Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chase Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo

Naunga mkono hoja..nimefungua mgahawa una mwezi tu lakini naona matunda
 
Huu wimbo wa maisha magumu.naona unaanza kukolea[emoji16][emoji16][emoji16]
Toka zamani watu wanaimba wimbo wa Maisha Magumu,na hata wakati niko mdogo pia Wazazi wangu nao walikuwa wanaimba wimbo huohuo tunaoimba Sasa!! Alafu siyo kweli kila Mtu anaesema Maisha Magumu ni kweli ana Maisha Magumu, Wengine wafuata mkumbo tu lakini wako vizuri sana kimaisha!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hapa sijajua watu wanawazaga nini ila mimi niliwahi waza hili swali ..unajua milioni 7 ukitulia vizuri bila papara unaweza zalisha zaidi ya laki 1 kwa siku bila kuiriski.
yani ununue babaji milioni 7 ili dereva akuletee sijui 20,000 kwa siku mpaka upate faida cjui lini hapo una-assume haijaharibika ,haijakamtwa,hujaibia spare,haijapata ajali ,mwendo wa presure tu
 
Hapa sijajua watu wanawazaga nini ila mimi niliwahi waza hili swali ..unajua milioni 7 ukitulia vizuri bila papara unaweza zalisha zaidi ya laki 1 kwa siku bila kuiriski.
Fafanua kidogo kama hutojali mkuu.
 
Mawazo yako hayaendani iyo Gari ukiuza ni 2.-2.4Million labda ununue pikipiki sio Bajaji wala kufungua Pub. Huu ndio Ukweli au ninasema uongo ndugu zangu. Tupambane hata uku kwangu maisha ni magumu Sijawahi kuona toka nibalehe
 
Mimi mwaka huu nimefungua biashara mbili..moja ya taaluma yangu na moja ndo huo mgahawa.

Mgahawa frem,ukarabati,vifaa kama viti na meza,masufuria,sahani nk nimetumia 984k nimeajiri wafanyakazi wawili ila mmoja nina ukaribu nae sana...ukitoa matumizi yote kwa siku nabakia na faida isiyopungua 10k hapo sijaanza kuuza vinywaji,maji,maziwa,juice nk nina uza wali,ugali,supu pekee na pia sikai mwenyewe nikianza kuuza hivo vitu na mgahawa ukichangamka vizuri nadhani faida ya 30+ nitaipata.
Fafanua kidogo kama hutojali mkuu.
 
Kweli ndugu yangu yaani mimi ndo ugeni tu wa biashara na kwakua sikai mwenyewe na bado sina jina kubwa na changa ila kwa siku faida ya 10-20K sikosi na hapo nauza ugali,wali na supu pekee nikianza kuweka maji,juice,soda nk nitaingiza 30-50k kwa hela hiyo huku nikiwa muajiria mahala flani na nina kimaabara bubu maisha angalau yatanipa nafasi nipumue miaka 2 ijayo.
mimi nmemfungulia wife hiyo biashara, anaingiza mkwanja mrefu kwa siku kunizidi mimi niliyeajiriwa
 
Uza hiyo gari nunua bajaji uendeshe mwenyewe , achana na hayo mawazo ya pub
 
98K mtaji uwongo
 
mimi na mke wangu kupitia hiyo biashara tumeweza kununua kiwanja na kuhusu mimi kutoa pesa ya matumizi nyumbani sitoi kabisa.. mke anamaliza mambo yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…