Maisha yetu huendeshwa na Nyota?

Maisha yetu huendeshwa na Nyota?

Status
Not open for further replies.

dexterous

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
2,037
Reaction score
3,134
Mengi nimesikia kuhusiana na nyota binafsi bado niko njia panda juu ya hili kutokana na maelezo yake kua watu hutofautiana nyota kulingana na mwezi na tarehe ya mtu kuzaliwa pia tabia ya mtu inatokana na nyota yake ilivyo hata kazi pia hutegemeana na nyota.

Swali langu linakuja kwanin iwe ivo inamaana ikitokea mtu nyota yake inamtaka afanye kazi ya aina fulan inabidi afanye hata kama haipend ilimrad tu nyota yake inasema ivo au hata kwenye masuala mazima ya mapenzi mtu itabidi achague yule anaye endana kwa kuangalia nyota ili aweze kudumu nae.

Mbona kuna mambo unaweza ukafanya na ukaenza kudumu katika mapenzi.naomben mchango wenu juu ya hili.
 
Ni zaidi ya nyota kuna factor nyingi sana na nguvu zisizoonekana ambazo huyafanya maisha yawe hivi yalivyo, sehemu tunazotembelea, shule tunazosoma, maisha tunayoishi, watu tunaokutana nao vyote vina uhusiano mkubwa sana na nguvu zisizoonekana
 
ni zaidi ya nyota kuna factor nyingi sana na nguvu zisizoonekana ambazo huyafanya maisha yawe hivi yalivyo, sehemu Tunazotembelea, shule tunazosoma, maisha tunayoishi, watu tunaokutana nao vyote vina uhusiano mkubwa sana na nguvu zisizoonekana
kwahiyo hizo nguvu ndo zinaendesha maisha ya mwanadamu kwa hyo hta mafanikio ya mtu yana tokana na hizo nguvu?
 
Kuna mambo ya nyota ambayo yanahusiana kwa namna fulani na tarehe ya kuzaliwa. Waweza kukuta 70% au zaidi ni sawa. Waweza kutazama mambo ya nyota kama ziada ya saikolojia. Tatizo ni kwamba nyota inatabiri lakini si lazima iwe sawa kwa 100%. Lakini ukipata mtabiri mashuhuri si ajabu 70% au zaidi atakayo husisha na tarehe yako ya kuzaliwa kuwa ndio uhalisia wenyewe.
 
Nilickiza ushuda mmoja wa Mkenya ambaye alijiunga na freemasoni, anasema kwamba ni mbaya kwa mkristo kusoma nyota, kwani utabiri huo hutengwnezwa moja kwa moja kutoka katika nguvu za giza, na ikitokea wewe ni mtu ambae unasoma kila mwez/siku nyota yako, basi wewe utakuwa unaendeshwa moja kwa moja na nguvu za giza.

Hiyo yote ni shetani kutaka kupata wafuasi wengi,na hiyo nyota ili iendane na wewe,wao hutumia hesabu tuu ili kujua kipi kinachofuata katika maisha yako na hivyo vitu katika hujirudiarudia kuringana na hesabu tu.na ili kupata mtiririko mzuri ndoo maana wanaitaka tarehe na mwezi uliozaliwa.Mwney Macho asome mwenye masikio aelewe.
 
Kwa kuwa wengi wetu hatuna maarifa ya kutosha kuhusu nyota kuna uwezekano mkubwa wa kuburuzwa kwa kudanganywa.
 
Mengi nimesikia kuhusiana na nyota binafsi bado nko njia panda juu ya hili kutokana na maelezo yake kua watu hutofautiana nyota kulingana na mwezi na tarehe ya mtu kuzaliwa pia tabia ya mtu inatokana na nyota yake ilivyo hata kazi pia hutegemeana na nyota swali langu linakuja kwann iwe ivo inamaana ikitokea mtu nyota yake inamtaka afanye kazi ya aina fulan inabidi afanye hata kma haipend ilimrad tu nyota yake inasema ivo au hata kwenye masuala mazima ya mapenzi mtu itabidi achague yule anaye endana kwa kuangalia nyota ili aweze kudumu nae mbona kuna mambo unaweza ukafanya na ukaenza kudumu katika mapenzi.naomben mchango wenu juu ya hili

ushirikina at work.
 
