Maisha yatakosa maana baada ya miaka 20 tu ijayo

2024 yetu ni 1990 ya Wazungu.

2045 yetu ni 2020 ya Wazungu.

Tunakoenda ujue kuna wenzetu wameshapita na Maisha kwao bado yana maana na kila mtu aliyekohuku anatamani kuishi huko ulaya.

Maisha yajayo ni mazuri na yenye maana zaidi kuliko haya ya Leo.
 
Sasa hivi watu wanajimilikisha mali hata viongoizi hawajali wengine ...Maisha tu ya leo mtu hana thamani mpaka awe na kitu , huko mbele ndio balaa kabisa .
Dunia ina system ya kuji reset, binadamu atafanya ufedhuli wee ufisadi, kukata miti, kuchoma ozone, oil spillage, pandemic za kuundwa, A.I, kuharibu maadili na mambo yote ila itafikia ku ji reset ianze upya tena!

Nafikiri huko kuji reset ndo tunachukulia kama kiama na tushakisogelea mno.
 
Ila sisi binafsi tukiamua kuishi katika kutokomeza umaskini kwa idadi ya watu waliopo inawezekana , kupunguza ubinafsi , kusaidiana kwa sana .

Dunia chini ya ubepari ni hatari sana .
 
Kwa bahati nzuri sana Leo taarifa ni nyingi..wababe pekee ndiyo wanaamua nini kuwepo
 
Labda kwa huko ulaya,Kwa Africa labda baada ya miaka500.
Kama sasa TU tunaishi Karne ya 17.je miaka20 baadae huoni kama ni karbu sana.
Sisi hata kupanda ndege ni hanasa na ni sherehe kwa familia
Umetazama kwa picha ndogo....hakuna kinachofanyika huko duniani ambacho hakiji kwetu. Tatizo lipo hapa.

Kama hatushiriki kwenye kuunda na kuweka sera basi sisi ndiye tutakuwa na mkwamo wa Kila kitu. Kwa sababu tunapokea Kila kitu.
 
Asilimia kubwa umeongelea hofu mfano mimi niko tayari kutengeneza familia kupitia IVF sio kosa sababu kupata mwanamke wa ndoa imekua ni ngumu sana
 
Asilimia kubwa umeongelea hofu mfano mimi niko tayari kutengeneza familia kupitia IVF sio kosa sababu kupata mwanamke wa ndoa imekua ni ngumu sana
Siyo kosa kwa Mujibu wa Sheria za wanadamu Lakini kwa Mujibu wa Sheria za Asili si sahihi
 
Extinction imeshaanza. Sixth extinction
 
labda ulaya uko lakini sio hapa Africa

au movie ya black panther imekudanganya mkuu

hizo sci-fi movies na mambo ya AI yata athiri uko magaharibi na sio Hapa kwetu sisi

ni primitive na tutastay hapo kizazi na kizazi
 
Tukipata muda vizuri tunaweza kujenga hoja kumi kumi Mimi na wewe then turuhusu wenzetu wachague....future ni mbaya narudia future ni mbaya
 
Kuna kipindi watu kama wewe walihofia kompyuta na hata smartphones
Hiyo siyo hofu ni prediction tu....haiondoi ukweli kwamba Madhara ya Tech ni makubwa kuliko faida when it comes kwenye maadili ya kijamii
 
Kumsomesha mtoto shule ya ada million 10 halafu akimaliza anauza matunda ni majanga.
 
Umetazama kwa picha ndogo....hakuna kinachofanyika huko duniani ambacho hakiji kwetu. Tatizo lipo hapa.

Kama hatushiriki kwenye kuunda na kuweka sera basi sisi ndiye tutakuwa na mkwamo wa Kila kitu. Kwa sababu tunapokea Kila kitu.
Hizo ni project za mabilioni,Dunia itajibalance,ipo hvyo Karne na karne.Hilo robot TU la akili mgando ni 60million above.We mshahara tu laki na nusu uezee wapi.DNA TU hapa ni tabu kupima,tunaishia kukubali kishingo upande watoto ambao ushahidi wa kimazingira si wetu.So still ni long journey mazee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…