Akaniuliza mbona wewe umeacha bajaj na bodaboda umekuja kuchukua taxi?
Kila mtu na abiria wake, jipange mdogo wangu shida inaweza kuwa wewe tukianza na gari unayotumia kufanya taxi.
 
Biashara ni uvumilivu kadri mda unavyoenda utapata wateja.
 
Umenena sahihi kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…