Wale akina mamajusi walifuata nyota mpaka wakafika alipozaliwa mtoto yesu.

Elimu ya nyota ipo sahihi kabisa katika kutabiri ila biblia imekataza.

Hata maandiko ya kipindi kabla hajazaliwa kristo,maandiko ya biblia yalionyesha kuwa atazaliwa mwokozi, Hivyo basi hata mamajusi walisoma maandiko hayo na siku aliyozaliwa mwokozi ilikuwa ni kutimiliza maandiko.

Licha ya hayo lkn biblia inatukataza tusijihusishe na mambo ya nyota.Kwa hivyo basi nyota sii nzuri,kwa matumizi ya mkristo.
 
Mengi nimesikia kuhusiana na nyota binafsi bado nko njia panda juu ya hili kutokana na maelezo yake kua watu hutofautiana nyota kulingana na mwezi na tarehe ya mtu kuzaliwa pia tabia ya mtu inatokana na nyota yake ilivyo hata kazi pia hutegemeana na nyota swali langu linakuja kwann iwe ivo inamaana ikitokea mtu nyota yake inamtaka afanye kazi ya aina fulan inabidi afanye hata kma haipend ilimrad tu nyota yake inasema ivo au hata kwenye masuala mazima ya mapenzi mtu itabidi achague yule anaye endana kwa kuangalia nyota ili aweze kudumu nae mbona kuna mambo unaweza ukafanya na ukaenza kudumu katika mapenzi.naomben mchango wenu juu ya hili

Tafuta hii ukiwa YouTube Ushuhuda wa mtu ambae alikuwa akimuabudu Shetani Moses. Kazungumzia kidogo kuhuus nyota,utamwelewa na wala hautakuwa tena njia panda.
 
Mengi nimesikia kuhusiana na nyota binafsi bado nko njia panda juu ya hili kutokana na maelezo yake kua watu hutofautiana nyota kulingana na mwezi na tarehe ya mtu kuzaliwa pia tabia ya mtu inatokana na nyota yake ilivyo hata kazi pia hutegemeana na nyota swali langu linakuja kwann iwe ivo inamaana ikitokea mtu nyota yake inamtaka afanye kazi ya aina
fulan
inabidi afanye hata kma haipend ilimrad tu nyota yake
inasema ivo au hata kwenye masuala mazima ya mapenzi
mtu itabidi achague yule anaye endana kwa kuangalia nyota
ili aweze kudumu nae mbona kuna mambo unaweza
ukafanya na ukaenza kudumu katika mapenzi.naomben
mchango wenu juu ya hili

Mkuu hili swala la nyota ni kweli kabisa tunalo kama binadamu kila mmoja wetu amezaliwa na nyota mfano mm ni mkristo na biblia inaniambia wakti krito(yesu)anazaliwa ishara kumbwa ilitokea ambayoni nyota iliyong'aa sana na waganga na watabiri(mama jusi) waliona nyota ile na kutmbua kabixa kwamba aliyezaliwa si mtu wakawaida hivyo waliifuatilia nyota ili wajue maali alipo.

Pengine walitaka kumuibia yesu nyota lkn walipomuona wakajikuta wao wenyewe ndo wanatoa dhahabu na manemane kumtunza mtoto yesu..(ni maajabu haya) kwa kisa hiki kindhihirsha kabisa kila mtu ananyota na wachawi na waganga uiba nyota za watu ambazo zinang'aa coz hatufanani na wakishaiba uzifanyia biasha ndo unakuta mtu anautajiri wa kupuliza.

