Prof_Adventure_guide
JF-Expert Member
- Dec 21, 2023
- 533
- 1,499
Kila siku bei zinapanda. Mafuta yakipanda, nauli inapanda. Nauli ikipanda, chakula kinapanda. Chakula kikipanda, maisha yote yanakuwa magumu. Halafu ukiuliza sababu unaambiwa “kuna vita ya Iran na Israel.” Sawa, vita vinaweza kuathiri mafuta duniani, hilo kila mtu analijua. Lakini swali la msingi ni hili, kwa nini maumivu yake Tanzania yanakuwa makubwa kiasi hiki mpaka mwananchi wa kawaida ashindwe hata kuishi kwa amani?
Ukweli ambao watu wanaanza kuuelewa ni kwamba tatizo si vita pekee. Tatizo ni mfumo mzima wa uchumi ambao mzigo wake umebebeshwa kwa mwananchi wa kawaida. Kodi ziko kila sehemu. Mafuta yana kodi, miamala ina kodi, bidhaa zina kodi, biashara zina kodi. Lakini pamoja na kodi zote hizo, maisha yanazidi kuwa magumu kila mwaka. Vijana hawana kazi, biashara nyingi zinakufa kimya kimya, na mishahara mingi haiendani tena na gharama za maisha.
Wananchi wamechoka kusikia “uchumi unakua” wakati mfukoni hakuna dalili ya huo ukuaji. Uchumi wa kwenye ripoti sio maisha ya mtaani. Mtu hawezi kula statistics. Wananchi wanataka kuona matokeo halisi kwenye maisha yao, sio kusikia maneno mazuri kwenye majukwaa huku bei ya mafuta na chakula ikiendelea kupaa kila mwezi.
Tatizo kubwa zaidi ni viongozi wengi kuonekana kama hawaishi maisha ya wananchi wa kawaida. Wakati watu wanahangaika kupata hela ya kula na kulipa kodi, wengine wanaonekana busy na siasa, misafara, na hotuba nyingi kuliko kutafuta suluhisho la kweli la gharama za maisha. Ndiyo maana hasira za wananchi zinaongezeka kila siku, kwa sababu watu wanahisi hawasikilizwi tena.
Suluhisho sio propaganda wala maneno matamu ya kisiasa. Suluhisho ni kuwa na mfumo unaomlinda mwananchi wakati wa crisis. Serikali ikiona mafuta duniani yanapanda, inatakiwa kupunguza baadhi ya kodi ili wananchi wapumue. Pia matumizi yasiyo ya lazima yanapaswa kubanwa na fedha nyingi ziende kwenye uzalishaji, ajira, biashara ndogo na maisha ya watu wa kawaida.
Wananchi nao wanapaswa kuamka kiakili. Waache kuamini kila wanachoambiwa bila kuhoji. Kodi zao zina haki ya kuonekana zinawasaidia vipi. Kwa sababu ukweli ni huu, nchi haiumizwi tu na vita vya nje, mara nyingi inaumizwa zaidi na maamuzi mabovu ya ndani yanayomfanya mwananchi abebe mzigo wote peke yake.