Hakuna kitu mbaya kinacho maliza pesa kama kununua vitu vidogo vidogo bila mpangilio,pipi, pombe, vyakula pasi na njaa, kumsaidia tu yoyote bila sababu za msingi, kununua tu viatu ilihali una pea za viatu vingine kama kumi na ni viatu vigumu tu, akili kubeba maoni yasiyo na tija, wewe ni mmoja kati ya wale wanaoamini kujenga ni mpaka uwe na Milion 100.
Jifunze kuweka akiba, tumia pesa ktk mahitaji ya msingi pekee na achana na mambo yasiyo na tija, rejea nyumbani mala tu utokapo kazini ili usiingie kwenye tamaa za Dunia ukiwa mitaani, mtengeneze mke awe mwenye uchungu na familia na maendeleo, akiweza utaona matumizi ya ndani ya elfu 50 per week, badala ya matumizi ya laki mbili per week... Tengeneza miezi yako ya kununua kimoja baada ya kingine, toka nje ya mji tafuta kiwanja nafuu nunua na anza ujenzi taratibu bila kuathili watoto wako swala la chakula na shule, pia hapo kwenye shule, usipeleke watoto kwenye shule ambazo zinakupa umasikini kwa sababu tu unataka watu wakuone umepeleka watoto shule za kulipia pesa nyingi,zenye raha ilihali watoto watakuja kuishi Afrika yenye majeraha yasiyo angalia mtoto alikula mkate shule na kubebwa na Coaster asbh na jioni, naweza kuendelea lakini naamini kwa uchache utakua umejua namaanisha nini.
N.B - mawazo yako yabebe kufanikiwa kimaisha, kutengeneza pesa na vyote unavyo vitaka maishani, utaona vinakuja kimoja kimoja maana utaweka bidii, achana na mambo ya Simba na Yanga huo ni upuuzi mkubwa unaokula muda wa waTanzania wengi mitaani