Binti Sayuni03
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 1,075
- 1,913
Habarini za wakati huu wana jamii forums, ni matumaini yangu mu wazima, kwa wale wenye changamoto za kiafya Mungu awafanyie wepesi.
Kuna kisa kilitokea miaka kadhaa iliyopita, nimekikumbuka nimeona nishee hapa jukwaani.
Shule ya msingi niliyosoma, mwalimu wetu mkuu ndiyo alikuwa anatufundisha Hesabu I mean Hisabati kwa shule zetu za St. Kayumba sasa kutokana na walimu wakuu kuwa na majukumu mengi ilikuwa ngumu kwake kufundisha sawasawa na ratiba.
Nakumbuka tulikuwa wanafunzi karibia 183 wa darasa la 7, baada ya mtihani wa taifa tuliofaulu kwenda sekondari ilikuwa ni idadi ndogo ukilinganisha idadi ya waliofeli, hii haikuwa rekodi nzuri kabisa.
Kutokana na hii rekodi mbovu ya matokeo, yule mwalimu mkuu alishushwa cheo kutoka kuwa mwalimu mkuu hadi kuwa mwalimu wa kawaida, hii haikuwa kitu kizuri.
Sasa mimi ninapokaa ni karibu na shule ya msingi, huwa nikipita kila siku asubuhi kwenda kibaruani, huwa namuona sasa sijajua kama aliomba uhamisho kutokana na aibu ya kushushwa cheo au alipangiwa hii shule aliyopo sasa hivi.
Binafsi nimemuonea huruma sana mwalimu wangu mkuu wa shule ya Msingi, lakini nimejifunza kuwa unapokuwa juu usijisahau muda wowote unaweza kudondoka, hakikisha unafanya juhudi zitakazokuzuia ukidondoka usiumie.