Prof Janabi wa JF
Senior Member
- Jul 7, 2023
- 165
- 450
Neno Marekani mtaliona sana tu, hadi nikirudi nyumbani. Ila leo niwape story kwa ufupi ili mjue safari zinaanzaje.
Kwanza mjue mimi ni kiumbe wa kutoka mkoani huko, sio Mdaslamu. Na nilikuwa sipapendi Dar nikaamini naweza toboa mkoani.
Mguu wa shingo mguu wa roho nikaingia sana vijijini huko kutafuta maisha. Nimepigika ile yenyewe hadi nikaona eekhe maisha ndio haya.
Unajua maisha ya kupambana kutafuta buku? Acha tu, unajichanga ukipata unakula kuangalia savings ikifika laki ujue kodi imekaribia. Hizo interviews za utumishi nishaenda sana, mnabadilishana namba na watu kila wakati ili tunapokutana tujue tunafanyaje. Dreams za wakati huo ni kuwa Banker, CV imechongwa kiutamu sana unaitwa kwenye interview ila mbele hutoboi.
Basi bwana, miaka kadhaa iliyopita, nikapata shavu ambalo lilitaka nije Dar. Muhuni nikatimba nikiwa na nauli tu.
Kupewa mkataba nikaomba hela ya kujikimu ili nijiweke sawa mjini. Nikapewa, nikatafuta dalali fasta, nitafutie chumba. Cha sh ngapi, nikamwambia kizidi 20k, nimejipa bei za mikoani kumbe Dar ni sehemu tofauti.
Basi siku hiyo dalali kaanza kunizungusha maeneo ya vyumba, nikasema mbona kama vymba vya Tsh 5k mkoani. Ikabidi nijibane nipande dau hadi 40k. Ndio nikapata chumba ambacho kwa wakati huo nililazimika kuridhika. Kipo uswazi kinyama ukitoka nje usiku unakuta watu wanakula msuba.
Mwanaume napewa funguo yangu mzee, nikaingia dukani fasta nikanunua ndoo kubwa moja, na ndogo moja kwa ajili ya kuogea, nikanunua mkeka(Ile ya plastic mikubwa), nikanunua mto, pazia, sufuria mbili, bakuli moja na sahani moja.
Nikanunua mwiko, kijiko kimoja na jiko dogo la gesi. Vitu vyote hivyo nikaweka kwapani nikahamia. Mwenye nyumba akashangaa sitoki, maana alidhani vitu vingine vitakuja labda na bajaji kumbe nilikuwa nishamaliza.
Mwanaume nikawa nalalia mkeka, oya, sio poa wanangu nilikuwa naumiza mbavu kinoma. Chumba kina joto kama motoni. Hela ya feni sina.
Kumbuka moja kati ya kitu nilikuwa siipendi Dar ni hilo suala la joto. Ila ndio nishapata kazi, ikabidi nikaze kibabe mtoto wa kiume.
Mimi ni mtu mkaksi sana, kwa hiyo japo wahuni walikuwepo kule mimi kidogo walikuwa wananiogopa. Kimsingi sura yangu haivutii, inaowavutia wananiambia imekaa kiume. Siku moja kuna binti wa chumba cha jirani alikuwa anarudi usiku wahuni wakawa wanamfuatilia, binti alipokaribia nyumbani akapiga kelele za mwizi, wakamfungulia mlango akaingia. Wahuni wakaja juu, "Wewe sisi tunakusindikiza wasikukabe unatuitia wezi" wakata wamfuate ndani. Nikasimama dirishani nikamwambia "Oya! Kausha" kwa sauti ya mamlaka wakajua tu huyu ndio yule mwanaume, wakakausha wakasepa.
Kimsingi sura yangu inaogopesha kama ukitaka kuniogopa ukishafahamiana vizuri na mimi unafurahi tu. Nilijua baadae sana kuwa naogopwa kwa sababu ya tembea yangu kujiamini na kuwa na maneno machache sana nikiongea na strangers.
Haikuchukua muda, maisha yalibadilika. Yalibadilikaje! Sio lazima ujue, cha msingi ni kwamba watu tunatoka mbali.
Nawasalimia kutoka Marekani.