Maisha yangu baada ya miaka 37!

Mafanikio ya mwanaume yanakuja kama mwanamke alonae ana akili na anaweza kuyabeba matatizo tofauti na hivyo hauna mke una kiburudisho tu
 
Mkuu issue kubwa hapo ni kodi ya nyumba, hiyo 300k ni kubwa tafuta nyumba ya 100k afu 200k anza kusave utanishukuru baadaye
 
Hapa hamna mtu! Kwa maelezo yako unaonekana ni mtu usie jielewa! Ushauri wangu wa kwanza, TAFUTA KUJIELEWA KWANZA
Kwa ufupi wewe ni ZUMBUKUKU kuna watu mtaani hata hiyo million hawapati kwa mwezi na wanaishi vzr kuliko ww
 

Watoto 4. Mke hana kazi, Nina kunywa pombe Mara kwa Mara, mshahara 1.3, Nina mkopo, he he he

Usitafute mchawi, maelezo yako Yana majibu, labda niulize, huna nyumba, huna Gari, kodi laki 3, huo mkopo ulifanyania nini?
 
Njoo upitie [emoji1484] utakuja kunishukuru mkuu

 
Pole sana mkuu ila njia yako haina tofauti sana na yangu. Ili nikushauri naanza kujielezea mm kwanza.

Nimeanza kaz X 2018 kwa mshahara wa 1.8m haina makato na ikafika had 5.4m

Mshahara wote huo nilikua naona hautoshi kuanza maisha.

Siku moja nilienda mkoani nikaona walimu wa shule za msingi wana nyumba na pikpk wakati huo mm sina hata baiskel (hii kitu iliniuma sana)

Nikaamua kufanya maamuzi magumu nikanunua gari japo nilikua sina uhitaji wa gari ila nilitaka linichangamshe akili kidgo

Baada ya hapo nikaingia kwenye viwanja japo sina uhitaji wa kujenga pia.

Nikaamua kujiingiza kwenye majukumu yatakayonifanya niache kutumia hela vibaya (hapa nilifanikiwa sana, asikwambie mtu kumsaidia mtu especially ndugu na akasema asante hiyo kitu inaleta baraka sana).

Mwisho nikajikuta siipendi pombe kwasababu ya majukumu niliyojiwekea.

Narudi kwako sasa, unaonekana humuamini mkeo na wewe ni aina ya watu wa changu ni changu mtu asinipangie namna ya kutumia hela yangu.

Tenga pesa ya kumuachia mkeo yaani usiwe na shida ya chakula hapo nyumbani halafu inayobaki anza kununua assets (najua unaogopa atarithi mkeo kwa njia ya kitonga ila fanya hivyo kwaajili ya wanao)

Kuacha pombe ni ngumu sana ni sawa na kuanzisha kikundi cha waasi wakati hauna jeshi la kutosha.

Punguza marafiki hata ukienda bar nenda na hela inayokutosha ww tu usiweke mambo ya emergency kwenye pombe, pombe italamba emergency yote.
 
Unahitaji maombi...ila najua watoto nao Kuna gharama zake ila ningetegemea fasta fasta hapo ungekuwa na kiwanja na kigari kwa mbali..
 
Mkuu hii shule ya bei nyingi sana umetupa bure, asante sana
 
Shida inaanzia hapo kwenye 300k za kupanga...

Kingine ni mkopo huo wa miaka 5...

Anza na hayo 2 utaona mabadiliko...
Asante kwa ushauri. Kodi naweza kurekebisha ila mkopo ndo mpaka uishe.
 
Huna mkosi wowote, mchawi hapo ninahisi ni hiyo namba nane hapo. Pombe, Pombe, Pombe, Pombe....

Acha pombe ndugu yangu, baada ya miaka mitatu tu, utakuja hapa kunishukuru.
.
mkuu issue kubwa hapo ni kodi y nyumba hy 300k ni kubwa tafuta nyumba ya 100k afu 200k anza kusave utanishukuru baadaye
Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…