Maisha yanaenda kasi sana. Ali Choki ndo yupo kule!

Maisha yanaenda kasi sana. Ali Choki ndo yupo kule!

Mmenikumbusha mbali enzi ya Muumini, na nyimbo zake zile Mgumba namba 1, namba 2 na mgumba namba 3,
Napenda sana ule wimbo wa Muumini wa 'Nampenda Nani ' kuna maneno anasema "ukimuona mzuri mchaguee " "nampenda mpenda naanii nampendaa "

Ali choki na extra bongo, Ali choki na nyimbo ya 'chuki binafsi ' ,'umbea hauna posho '
Akudo wazee wa 'pekecha pekecha '
Nyoshi saadat huwa anapigaga Show tegeta Kwenye bar moja inaitwa Brazil.

Hadija mnoga, Sada saleh,
 
yupo super kamanyola ya mwanza.......nafikiri wanaimba tu nyimbo zilizotamba zamani. nimemuona akikomalia kuiimba 'nawashukuru wazazi wangu' ya ddc mlimani park. najihisi kuhuzunika kiasi, lkn sijui ni kwanini!!
Sawa

Nicheke tu
 
ahsante ndugu. ni ujumbe murua kabisa......
tatizo sisi binadamu ni wepesi sana kusahau na kupuuzia mambo, hata hao kina choki na muumini walipokuwa juu nadhani mifano ya wakongwe wa zamani waliotamba ambao sasa ndo hizo nyimbo zao wanaziimba walikuiwa nayo lakini hawakutilia maanani.
kuna makumi ya wastaafu, wa kitambo kama hao unaowasema na wengine wa miaka hii hii ya juzi tu (2015 kuja juu), ambao tayari wameshapoteza dira ikiwemo hata kushindwa kumalizia nyumba walizoanza kuzijenga baada ya kustaafu na kutokuwa au kushindwa kuendeleza mradi.....bado unawaona vijana wakishindwa kuona na kujifunza, wanaponda tu maisha!!
Hakika mkuu [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Ndugu zangu wana JF, anayopitia Ali Choki, na wengine ndio mfumo mzima wa Maisha ya watanzania. Wao wanajulikana na ndio maana tunawaona kirahisi walivyokuwa sasa tofauti na zamani

Tusiwabeze ndio mfumo ulivyo. Wazazi wetu sisi wengine walikuwa wakubwa serikalini lakini leo tunachangishana watoto kuwakatia Bima za Afya hawana uwezo tena na Maisha yamewapiga wanatutegemea sisi watoto wao. Tusipojipanga vyema na sisi tutakuwa hivyo hivyo tegemezi kwa watoto wetu. Wakati ni ukuta huwezi kubaki juu milele tecnolojia inabadilika na dunia inabadilika vizazi vinabadilika.

Kuna wengi upande wa wafanyakazi na wakulima, Mapedeshee ukiwaona wamefulia tofauti na kipindi cha nyuma

SOMO MUHIMU: Ukiwa juu jitahidi kuwekeza na kujijenga ili wakati unapobadilika ubaki kuwa juu au usitetereke sana
Funzadume,

Umeandika 100/100. Ni kweli hili ulisemalo. Mfano mimi mzazi wangu wa kiume. Miaka kenda nyuma CO wa kambi ya jeshi, mjuvi wa fani aina 3 za engineering na tegemeo jeshini na mbabe yeye. Leo ukimuona anatia huruma ujanja kwisha. Na mbaya zaidi alitumia na akafuja. Leo si yule..hata ujenzi alisahau. Anaishi nyumba ya rafiki.
 
"Jirani jirani yangu, nimekukosea nini * kila unachokitaka jirani, mimi ninakupatia * mimi ninachokuomba jirani, mwenzangu wanikatalia*" - Twanga pepeta (Ally Choki)
Huu wimbo ulisababisha nimle jirani yangu kimasihara [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]

cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
 
Nakumbuka siku moja pale Mango Garden vijana kabla haijavunjwa walikuwepo Malaika Band chini ya Mzee wa Masauti wanaburudisha alikuja Msafiri Diouf kupiga mzinga wa buku 2 huku akijitambulisha mie ndio Msafiri Diouf naomba niwezeshe buku 2 angalua niweze kula.
Dah haya maisha noma sana.
Tatizo wasanii wanafanya starehe sana bila kujua future yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Msafiri Diof aliLost kitambo kabla ya hata mziki wa dansi baada ya kuanza kutumia ngada.wawezeshaji wa mziki wa dansi kina papa Msofe,Said Ntimizi,Abdul Karim,Fikiri Madinda,Juma Kapuya.nk baada ya kupotea na mziki ukapotea!
 
Dansi zama zake zishaisha.

Mwenyewe leo nilikuwa nasafiri kutoka Ushirombo kwenda Mwanza, Jamaa wamepiga sana nyimbo za akila Msondo ngoma, Akudo impact na bend nyingi tu. Japo mimi sio mhenga ila nimepatwa maswali kwanini huo mziki zama hizi umepoa sana hasa hasa Bongo ?? Lakini kwa wakongo naona bado unapigwa pigwa


Happy dude [emoji67]‍[emoji538]
 
yupo super kamanyola ya mwanza.......nafikiri wanaimba tu nyimbo zilizotamba zamani. nimemuona akikomalia kuiimba 'nawashukuru wazazi wangu' ya ddc mlimani park. najihisi kuhuzunika kiasi, lkn sijui ni kwanini!!
yaaah, jana alikuwa antumbuiza pale Villa Park
 
Khadija kimobitel na Bad Bakule mwaka 2018,walikuwa wanapiga show bar ya TOT Tabata,kila Jmosi kiingilio kinywaji.Weekend nikiwa naandalia EPL nasindikizwa na burudani kutoka kwao.

Ali Choki aka mzee wa Farasi enzi zake alikuwa hatari.Sijui super Nyamwela na super Danger wapo wapi nao.Nakumbuka kipindi cha nyuma nipo Manyanya kituoni,nilimuona Nyamwela anashuka kwenye gari na demu mkali kinyama.
Enzi hizo kuna mpaka viatu fulani hivi vya kuchomeka miguu viliitwa Ally Choki..Kweli zama zinapita.
 
Nakumbuka siku moja pale Mango Garden vijana kabla haijavunjwa walikuwepo Malaika Band chini ya Mzee wa Masauti wanaburudisha alikuja Msafiri Diouf kupiga mzinga wa buku 2 huku akijitambulisha mie ndio Msafiri Diouf naomba niwezeshe buku 2 angalua niweze kula.
Dah haya maisha noma sana.
Tatizo wasanii wanafanya starehe sana bila kujua future yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yahaya Mkango naye sijui yuko wapi? Alikuwa anacharaza gita hapo Twanga , nakumbuka alikuwa anakuja sana Mwananyamala Mchangani kwa demu wake Hidaya. Wakati huo Twanga Twanga kweli.. .Kabla ya Banza kuondoka na mara baada ya Banza kuondoka na Ally Choki kudhibiti dimba.
 
Yahaya Mkango naye sijui yuko wapi? Alikuwa anacharaza gita hapo Twanga , nakumbuka alikuwa anakuja sana Mwananyamala Mchangani kwa demu wake Hidaya. Wakati huo Twanga Twanga kweli.. .Kabla ya Banza kuondoka na mara baada ya Banza kuondoka na Ally Choki kudhibiti dimba.
Hivi kati na banza stone na Ally choki nani alikuwa ni nan enzi zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom