Mimi naona kama ni agizo la rais, maana alisema kila kitu kitapanda bei.
Rais hakusema vipi serikali ingefanya vitu vikipanda maisha yasiwe mgumu sana kwa wananchi wa chini kabisa.
Serikali haijawahi kuonja ugumu wa maisha kwa wananchi wake wao kwa vile wako normal life, hawana mawazo juu ya kula kwao kulala kwao na kuvaa kwao, huduma muhimu kama afya , elimu, maji si changamoto kwao , usafiri unawafuata hadi mlango wa chumba chao wao na watoto wao , hawawezi kujua namna gani mwananchi wa kule ihanga njombe anavyo pata 4,000 ya kununua sukari ambayo kiongozi wa serikali anaye pata kila kitu kwa urahisi ana nunua 4,000 hio hio huko dar es laam!