Maisha yanaenda kasi sana. Ali Choki ndo yupo kule!

Maisha yanaenda kasi sana. Ali Choki ndo yupo kule!

yupo super kamanyola ya mwanza.......nafikiri wanaimba tu nyimbo zilizotamba zamani. nimemuona akikomalia kuiimba 'nawashukuru wazazi wangu' ya ddc mlimani park. najihisi kuhuzunika kiasi, lkn sijui ni kwanini!!
aysee juzi jmos nlikuwa pale villa park kirumba sikuamini kuwa Ali ndo anaimba live band akiwa kwny muonekano ule,jamaa kachoka saanaa mkuu
 
Ndugu zangu wana JF, anayopitia Ali Choki, na wengine ndio mfumo mzima wa Maisha ya watanzania. Wao wanajulikana na ndio maana tunawaona kirahisi walivyokuwa sasa tofauti na zamani

Tusiwabeze ndio mfumo ulivyo. Wazazi wetu sisi wengine walikuwa wakubwa serikalini lakini leo tunachangishana watoto kuwakatia Bima za Afya hawana uwezo tena na Maisha yamewapiga wanatutegemea sisi watoto wao. Tusipojipanga vyema na sisi tutakuwa hivyo hivyo tegemezi kwa watoto wetu. Wakati ni ukuta huwezi kubaki juu milele tecnolojia inabadilika na dunia inabadilika vizazi vinabadilika.

Kuna wengi upande wa wafanyakazi na wakulima, Mapedeshee ukiwaona wamefulia tofauti na kipindi cha nyuma

SOMO MUHIMU: Ukiwa juu jitahidi kuwekeza na kujijenga ili wakati unapobadilika ubaki kuwa juu au usitetereke sana
 
Bora Choki Ukimuona Muumin utamuonea Huruma kweli maisha yanaenda kasi sana...Kuna siku nilimuona kwenye Bajaji za kuchangia jero jero anaenda kunegotiate na manager wa BAR apige show siku ya valentine na siku nyingine tukapanda naye Mwendokasi aiseee yaani mpole anatia huruma.
Mwijuma Muumini anapatikana kwenye Mghahawa Bubu pale Mtoni Mtongani,anamsaidia Mmama kuuza chakula,ujira wake ukiwa ni kupewa msosi wa bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ach
Mapedeshee wengi waliokuwa wanaziwezisha hizi bendi wamepigwa pini na huu utawala wa jpm.unaweza kuhusisha na kufulia kwa wanamziki hawa


Sent from my iPhone using JamiiForums
Siyo kweli hata kidogo muziki wa dansi ulishakufa hata kabla utawala huu wa awamu ya tano haujafikiriwa hata kuwa mgombea urais
 
yupo super kamanyola ya mwanza.......nafikiri wanaimba tu nyimbo zilizotamba zamani. nimemuona akikomalia kuiimba 'nawashukuru wazazi wangu' ya ddc mlimani park. najihisi kuhuzunika kiasi, lkn sijui ni kwanini!!
Bongo hakujawahi kuwa na mziki wa dansi,hizo mambo tuwaachie wakongo wenyew hawa wa kwetu ni wapiga mayowe tu.
 
Back
Top Bottom