Habari.
Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama Kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite...Mshana Jr etc. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo.
1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3m. hapo Nina mkopo wa miaka 5 NMB.
2. Kazi nimeanza tangu 2012. Hivyo Nina miaka 9+ kazini.
3. Naishi Dar es Salaam.
4. Nina mke na watoto wanne. Mtoto wa nne bado ni kichanga.
5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda. Sina kiwanja Sina akiba. Bado nimepanga Kodi laki tatu kwa mwezi.
6. Mahusiano yangu na wife sio mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Lakini bado tunasonga.
7. Wife Hana kazi Hana biashara.
8. Nakunywa pombe mara kwa mara.
9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, etc
10. Sina gari. Nilioanza nao kazi Wana nyumba kubwa na magari mawili. Moja la wife....
Nahisi Nina mkosi nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale. Ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki Tano wametoboa mi nipo nipo tu mpka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni Binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Pole sana mkuu ila njia yako haina tofauti sana na yangu. Ili nikushauri naanza kujielezea mm kwanza.
Nimeanza kaz X 2018 kwa mshahara wa 1.8m haina makato na ikafika had 5.4m
Mshahara wote huo nilikua naona hautoshi kuanza maisha.
Siku moja nilienda mkoani nikaona walimu wa shule za msingi wana nyumba na pikpk wakati huo mm sina hata baiskel (hii kitu iliniuma sana)
Nikaamua kufanya maamuzi magumu nikanunua gari japo nilikua sina uhitaji wa gari ila nilitaka linichangamshe akili kidgo
Baada ya hapo nikaingia kwenye viwanja japo sina uhitaji wa kujenga pia.
Nikaamua kujiingiza kwenye majukumu yatakayonifanya niache kutumia hela vibaya (hapa nilifanikiwa sana, asikwambie mtu kumsaidia mtu especially ndugu na akasema asante hiyo kitu inaleta baraka sana).
Mwisho nikajikuta siipendi pombe kwasababu ya majukumu niliyojiwekea.
Narudi kwako sasa, unaonekana humuamini mkeo na wewe ni aina ya watu wa changu ni changu mtu asinipangie namna ya kutumia hela yangu.
Tenga pesa ya kumuachia mkeo yaani usiwe na shida ya chakula hapo nyumbani halafu inayobaki anza kununua assets (najua unaogopa atarithi mkeo kwa njia ya kitonga ila fanya hivyo kwaajili ya wanao)
Kuacha pombe ni ngumu sana ni sawa na kuanzisha kikundi cha waasi wakati hauna jeshi la kutosha.
Punguza marafiki hata ukienda bar nenda na hela inayokutosha ww tu usiweke mambo ya emergency kwenye pombe, pombe italamba emergency yote.