Hiyo anakuwa ameingia na mganga kutumia nyota za watu ambazo mganga aliziiba kwa ajiri hiyo ndugu ndio namna sheteni anavyofanya Kazi hiyo kuiba nyota za watu na kuwapa wale wenye tamaa ya utajir,tamaa ya kuwa mwasiasa maharuf na mengine..!! NInakushauri wewe muombe bwana yesu tu akulinde na adui shetani basi utakuwa salama kabixa wewe na nyota yako !
 
kwangu maisha yangu yanaongozwa na Mungu na sio nyota kama watu wanavyofikiri hivyo nakana kuwa maisha ya mwanadamu yanaongozwa na Mungu yeye ndo upanga awepo duniani au asiwepo amchukue hivyo ni vyema tukatambua hilo

Mengi nimesikia kuhusiana na nyota binafsi bado nko njia panda juu ya hili kutokana na maelezo yake kua watu hutofautiana nyota kulingana na mwezi na tarehe ya mtu kuzaliwa pia tabia ya mtu inatokana na nyota yake ilivyo hata kazi pia hutegemeana na nyota swali langu linakuja kwann iwe ivo inamaana ikitokea mtu nyota yake inamtaka afanye kazi ya aina fulan inabidi afanye hata kma haipend ilimrad tu nyota yake inasema ivo au hata kwenye masuala mazima ya mapenzi mtu itabidi achague yule anaye endana kwa kuangalia nyota ili aweze kudumu nae mbona kuna mambo unaweza ukafanya na ukaenza kudumu katika mapenzi.naomben mchango wenu juu ya hili
 
Rafiki acha nikujibu hivi ili uelewe "Ukristo ni nini" na mkristo ni nani?

Jibu:
Wakorintho wa kwanza 15: 1-4 inasema, "Tena ndugu zangu, ninawatangazia tena ile injili ambayo nimekwisha kuwahubiri ambayo mmeipokea nakusimama ndani yake; ambayo kupitia hiyo mmeokolewa mkiendelea kukumbuka yale niliyowahubiri msije mkawa mmeamini bure. Kwa kuwa niliwapatia kwanza kile nilichokuwa nami nimepokea, kwa jinsi ile Yesu aliyokufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na maandiko; na akazikwa, hatimaye akafufuka tena siku ya tatu kulingana na maandiko.

Kwa kifupi hii ndiyo imani ya kikristo. Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.

Wakristo huamini ya kuwa biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.

Wakristo huamini yakwamba mwanadamu aliumbwa ili awe na ushirika na Mungu lakini dhambi hutenganisha watu wote na Mungu (Warumi 5:12, Warumi 3:23). Imani ya kikristo hufundisha ya kwamba Yesu kristo alitembea juu ya ardhi akiwa Mungu kamili na huku akiwa pia mwanadamu (Wafilipi 2:6-11), na akafa msalabani. Wakristo huamini ya kwamba, baada ya kifo chake msalabani, Yesu alizikwa, akafufuka na sasa anakaa upande wa kuume wa Mungu Baba akiwaombea waumini milele (Waebrania 7:25). Imani ya kikristo inasema ya kwamba kifo chake Yesu kristo msalabani kilitosha kufidia dhambi za watu wote na hili ndilo linalorejeza ushirika baina ya Mungu na mwanadamu (Waebrania 9:11-14, Waebrania 10;10, Warumi 6:23, Warumi 5:8).

Ili uokolewe, sharti uweke imani yako juu ya kazi Yesu aliyoimaliza msalabani. Mtu akiamini kuwa Yesu alikufa mahali pa yeye ili amlipie gharama zake za dhambi na akafufuka tena basi mtu huyo ameokoka. Hakuna kitu mtu anachoweza kufanya mwenyewe binafsi ili aokoke. Hakun mwema wa kutosha kumpendeza Mungu kwa kuwa sote ni wenye dhambi (Isaya 64:6-7, Isaya 53:6). Lengine ni kwamba hakuna cha ziada maana kazi yote ilifanywa na kristo! Alipokuwa msalabani, Yesu alisema, "Imekwisha" (Yohana 19:30).

