Maisha yanahitaji uwe karibu na watu na kujuana. Tabia za kuogopa kuchangamana na kujitenga tenga zinachangia sana umasikini

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Na si mara ya kwanza unaskia mtu anasema mimi sitaki mazoea na watu.

Mimi sitaki marafiki.

Mtoto wangu ni geti kali, sitaki hata marafiki zake waje.

Niseme tu ya kwamba tabia hizi huwa zinachangia sana umasikini, Ni nani asiejua kwamba binadamu hawaaminiki ? lakini jibu ni kuwakwepa ? NO!

Binadamu ndio wanatuzunguka ni vema kujua kuishi nao kwa tahadhari kuliko kuwakwepa. Watu wabaya wajue ila ishi nao kwa mipaka, Watu wazuri nao ishi nao kwa tahadhari.

hata polisi hawa wanaoonea raia kuna kipindi wanaweza kukusaidia na hata kwa watu wa karibu jifunze kuishi nao kwa tahadhari huku amani ikitawala.
 
Wabaya na wazuri wote ni funzo katika maisha, tusikimbiane tuishi humohumo
 
Tatizo ni kuwa unajichanganya na watu ambao ..

Ukipata tatizo wanafurahi ..

Ukikosa pesa hawana cha kukusaidia ...

Maneno na majungu ndio kazi yao kijiweni ...

Kutwa kufuatilia familia yako ,mkeo ,umekulia nin ,umeshindia nin ,kila siku hubadili nguo ,kazin kwako ni wapi ,...maneno ,majungu ,uchawi ,kisengenyana ...


Kiufupi wanataka wakujue kiundani ili wakudharau zaidi wakuone kama takataka mtaani ...au wakuheshimu na kukupa kipaombele kwenye maisha yao ...baada ya kuona unapesa au unafanya kazi sehemu nyeti ya serikali ......


Mim siwezi weka ukaribu na watu wengi ,never ever .........

Hao naowaweka karibu ndio maadui wangu wakubwa wa badae ,ndio wanaweza niua ndani ya dakika Moja....
 
Kujichanganya na watu au kujitenga hyo ni asili ya mtu. Mfano mm sometimes napenda nijichanganye kwny kundi la watu nipige story, nichangie maada fulan lakn mara gafla nafeel bored kua pale au najkuta nakaa kmya yaan gafla tu sjiskii kuongea wala kuendelea kuwa pale kundini!!!!!!

Hali hii inanicost kwa sababu inanikosesha raman za kupata hela!!
 
Hela gani hizo watu watumie Kama daraja na uwageuze ndo daraja lako la kufanikiwa na sio kutwa kukaa nao
 
Katika Maisha ya kila siku tunayoishi tunakutana na watu wema pia tunakutana na watu wabaya

Iwe mahala pa kazi iwe nyumbani ama ofisini tunakutana na hzo mambo ,kuna mambo yanayotutokea au yanawatokea watu kusudi tujifunze kwa hayo mazur yao au mabaya yao uwezi kuepuka hilo
Cha msingi ni kuwa na tahadhari
Kuna mtu mbaya anaweza kuja kwako na kupitia huo ubaya wake likatokea jema kwako
Kwa hyo tusiogopane sana cha msingi tukae kwa tahadhari
 
Hata ukiwa na duka utahitaji watu ili uwaite wateja kujitenga unakosa mengi ni sawa na kujitengenezea kisiwa chako peke yako
 
Kupata Mafanikio ni Akili yako Wala hauitaji kuwa unachanganya na watu

Binafsi nachojua kufanikiwa kwa Mtu ni mchakato wa kiakili
Huwezi pata mafanikio bila watu,yawe mafanikio ya kisiasa,kiuchumi,kijamii au ki vyovyote vile lazima uchangamane na watu-hata ungekuwa na akili zaidi ya akina Nikola Tesla lazima uchangamane na watu.
Matajiri wote wakubwa,wanasayansi,wafanyabiashara,wanasiasa wote wamefika katika mafanikio hayo kwa migongo ya wengine.Watu huishi kwa kutegemeana huwezi kukamilisha kila kitu peke yako.
 
Hujaelewa nachomaanisha Mimi nachojua huwezi kutoboa Maisha bila watu kinachompa Mtu Mafanikio ni Akili yake na sio kuzungukwa na watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…