Kama vile haikugharimu chochote kuokolewa ila kuamini kazi iliyofanywa na Yesu msalabani vile vile hakuna kazi ambayo unahitajika kufanya ili upoteze wokovu wako. Kumbuka kazi ilifanywa na kumalizwa na yesu! Hakuna chochote kinachotegemea wewe mwenyewe katika wokovu. Yohana 10:27-29 inasema "Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na ninawajua na wao hunifuata. Nami huwapa uzima wa milele; nao hawatapotea wala hakuna awezaye kuninyang'anya kutoka mikononi mwangu. Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa kutoka mikononi mwa Baba."

Wengine hufikiria nakusema, "Nikiokolewa tu naweza kufanya kila nitakacho na wala sitapoteza wokovu wangu!" lakini wokovu si juu ya kuwa huru kufanya mapenzi yako. Wokovu ni kuwa huru kutoka kwa nyororo za dhambi ulizokuwa ukizitumikia iliuwe huru kumtumikia Mungu. Kadri waumini wanavyoishi duniani, kutakuweko na hali ya kupingana na dhambi katika miili yao. Kuishi na dhambi kunazuia ushirika na Mungu na muumini yeyote atakaye amua kuishi na dhambi hatafurahia ushirika wake na Mungu. Hata hivyo wakristo wanaweza kushinda dhambi kwa kulisoma na kulitumia neno la Mungu (biblia) maishani mwao na kuongozwa na Roho Mtakatifu – hiyo ina maana ya kujiachilia uongozwe na Roho katika kila shughuli ya siku na pia kupitia Roho uheshimu neno la Mungu.

Kwa hivyo, huku dini nyingine zikitaka waumini wao watende mambo Fulani Fulani au wasitende mambo Fulani ukristo ni juu ya kuwa na ushirika na Mungu. Deni lako la dhambi limelipwa na unaweza kuwa na ushirika na Mungu. Unaweza kuwa na ushindi juu ya maisha yako ya dhambi na ukatembea na ushirika na Mungu ukiwa mtiifu. Huwo ndiwo ukristo wa kweli unaoelezewa katika Biblia.

Hivyo ndivyo ukristo ulipoanzia na ndio maana ya mkristo ni nani nadhani mpaka hapo umeelewa na umefunguka una jingine la kuuliza hapo rafiki?



mkristo ni nani? na ni lini mlianza kuitwa wakristo?

usipanic njoo taratibu kuna somo leo utajifunza, naomba kudeclare mapema mimi siyo muislamu and over my dead body siwezi kuwa mwislamu.
 
Kwa wakristo BIBLIA TAKATITU imekataza kufuata utabiri wa nyota na mengine yafafananayo na hayo sijui kwa jirani zetu wa kibla

Tatizo lenu wakristo ni kutosoma biblia na kuielewa Yesu alipozaliwa nyota ya kung'aa ilionekana kwa wasafiri na ikawaongoza hadi mji alipozaliwa yesu. Biblia haikuchambua kwa kina juu ya nyota japokuwa wakati wa kuzaliwa yesu mamajusi wa mashariki walikwenda yerusalem Math. 2:1-2. Sasa niwaulize swali wakristo je, ile nyota inauhusiano gani na yesu? Au kabla ya kuzaliwa yesu nyota hazikuwepo?

Ukweli ni kwamba nyota zina uhusiano mkubwa na maisha yetu sisi wanadamu. Tatizo letu hatupendi kusoma na kuchunguza juu ya maisha yetu. Mungu aliturahisishia maisha yetu ili tuweze kumuabudu bila vikwazo tumeyafanya maisha yetu kuwa magumu ndo maana hata ibada zetu zimekuwa ngumu kwa sababu tumejipa uvivu wa kufikiri na kujifunza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom